Pekua/search

Saturday, October 4, 2008

RAIS KIKWETE AWAJIBIKE KWA KUAHIRISHA ZIARA MBEYA??

AMANI IWE KWENU WAPENDWA WANAZUONI.

Jana nilichangia hoja za ndugu Maro kuhusu kuahirishwa kwa ziara za Rais mkoani Mbeya. Baada ya hapo nimeendelea kulifuatilia jambo hili na kulitafakari zaidi.Mwanzo nilidhani Mkuu wa Mkoa wa Mbeya John Mwakipesile alikuwa na wajibu wa kueleza ukweli juu ya kuahirishwa kwa ziara ya rais mkoani humo kwani sababu alizozitoa hadharani kwa vyombo vya habari kuwa rais hakwenda mbeya kwa vile kulikuwa na mtihani wa darasa la saba na kwamba ulikuwa mwezi mtukufu hazina mashiko (ippmedia.com/ ipp/nipashe/ 2008/09/19/ 122887 .na http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/17107-kikwete-aahirisha-ziara-ya-mbeya.html.

Sababu hizo hazina mashiko kwa vile kwanza licha ya Mwezi mtukufu wa Ramadhani na mtihani wa darasa la saba rais aliendelea na ziara mahali pengine. MATHALANI ALITEMBELEA MKOA WA MANYARA WAKATI WA MFUNGO HUO HUO ULIODAIWA KUMZUIA KWENDA MBEYA (http://www.ippmedia.com/ipp/radio1/2008/09/10/122313.html).

KUTOKANA NA KUKOSA NGUVU KWA SABABU ZA MKUU WA MKOA WA MBEYA, NADHANI NI SASA WA KUWAJIBIKA NI RAIS MWENYEWE. KWANZA AWAJIBIKE KWA KUWACHUKULIA HATUA WALIOUNDA UZANDIKI NA KUSEMA UWONGO HADHARANI KWAMBA RAIS HAFANYI ZIARA MIKOANI WAKATI WA MWEZI MTUKUFU.WAMEMDHALIL ISHA. AWAADHIBU. LA SIVYO BASI RAIS AELEZE WAZI WAZI NI KWANINI HAKWENDA MBEYA KWA TAREHE ZILIZOPANGWA.

NAWASILISHA.
ADAM, L
BOX 16335
ARUSHA, TANZANIA

http://uk.mc254.mail.yahoo.com/mc/compose?to=lingsadam@yahoo.co.uk
http://www.upolesana.blogspot.com/ --- On Fri, 3/10/08, lingson adam wrote:
From: lingson adam Subject: Re: [wanazuoni] JK KUSAFIRI TENA (NINI TATIZO LA MNETE ???)To: wanazuoni@yahoogrou ps.comDate: Friday, 3 October, 2008, 12:53 PM
Ndugu yangu Maro nashukuru kwa majibu yenye kuzalisha maswali mengi zaidi.

Ila utanisamehe kwa vile MOYO WANGU UMEKATAA KUAMINI KWAMBA SERIKALI YA JK IMEJAA HOFU NA IMANI ZA AJABU AJABU HATA VIONGOZI WAKE WAOGOPE KUTEMBELEA MAENEO KADHAA ETI KUHOFIA 'KUDHURIKA.' Pamoja na kwamba umemwita Mwandosya rais wa mkoa wa Mbeya, ni wazi hana majeshi huko. Hicho wanachoogopa hao viongozi wakuu ni kipi ambacho vyombo vyote vya ulinzi na usalama vinashindwa kudhibiti??? KWA HISTORIA NAFAHAMU WATU WAMKOA WA MBEYA NI WATIIFU SANA. NA REKODI ZINAONYESHA KWAMBA JK ALIPATA KURA NYINGI ZAIDI MKOANI MBEYA. HAIINGII AKILINI KWAMBA WATU WA MKOA WA MBEYA WANAWEZA KUWA NA KISASI NA JK SASA, MAANA WANGEKUWA NA HASIRA NAYE BASI WANGEMNYIMA KURA ZAO. LABDA TUSEME YEYE JK NDIYE MWENYE KISASI NAO??? LAKINI KWA LIPI???? naulisaaaaaa! !!!!!!!!! !!!!!

kama kweli viongozi wakuu wa kaya hii wanaogopa kwenda mbeya kwa sababu yoyote ile, BASI WANAOGOPA VIVULI VYAO TU. NA BASI BORA TUKAUSIMIKA MTI, KISIKI AU MLIMA WOWOTE UTUONGOZE KULIKO WALONGOZI WAOGA NAMNA HIYO!!!!!!!!
sitaki kuamini kirahisi

Kaka Maro, na HILI LA SUDI MNETE??????? ????????? ????????? ?????? Naamini ukipata muda utalitolea ufafanuzi.

NAWASILISHA.
ADAM, L
BOX 16335
ARUSHA, TANZANIA

http://uk.mc254.mail.yahoo.com/mc/compose?to=lingsadam@yahoo.co.uk
http://www.upolesana.blogspot.com/ --- On Fri, 3/10/08, Yona Fares Maro wrote:
From: Yona Fares Maro Subject: Re: [wanazuoni] JK KUSAFIRI TENA (NINI TATIZO LA MNETE ???)To: wanazuoni@yahoogrou ps.comDate: Friday, 3 October, 2008, 11:19 AM
Ahsante kwa kuuliza nitakujibu kwa ufupi lakini kwanza kuhusu suala hili la mbeya .

Mzozo kuhusu mbeya ulianzia wakati ule wa kumchagua mgombea wa uraisi toka chama cha mapinduzi kulikuwa na makundi kule mbeya walikuwa wanamtaka raisi wao mwandosya , wao walitegemea yeye ndio atapita lakini ndani kwa ndani akachomewa utambi akabwangwa na huo ndio ukawa mwanzo wa hizi choko choko za mpaka leo .

Kama unafuatilia mambo mtu wa kwanza aliyetakiwa kulipia alichofanyiwa Mwandosya wakati wa kampeni zile ni Lowassa wakati fulani alitakiwa awe kwenye safari ya mkoa ule kama waziri mkuu lakini akashindwa kwenda kwa sababu alikuwa amelewa sana alitoka kwenda sherehe ya mtoto wake ile iliyotumia zaidi ya mil 300 , akatumwa juma akukweti akamwakilishe na safari yenyewe ilicheleweshwa mpaka saa 8 ndio alitoka dar kwenda mbeya muda wote huo lowassa alikataa kwenda .

Wakamkosa Lowassa akapatikana akukweti na hata yeye alicheleweshwa kupelekwa hospitali kwa sababu zao tu wenyewe wanazozijua alikaa zaidi ya masaa kadhaa
"If you won't take the personal responsibility to help raise the level of debate on PwaniForums, you do not have much of a case for expecting anyone else to do so on your behalf." --- On Fri, 10/3/08, lingson adam wrote:
From: lingson adam Subject: Re: [wanazuoni] JK KUSAFIRI TENA (NINI TATIZO LA MNETE ???)To: wanazuoni@yahoogrou ps.comDate: Friday, October 3, 2008, 7:13 AM
AMANI IWE KWENU

SHUKRANI KWA KUTUHABARISHA NDUGU MARO.
KUHUSU MBEYA:
KUNANI MBEYA HATA RAIS WA NCHI AOGOPE KWENDA???? AU KUNANI MOYONI KWA JK HATA AJIKUTE NAFSI YAKE IKISUTWA???? ? AMA KUNANI AKILINI KWETU KINA SISI WACHAMBUZI TUNAOJARIBU KUENEZA UWEPO WA FITNA,HOFU, MASHAKA, TISHIO LA USALAMA HUKO MBEYA HATA KUJARIBU KUUFANYA MKOA WA MBEYA KUWA NA TASWIRA YA MKOA WA AJABU KIASI KWAMBA RAIS ALIYEPIGIWA KURA NA WANANCHI WA MKOA HUO HUO NA AKASHINDA KWA KISHINDO ANAOGOPE KUFANYA ZIARA???

ZAIDI YA YOTE TIJA YA ZIARA YA RAIS KWENYE MKOA WOWOTE NI IPI???WATANZANIA TUCHAPE KAZI. RAIS MAKINI NA MAHIRI ANAWEZA KUSIMAMIA MAENDELEO YA NCHI VIZURI KABISA KUTOKEA IKULU YAKE NA KUPITIA MIFUMO YA KIUONGOZI NA KIUTAWALA ILIYOPO. SI LAZIMA AENDE KILA MAHALI KUUZA SURA YAKE. IWAPO TUTAKAZANIA KUAMINI NA KUWAAMINISHA WANANCHI WENZETU KWAMBA MATATIZO YAO HAYATAWEZA KUONDOSHWA MPAKA TU-RUB SHOULDERS NA RAIS, BASI TUMO HATARINI.

Mwisho Kamaradi Maro, sidhani kama shambulizi ulilofanya kwa Mnete kuwa ni la haki. Je hatangazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma hiyo??Pengine mwenzetu utwambie UNAJUAJE KIWANGO CHA TAALUMA YA KILA MTANZANIA, wewe ni nani hasa kaka?? NA PIA TUTAABUDU MADIGRII YA KARATASI HATA LINI???KOSA LA MNETE LIKO WAPI KWA YEYE KWENDA KWENYE ZIARA YA RAIS?? NA UNATHIBITISHAJE IWAPO ANAYEMLIPIA NI JK AMA SERIKALI NA SI CHOMBO CHAKE (ITV)?? KUONGOZANA NA RAIS KUNA SHIDA GANI? JE WAWEZA KUTOA USHAHIDI UBAONI KUTHIBITISHA UTENDAJI ULIOCHINI YA KIWANGO WA SUDI MNETE NA KWAMBA UMETOKANA NA KIWANGO CHAKE USICHOKIELEWA CHA KITAALUMA NA KITAALAMU?JE HUDHANI KAMA UMETUMIA JUKWAA HILI KUMDHALILISHA MNETE?? pima mwenyewe!!!Chukua hatua.

NAWASILISHA.
ADAM, L
BOX 16335
ARUSHA, TANZANIA

http://uk.mc254.mail.yahoo.com/mc/compose?to=lingsadam@yahoo.co.uk
http://www.upolesana.blogspot.com/ --- On Fri, 3/10/08, Misha wrote:
From: Misha Subject: Re: [wanazuoni] JK KUSAFIRI TENATo: wanazuoni@yahoogrou ps.comDate: Friday, 3 October, 2008, 9:40 AM
Heeeeeeeeeeeeeeee, ushasahau kuwa, huko huwa anaenda kutafuta wadau wa maendeleo kwa taifa letu kama vile wawekezaji

Na je umeshasahau kuwa akirudi atakuwa ameahidiwa, kwamba Tanzania itapewa msaada wa kiasi fulani cha fedha.

Jamani hivi umesahau kuwa ombaomba si lazima kujipanga barabarani na kikopo cha bati, huku ukisema saidia baba saidia mamaaaaaaaaaaaaaaa.

Inawezekana kuna kuwa ombaomba ya kiutaalamu zaidiiiiiii! !!! jamani subiri atakuja kaahidiwa mabilioni ya pesa, na yeye amekubaliana na mambo fulani ya kibinafsishaji
Sasa sijui hiyo itakuwa ni WIN WIN situation ama WIN LOSE situation??? ?
MAZUNGUMZO YATAKUWA HIVI

Jei Kei: Saidia baba

Wadau wa maendeleo ya Tanzania nchi za nje: Nikusaidia nini mbona una rasilimali kibao

Jei kei: Kuzifaidi inahitaji kufikiri baba tena na investment ya hali ya juu nasi hatuna.

Wadau wa maendeleo ya Tanzania nchi za nje: http://uk.mc254.mail.yahoo.com/mc/compose?to=&?@@@$$$$*******&&&&&&!!!^^^????!! !!

Jei kei: Tafadhali njoo uwekeze nami nipatiemo kidogo, eeee baba tehe tehe. PLEASE

Wadau wa maendeleo ya Tanzania nchi za nje: Dont woree, i will help you, Dont distabu your mind. THINKING IS TOO HARD, I WILL THINK FOR YOU

Jei Kei: seikyu vere muchi
Alamsiki--- On Thu, 10/2/08, Yona Fares Maro wrote:
From: Yona Fares Maro Subject: [wanazuoni] JK KUSAFIRI TENATo: "techtz alphonse" Cc: wanazuoni@yahoogrou ps.comDate: Thursday, October 2, 2008, 6:40 AM
Raisi jakaya mrisho kikwete anatarajiwa kusafiri tena kuelekea nchi za amerika ya kusini kuanzia wiki mbili zijazo , anatarajiwa kwenda brazil , cuba pamoja na Venezuela , anazidi kutuka viunzi tena kuhusu safari yake ya mkoa wa mbeya ambayo inasemekana alitakiwa aifanye baada ya mwezi mtukufu .

Ziara nyingi za raisi zimekuwa zinasindikizwa na misafara mirefu ambayo haina umuhimu wowote katika safari hizo pamoja na waandishi wa habari ambao hawakidhi fani hiyo ya uandishi kama sudi mnete wa ITV ambaye elimu yake ya uandishi wa habari haieleweki vizuri nab ado anaongozana katika misafara hii ya raisi .

Sasa ni wakati kwa wananchi wa Tanzania haswa wadau wa habari kuanza kuhoji kuhusu safari hizi haswa gharama zake na faida zake kwa taifa , miaka michache iliyopita waziri mkuu mstaafu aliwahi kusafiri kwenda ulaya aliporudi watu walilalamika sana kuhusu safari hiyo na garama zake .

Basi jambo hili pia lifanywe kwa raisi wetu na wale wote anaoongozana nao katika misafara hii watanzania wajue kinachoendelea ni nini haswa

SOURCE: WANAZUONI YAHOOGROUP

0 comments:

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP