Pekua/search

Saturday, May 31, 2008

Mulinda; Msanii wa Injili aliyepania kuimba ‘Live’

KARIBU kila fani hapa nchini, kwa njia moja au nyingine imewahi kulalamikiwa kuvamiwa na wababaishaji ambao hufanya kazi au kutoa huduma zisizokidhi haja kwa walengwa, wala ubora wa bidhaa husika.

Uimbaji wa nyimbo za Injili ni miongoni mwa fani ambazo licha ya kwamba ni burudani, ni ajira ambayo huifanya fani hiyo ithaminiwe na hivyo mazingira hayo kuvutia baadhi ya watu wasio waaminifu.

Katika siku za hivi karibuni, kumekuwapo na ongezeko kubwa la waimbaji binafsi wa nyimbo za Injili ambao kwa majira na maeneo tofauti wamekuwa wakizindua albamu zao kwa kuufahamisha umma kuhusu kazi zao.

Pamoja na mambo mengine, wageni wa heshima katika matamasha hayo ya uzinduzi wa albamu hizo, wamekuwa wakitoa changamoto mbalimbali pindi wanapotakiwa kutoa nasaha zao katika hafla hizo.

Akinukuliwa na vyombo mbali mbali vya habari mapema mwezi uliopita katika tamasha la uzinduzi wa albamu ya Mwimbaji Vita Kissi Tabata Segerea Dar es Salaam, mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya African Evangelical Enterprises (AEE) aliwataka wasanii wa nyimbo za Injili nchini kuwa waadilifu ili kuepusha uwezekano wa kuwepo vitendo vya kifisadi katika fani hiyo.

Aidha, akitofautisha uimbaji wa nyimbo za Injili na zile za bongofleva, mkurugenzi huyo alisema, tofauti na nyimbo za ‘bongofleva’ jukwaa la nyimbo za Injili ni eneo ambalo huhitajika uadilifu kutokana na umuhimu wa huduma hiyo kwa jamii.

Pamoja na kwamba fani hiyo ni ajira, Masangakulangwa alikemea tabia ya baadhi ya wasanii wa nyimbo za Injili hapa nchini kufanya huduma zao kibiashara zaidi kuliko kihuduma.

Fredrick Mulinda mkazi wa Mbezi Dar es Salaam ni msanii chipukizi wa nyimbo za Injili nchini ambaye amerekodi albamu yake ya kwanza yenye nyimbo kumi hivi karibuni.

Mapema akizungumza na safu hii, mwishoni mwa wiki Dar es Salaam anasema, albamu hiyo inakwenda kwa jina la Moyo wangu, na kwamba alirekodia studio ya Don Bosco ya Upanga Dar es Salaam. Anasema, albamu hiyo ipo katika mfumo wa CD na Audio (kaseti) ambayo wakati wowote itaingia sokoni katika kukosha nyoyo za wapenzi wa nyimbo zenye mahadhi ya Injili ‘gospel flavor’.

Msanii huyo ambaye anatokea katika familia ya kidini anasema, yeye na washauri wake wapo katika dakika za mwisho mwisho kwani anatarajia kuingia sokoni katika jukwaa zima la nyimbo za Injili ndani na nje ya nchi kwa ‘staili’ ya tofauti.

Mulinda, ambaye kitaaluma ni mwanasayansi wa Afya ya Mazingira aliyehitimu katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Muhimbili (MUCHS) anasema, mashabiki na wapenzi wa nyimbo za Injili wakae mkao wa kula kwani dhamira yake ni kufikisha ujumbe unaobadilisha tabia na hali duni za watu na hajaweka kipaumbele cha kutafuta pesa.

Anasema, lengo la msingi la kuimba katika maisha yake kwanza ni kujitokeza hadharani ili kipaji chake alichokifanyia majaribio kwa miaka mingi kiweze kuonekana na pili matokeo ya kipaji hicho iwe ni fursa ya kipekee kuifikishia jamii ujumbe wenye maudhui mbali mbali sambamba na kumtumikia Mungu.

Kihistoria msanii huyu anaonekana tofauti kidogo na wenzake katika fani hiyo kwa sababu kipaji chake kililelewa vema na baba yake mzazi Fulgence Mulinda (sasa marehemu) aliyekuwa Askofu wa Kanisa la Pentecostal Holliness Mission (PHM) Jimbo la Kagera kwa zaidi ya miaka 15 iliyopita.

Kama hilo halitoshi, Fanuel Mulinda ambaye ni kaka yake wa kuzaliwa, ni Mchungaji ambaye na yeye amejaliwa kuwa na kipaji cha kuimba cha aina yake na hivyo ‘kumpiga msasa’ mara kwa mara ili ang'ae katika medani ya nyimbo za Injili.

Mulinda anasema anawashukuru wahisani mbalimbali waliofanikisha kurekodi albamu yake hiyo kwani msanii kufikia hatua ya kurekodi katika hali ya kawaida huwa ni jambo la kutia moyo na linaloonyesha wazi kuwa msanii husika yupo makini katika kazi yake.

“Kusema kweli tangu mchakato wa kutoa albamu hii uanze miezi kadhaa iliyopita nilikutana na misukosuko ya hapa na pale ambayo huwa haikwepeki kutokana na hasa ufinyu wa bajeti ya kufanyia shughuli hiyo, lakini hii ni changamoto kwangu ili nijipange zaidi kwa albamu nyingine zijazo Mungu akitujalia,” anasema.

Anasema, anachokifanya hivi sasa, ni kuendelea kumuomba Mungu malengo yake yatimie kama alivyopanga, hatimaye azalishe nakala nyingi kadiri iwezekanavyo na kuzisambaza kwa wateja. Katika albamu hiyo amewashirikisha waimbaji watatu ambao ni Nicodemus Shaboka wa CAG Urafiki, Angel Bernard (Amana Vijana Center) na Hossiana Masang'ula (PHM Salasala) wote wa Dar es Salaam.

Mulinda hakuibuka hivi hivi, hadi kufika hapo alipo sasa, kapitia maeneo mbali mbali ambayo yalikuwa ni shule tosha kwake hadi kufaulu kuwa mwimbaji chipukizi wa ‘gospofleva’ anasema, mwaka 1995 hadi 1998 akiwa Ihungo Sekondari Bukoba Mjini akiwa na kikundi cha Voice Boys Fellowship (VBF) ndipo nyota yake ilipoanza kun’gara kiuimbaji.

Anasema, kundi la Voice Boys Fellowship lililokuwa na vijana 25 yeye alikuwa tegemeo kwao kwani kwa kiasi fulani aliwasaidia katika kuwafundisha kuimba kwa ustadi unaotakiwa. Anasema, upako wa uimbaji ulimsukuma hadi alipomaliza shule hapo Ihungo sekondari hadi alipojiunga na Mkwawa High School ya Iringa mwaka 1999 hadi 2001.

Iringa Pentecostal Youth Association (IPYA) ni kikundi kingine ambacho baada tu ya yeye kujiunga kama mwanachama muda mfupi tena kipaji chake kilionekana kun’gara, jambo lililosababisha apewe wadhifa wa kuwa mwalimu wa kwaya shuleni hapo wakati huo ikijulikana kama Agape kwaya. Agape kwaya wakati huo ikiwa na waimbaji watano, ilikuwa chini ya uongozi wake, walitunga nyimbo saba ambazo kati ya hizo, wimbo wa “Mwokozi Yesu ninakupa sifa ulikuwa unaongoza”.

“Kikundi kile kwa kweli kilikuwa ni wamisionari ambao tulikuwa tukipeleka huduma ya uimbaji na neno la Mungu katika makanisa na jamii ya watu mbali mbali popote tulipoalikwa mkoani Iringa,” anasema. Mulinda anamtaja Cyprian Gabriel kama swaiba wake wa karibu ambaye alikuwa naye bega kwa bega katika kuhakikisha kuwa, Agape kwaya inakosha nyoyo za wasikilizaji, hasa watu wa Mungu mkoani Iringa kwenye mikutano na makongamano mbali mbali.

Anasema, alipomaliza masomo Mkwawa High School, ulikuwa ndio mwanzo wa kuingia katika zama mpya kiuimbaji kwani mwaka 2002 hadi 2005 akiwa Chuo Kikuu Kishiriki Muhimbili (MUCHS) alikutana na hamasa tofauti tofauti kutoka kwa vijana wenzake wenye kipaji cha kuimba kama yeye, jambo lililompa msukumo zaidi katika kutaka kutimiza ndoto zake katika fani hiyo.

Akiwa MUCHS kati ya mwaka 2005 na 2006 ndipo mazingira yalipomruhusu kutimiza ndoto zake kwa njia yoyote, jambo lililomfanya aanze kuwa na muda wa kutosha kutulia mbele za Mungu kwa ajili ya maelekezo maalum baada ya kumaliza masomo yake.

Anasema, mapema mwanzoni mwa mwaka huu alianza rasmi kukusanya nyimbo zake na hatimaye akafanikiwa kurekodi albamu yake hiyo. Matarajio yake ni kuwa na kikundi kitakacholeta mapinduzi katika fani ya uimbaji kwa kuondoa mfumo wa kuimba kwa kutumia CD na badala yake kuimba ‘live’.

Mulinda amefunga pingu za maisha na Lucy Kyombo mapema mwaka jana, wamejaliwa kupata mtoto mmoja anayeitwa Michael mwenye miezi miwili sasa.

Msanii huyo ni mtaalamu wa mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) wakati mkewe ni muuguzi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wanaishi Mbezi Dar es Salaam.

CHANZO:
Innocent MallyaDaily News; Friday,May 30, 2008 @20:05

Friday, May 30, 2008

MJADALA WA ADVANCED DIPLOMA VS HIGHER DIPLOMA

AMANI IWE NANYI WANAZUONI JADIDI.
NDUGU BAKARIUMEFANYA VEMA KUANZISHA MJADALA HUU.

MFUMO WA ELIMU NCHINI UTAELEWEKA NA KUWA NA MAANA PALE TU SERA ZITAKAPOTUNGWA NA WANANCHI ( KWA NJIA SHIRIKISHI). HIVI SASA TUTAENDELEA KUTUMIKIA MIUNGU TUSIOIJUA, KWANI SERA ZETU NYINGI ZINATUNGWA NA 'WAGENI'.MUNGAI ALIWEZA KULALA NA KUAMKA, HIKI KIKAWA, KILE NA KILE VIKAFUTWA. MSOLA VIVYO, HATA KABLA HAJALALA, ADV.DIP IKAWA IMEFUTWA NA HAYA DIPULOMA INAKUWA.MAGHEMBE KAJA NA YAKE, TENA KWA KASI KULIKO KIPANGA,ETI KIINGEREZA IWE LUGHA YA KUFUNDISHIA KUTOKA MSINGI HADI VYOO VIKUUBWA.TOBA! !! WALIMU TUNAOPATA SHIDA KUFUNDISHA KWA KISWAHILI, TUTAWEZA KUFUNDISHA VIZURI ZAIDI KWA KIINGLISHI, MUNGU WANGU!! HIVI HAWA WADHEE WANATUMIA NINI KUFIKIRI? AU VISIGINO NA SIO UBONGO!!!TUNATUMIKIA MIUNGU TUSIOIJUA NDUGU ZANGU. HAYA MAAMUZI YA MTU MMOJA KUFUMBA NA KUFUMBUA YATAENDELEA KUTULIZA NA KUTUMALIZA. LAZIMA UWEPO MFUMO WA KUSHIRIKISHA WADAU WENGI NA KUZINGATIA MAWAZO NA MITAZAMO ANUAI YA WADAU HAO. HUU MWENDO WA SASA WA WANASIASA KUFANYA KILA KITU NI BALAAA TUPU.NCHI WALA KWA NIABA YETU, NA KUFIKIRI WAFIKIRI KWA NIABA YETU???

JAMANI, TUMENENA SANA, NA ADA YA MJA KUNENA, MUUNGWANA KUTENDA. SASA NATWENDE MITAANI.NAPENDEKEZA , TUSIWE WAPOLE KWA MASUALA YA MUSTAKABALI WA TAIFA LETU.JAPO ULINGO WETU HUU SI RASMI, TUNAWEZA KUJIPANGA KUHAMASISHA MAANDAMANO KATIKA TAASISI ZA ELIMU, WALAU YA JUU, TWENDE MTAANI.TUFANYE MAANDAMANO YA AMANI.DUNIA ISIKIE JAMANI. KWA KWANZIA NAPENDEKEZA MASUALA HAYA MAWILI.TUDAI SERIKALI ITOE MAELEZO YANAYOELEWEKA KUHUSU KAULI ZAKE JUU YA ADVANCED DIPLOMA NA HILI LA KUFUTA KISWAHILI USWAHILI!!!! JAMANI SI DHAMBI. NCHI NI YETU, ALAH!NA SISI NDIYO WANA WA NCHI WENYEWE. TUNAPASWA KUJIRIDHISHA PASIPO SHAKA KUWA MAAMUZI YANAYOFANYWA NA SERIKALI YANAKUWA NA TIJA KWETU NA VIZAZI VIJAVYO, LA SIVYO WANAZUONI TUDAI, TUDAI, TUDAI NA KUDAI UFAFANUZI NA TUSHAURI NA KUSHINIKIZA NJIA MBADALA.NAWASILISHA.
ADAM
Arusha.

--- In wanazuoni@yahoogrou ps.com, "Kiula Kiula" wrote:>>

Amani kwenu wandugu,> > > >
Ninaomba kukosolewa kama nitakuwa nje ya mstari. Advance Diploma ipo juu> kuliko Higher Diploma. Kwa mujibu wa mdau mmoja kutoka NACTE ni kwamba> baada ya kuiphase out Advance Diploma nafasi yake itachukuliwa na Higher> Diploma. Ordinary Diploma itabaki kama kawaida. Kwa mujibu wa NACTE> mambo yatakuwa hivi; Unapotoka A- Level au kwingineko na kujipatia> Ordinary Diploma basi utapaswa pia kusoma Higher Diploma (wanasema kwa> muda mfupi ila sijui ni muda gani), hii Higher Diploma ndiyo itakayokupa> sifa ya kusoma Bachelor Degree.> > > > Asubuhi adhimu.> >

From: wanazuoni@yahoogrou ps.com [mailto:wanazuoni@yahoogrou ps.com] On> Behalf Of BAKARI ISSA> Sent: Monday, May 26, 2008 5:30 PM> To: ethinktanktz@ yahoogroups. com; techtz@yahoogroups. com;> wanazuoni@yahoogrou ps.com> Subject: [wanazuoni]

ADVANCED DIPLOMA Vs HIGHER DIPLOMA COURSES> > > >

habari za kazi na harakati za kulihudumia taifa kwa ujumla> > Naombeni nitumie muda wenu kidogo kulijadili swala hili ili kichwa> changu kipate utulivu kidogo> > "Juzi nliskia kuwa mh. waziri wa elimu ametangaza kwamba wale> waliotayari ndani ya mchakato wa advanced diploma wao watatambulika na> wale wanaoaply sasa wasifanye application for advanced diploma kwani> hazitotambulika kwao"> > ila pia kuna mchakato wa higher diploma ulio vichwani mwetu ambao ndio> utakao replace advanced diploma sasa ninachohitaji kujua ni kama> yafuatayo> > 1: Vyuo karibu vyote vilivyokuwa vinatoa Advanced Diploma naona sasa> vinaendelea kutoa applications for the new intake 2008/09 based on> advanced diploma sasa sijui baadae itakuwaje> > 2: ni vyuo gani vinavyotoa higher diploma? maana nimejaribu> kufuatilia kwa uwezo wangu bila mafanikio> > 3: Je mitaala iliyokuwa ikitumika kwenye advanced diploma ndio> hiyohiyo itakayotumika kwenye higher diploma?> > 4: Vipi system ya elimu ikoje? maana wakati wa mheshimiwa mungai> mambo yalichange kabisa sisi tukiwa kama mfano nikiwa form six 2005> tukalazimika kufanya mtihani mwezi wa tatu badala ya mwezi wa tano, na> mifano mingi iko wazi kwa wanaofuatilia sasa kuna higher diploma Vs> Advanced diploma naomba ufafanuzi zaidi wenye kina na mashiko nadhani> hapa ndio kwenye solution> > > >
BAKARI ISSA> > 3rd Year Student > >
ADvanced Diploma in Computer Science> > Institute of Finance Management (IFM)> > +255 756 876534> > P.O.BOX 77094> > DSM

Chanzo: wanazuoni yahoogroups

SULLIVAN YATIKISA TANZANIA NZIMA


MKUTANO wa kimataifa wa Leon H. Sullivan VIII umekuwa gumzo Tanzania nzima!
Pichani ni bango la kuhamasisha likiwa limewekwa eneo la Uyole katika jiji la Mbeya kusini magharibi mwa Tanzania.

Thursday, May 8, 2008

Mfano rais Truman kwa Wanasiasa wa Bongo

Amani iwe nanyi.
Na kwa yakini, mheshimika Truman alikuwa sahihi. Hakuna tofauti kati ya kazi mbili alizochagua; uanasiasa na upiga mziki kwenye 'danguro,. Ndiyo maana Mh. Lower sir na Chen ge wanaibuka mashujaa majimboni mwao na katika chama chao (kwa viongozi wa chama kuwaandalia mapokezi mazito, kana kwamba wametoka vitani!) na upande wa pili Dkt. Mwakyembe, alizuiwa na viongozi wa chama chake (wa ngazi sawa na wale wanaoandaa mapokezi kwa watajwa hapo juu) kushiriki maandamano yaliyoandaliwa na wananchi kumpongeza na kumfariji baada ya kutijotaa mhanga na 'kujilipua' bungeni. Uongozi wa CCM mkoa wa Mbeya uliripotiwa kujaribu kumzuia asishiriki mapokezi ya wananchi kwa madai ya maelekezo kutoka ngazi za juu za chama hicho. Sasa sijui na mapokezi ya kina Lowasa na Chenge, ni maelekezo ya CCM ngazi za juu??? JE BADO CCM NI MOJA?? JE CCM BADO KIPO?

Wenzetu mnaokuwepo kuushuhudia 'utitiri' wa watu kwenye mapokezi hayo, tujuzeni, MWAANDAAJI NI NANI??? Haitoshi kutuambia kwenye vyombo vya habari kuwa watu walifurika kumpokea shujaa 'pengine wa kifisadi'. Twambie jamani, iliitwa na nani kadamnasi hiyo? Kama watu walizuka tu kama madume ya mbwa yamtokeavyo mbwa jike aliyetayari kupandwa, napo mtwambie. Kama wananusa tu, kuwa shujaa wao anashuka eapoti saa fulani na haraka haraka wanajikusanya kama tai wauzongavyo mzoga, si vibaya tukaambiwa pia.

Hata Kama mhusika, ndiye anayeandaa ili kupata fursa ya kuwagawia vijisenti vya 'kifisadi' wapiga kura wake, napo tuambiwe ati!!TUJUE,kwani TUSIJE PIGA KELELE KUMBE WANAJIMBO na CHAMA HUSIKA NDIYO WALIOWATUMA WAHESHIMIWA HUSIKA KUIFISIDI NCHI, NA NDIPO BAADA YA MAFANIKIO WANARUDI MAJIMBONI KUSHEREHEKA NA WATU WAO!!TUJUE MUKTADHA WA MATUKIO HAYA KUTOKA PANDE ZOTE. KUTUAMBIA MHESHIMIWA ALIVAA SUTI GANI, TAI NDEFU AU FUPI, ALIONGOZA NA MKEWE AU KIMADA, BI MKUBWA AU MDOGO,(kama msomi mmoja alivoandika habari za lowasa) HAITUSAIDII SANA.

WANASIASA WATU WAAJABU. Mathalan, si ajabu Chen ge, ALIJIUA maksudi ili apate agenda ya kutambia jimboni kwake. "Mnyantuzu hawezi kujiua aache vijisenti vyake" ndivyo yalivyo mnukuu magazeti ya leo. Kwa hiyo yaweza kuwa yeye na wapendwa wake, alipanga maigizo haramu. Akajiua. akaonewa huruma. akageuza mjadala, Dar hadi jimboni kwake, na Tanzania nzima. Hoja kwa wapiga kura wake, imekuwa si kutuhumiwa ufisadi, bali kuzushiwa kifo!!!Kutotakiwa mema.Kuandamwa kisiasa. (NANI ANAMWANDAMA? KISA NINI? WAMEANZA LINI KUMWANDAMA? YEYE KAWAANDAMA WANGAPI?). SIASA BWANA!!!

CHENGE anakwenda kwa wapiga kura wake kuwaambia yaliyomtokea ni nasema NI AJALI YA KISISA!! Hii ni dharau ya hali ya juu. je hii si kejeli ya mara ya pili kwa JK baada ya kuwajibu jeuri waandishi, "KAMUULIZENI ALIYENITEUA" . Sasa anakariri maneno ya JK huyo huyo, alipokuwa akijaribu 'kumtetea' swahiba wake Lowasa mbele ya wazee wa jiji la Dar es Salaam.(Lakini wacha JK AKOME!!MAANA UKING''ANG'ANIA KUBEBA ZIGO LA MAVI, LAZIMA UKOME. HARUFU YAKE SI MCHEZO, ATI!!)Wacha JK anyooshwe!! kwani maandiko matakatifu yanabainisha, "MTU AKISHUPAZA SHINGO, HUVUNJIKA GHAFLA"

WALAU, CHENGE angejitetea kwa wapiga kura wake kwa kueleza alivyopata vijisenti vyake (hana haja kusubiri SFO wampe madokezo), na ni kwanini ameviweka nje ya nchi kimya kimya, wakati hata Bariadi au Shinyanga benki zipo (na kama hazipo vijisenti hivyo vingeweza kusaidia kuwa mtaji wa benki ya 'wanyantuzu' ! Sasa anaenda jimboni kupeleka kejeli!!. AMA KWELI, 'MUNGU HUWAPIGA UPOFU WENYE DHARAU, MAJIVUNO NA KIBURI'.

SIJARIBU KUMHUKUMU CHENGE, LAKINI HAKIKA NI AFADHALI KUSIKILIZA wimbo "Jini jini anipenda sana, anasema ananipenda.. . au hata zaaaaali la mentali..ama mabinti wa kitanga na kujipamba kwao" tukaburudisha nyoyo, KULIKO KUSIKILIZA porojo zake CHENGE na nduguze.

AHSANTE NDUGU KISINDA KWA KUMUVUZISHA KA INSIGHT HAKA KUHUSU MAISHA YA MODO TRUMAN. I COULDNT RESIST IT THIS MORNING, SASA WALAU, NAWEZA KUENDELEA NA KAZI.TRUMAN IS TRULY A GREAT INSPIRATION! !!!

Adam, L

--- In wanazuoni@yahoogrou ps.com, Mgune Masatu wrote:

Fewer are like Him.

Octavius Kisinda wrote:
FYI

Harry Truman....proof that there is some good men in the World.......

Harry Truman, Former President of US When President Truman retired from office in 1952, his income was substantially a U.S. Army pension reported to have been $13,507.72 a year. Congress, noting that he was paying for his stamps and personally licking them, granted him an "allowance" and, later, a retroactive pension of $25,000 per year.

When offered corporate positions at large salaries, he declined, stating, "You don't want me. You want the office of the President, and that doesn't belong to me. It belongs to the American people and it's not for sale."

Even later, on May 6, 1971, when Congress was preparing to award him the Medal of Honor on his 87th birthday, he refused to accept it, writing, "I don't consider that I have done anything which should be the reason for any award, Congressional or otherwise."

We now see that the Clintons have found a new level of success in cashing in on the presidency, resulting in untold wealth. Today, many in Congress also have found a way to become quite wealthy while enjoying the fruits of their offices. Political offices are now for sale.

Was good old Harry Truman correct when he observed, "My choice early in life was either to be a piano player in a whorehouse or a politician. And to tell the truth, there's hardly any difference".

NB: I, for one, believe the piano player job to be much more honorable than current politicians. What do you say????

Source: wanazuoni yahoogroup

Wednesday, May 7, 2008

KANUNI MUHIMU YA BUNGE IWAPAYO NGUVU WANANCHI (LAKINI HAITUMIKI!!!!)

Amani iwe juu yako..
MOTO MKUBWA HUANZA KWA CHECHE” Alhaj Ali Hassan Mwinyi.


Hapa chini nakuleteeni nukuu ya kanuni moja ya Bunge kama ilivyowasilishwa na Dkt. Wilbroad Slaa, hivi majuzi (Mei 2, 2008) kwenye mdahalo wa ulingo wa maendeleo hapa mjini Arusha.

“Kanuni ya 34 ya Kanuni za Bunge inatoa nafasi adimu sana ambayo katika Bunge letu haijawahi kutumika tangu uhuru kwa vile si Wabunge au Wananchi wanaoielewa vizuri kanuni hii. Kanuni hii inatamka ifuatavyo, ‘Mbunge yeyote anaweza kuwasilisha Bungeni maombi kuhusu jambo lolote kwa niaba ya watu wanaotoa ombi hilo…’ Ombi la aina hii linachukua nafasi kubwa Bungeni, na linachukua nafasi ‘precedence’ kuliko hata shughuli za Serikali. Matakwa pekee ni kuwa lazima liwe limewekewa saini na Wananchi (Wasiopungua 200) wenye kutaka ombi hilo liwasilishwe, na mbunge asiwe na maslahi yoyote na ombi hilo yeye mwenyewe. Hii ni nafasi muhimu sana, kama ingeliweza kutumika. Inahitaji uelewa mkubwa, ujasiri wa wananchi na wananchi kutokuwa na uwoga katika kutafuta na kudai haki zao.” Alisema


Je, hapo hapawezi kuwa mahali pa kuingilia ikizingatiwa hii ni kanuni ya Bunge, si ya chama chochote? Je tuendelee kungoja utashi wa wabunge kuwasilisha ‘hoja’ binafsi? Je inatosha wananchi waendelee kuwalaumu wabunge kwamba hawasikilizi kero zao?

Dkt. Slaa anasema, “Inahitaji uelewa mkubwa..”
Nani atawajengea uelewa mkubwa wananchi? Mimi nimekutumia wewe mbiu hii (bila kujali iwapo unajua au la), ni vema ukiimuvuzisha zaidi….
Wasalaam,
Adam, L

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP