Pekua/search

Friday, April 18, 2008

Mama Salma Kikwete aigwe. (Mchango zaidi)

Mjadala huu ni muhimu na hauwezi kufungwa kirahisi bila nasi wengine kutia timu.
Historia inaonyesha kuwa inahitajika utashi wa Kisiasa katika kuifanikisha hilo. Naomba ifahamike kuwa, hata Kiingereza kutumika kama lugha rasmi haikuwa rahisi kama tunavyofikiria. Kuna Wanazuoni, Maprofesa wa vyuo vikuuu walijiuzulu kwa kuwa tu Kilatini kilisitishwa kama lugha rasmi ya mawasiliano na kujipatia maarifa. Watu walikiona Kiingereza kuwa na mapungufu makubwa katika kujifunza na kwamba hakikuwa na misamiati ya kutosha kama ilivyo Kiswahili pengine kwa leo.
Lakini kwa upande mwingine naomba niwakumbushe kuwa lugha kama lugha inapitia hatua mbalimbali mithili ya kiumbe hai. Hivyo kadiri ya mahitaji na misamiati mipya, ndivyo itakavyotoholewa kwa kadiri ya mahitaji ya jamii na hatimaye kuwa na maneno maalumu. Hatupaswi kukata tamaa na kama neno halipo ina maana kuwa katika jamii hiyo hicho kitu hakifamiki. Endapo kitafahamika kitapewa jina.
Je, leo hii ni nani wanaongea na kutumia Kilatini kama lugha rasmi? Sina hakika kama kuna nchi zaidi ya Vatikano ambayo inakikubali na kukitumia Kilatini kama lugha rasmi katika mawasiliano na kufanyiwa tafsiri katika lugha mbalimbali. Lakini haina maana kuwa Kilatini hakipo na kwamba hakitumiki.
Ukipenda kitu chako utashawishi na wengine pia wakipende na kukutumia ndivyo utakavyoshawishi na wengine pia.
Inawezekana, timiza wajibu wako!

KISINDA,Octavius Alex
P O Box 13547
Dar es Salaam
Tanzania,The United Republic

Chanzo: Wanazuoni yahoogroup

0 comments:

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP