Pekua/search

Tuesday, October 7, 2008

WENYE MOYO WANAPOJENGA NCHI WASISAHAU KUWANG'OA MENO WALA NCHI

TAIFA HUJENGWA NA WENYE MOYO.
NA HULIWA NA WENYE MENO.
WENYE MOYO WAKIIJENGA NCHI HUKU
WENYE MENO WAKIACHWA KUTANUA MAJIANI
WAJENGAO NCHI WAFANYAKAZI BURE.
WANAKESHA BURE!!!
LAZIMA WENYE MENO WADHIBITIWE.

MOYO KABLA YA SILAHA,
LAKINI SI VITA AU MOYO BILA SILAHA.
"Octavius Kisinda" Add sender to Contacts
To:
wanazuoni@yahoogroups.com
Kamaradi Lingson,

Nimekupata na kukusikia vilivyo. Kinachofuata hapo ni kuchukua hatua mahsusi ili kufikia malengo.

Mchana mwema

The Millenium Court No. 20
8 Cottam Avenue
BRADFORD, Western Yorkshire
BD7 2BT
Mobile: +44 7501 871 805 , +255 754 470 321


'Quid Non Deo Juvante (With God Everything is Possible).'
----- Original Message ----From: lingson adam To: wanazuoni@yahoogrou ps.comSent: Tuesday, October 7, 2008 9:02:37 AMSubject: [wanazuoni] Tanzania itajengwa na wenye moyo SAWA; WENYE MENO JE???
AMANI KWENU WANAZUONI

Hongera pia nakupeni ninyi nyote ambao japo mko mjini mnajisikia kuguswa na kusukumwa kufanya kitu juu ya maisha ya huko kijijini.

Kamaradi Octavius, HAKIKA TANZANIA IMEKUWA IKIJENGWA NA WENYE MOYO. IMEFIKA HAPA (hata kama inachechemea, iko hoi, mahututi au taabani) KUTOKANA NA JASHO LA WENYE MOYO.

KIFUATACHO KWENYE HICHO NA AMBACHO NINADHANI NDIYO WAJIBU WETU MKUBWA KWA SASA NI KUHAKIKISHA TUNAKASIRIKA NA KUJAZIBIKA NA KUWAJAZIBISHA WENZETU ILI KWA PAMOJA TUWANG'OE MENO WALIOKUWA NAYO, AMBAYO KWAYO WANAKULA NCHINI INAYOJENGWA NA WENYE MOYO. AMBAYO KWAYO WANAKULA MATUNDA YOOOOTE YA UHURU BILA KUSAZA, HUKU KINA YAKHE WAKIACHWA KUAMBULIA MAJANI YA UHURU YALIYOPUKUTIKA HAPA NA PALE.

NAWASILISHA
ADAM, L
BOX 16335
ARUSHA, TANZANIA

lingsadam@yahoo. co.uk
www.upolesana. blogspot. com --- On Mon, 6/10/08, Octavius Kisinda wrote:
From: Octavius Kisinda Subject: [wanazuoni] Tanzania itajengwa na wenye moyoTo: wanazuoni@yahoogrou ps.comDate: Monday, 6 October, 2008, 10:08 PM
Mpendwa Anastazia,

Nimefurahi na kufarijika kwa jinsi ambavyo umekuwa mmoja kati ya wanazuoni wachane na Watanzania wachache walioweza kujitoa kwa hali na mali kuleta mabadiliko kwa makundi yaliyo pembezoni. Hakika unapaswa kupongezwa na kujifunza toka kwako.

Kwa kuwa mchango wako ni bayana hasa kwetu ambao tumewahi kushi vijini (Usandawe, Kondoa mkoani Dom kwa miaka 5), changamoto ninayoipata hapo ni jinsi ya kuwashauri na kuwashawishi vijana wanaomaliza elimu ya juu kujitolea kulifanya hilo walau kwa mwaka hata mmoja kabla ya kurudi mjini. Kinachonisikitisha ni jinsi ambavyo 'white colour jobs and material accumulation' vinavyoonekana kama ndo elimu kwa sasa. Nadhani tunahitaji kufanya mapinduzi katika eneo hilo na tuone kuwa utumishi uliotukuka wa kujitoa kwa moyo kwa maslahi ya wengi ndo kipaumbele.

Hakika ninayakumbuka kwa dhati maisha yangu ya kijijini kusikokuwa na umeme, barabara ya vumbi na kulala njiani wakati wa mvua ni kitu cha kawaida kabisa, kuendesha pikipiki na kuanguka ni sehemu ya maisha, mawasiliano ni radio simu ya upepo (radio koo) pekee na basi ni mara tatu tu kwa wiki siku nyingine kuifika Dom mjini inakubidi kupanda magari ya mizigo. Ukiwa ndo msomi pekee kwenye tarafa nzima mchango wako unaonekana kwa haraka kulikoni ukiwa Dar kwenye wasomi wengi na wengine wanaotafuta kazi.

Ninafikiria kurudi huko kwa ajili ya utafiti wangu lakini pia kuwatia moyo ndugu zangu kuwa inawezekana. Changamoto niliyonayo ni kuhakikisha kuwa ama ninarudi tena huko au ninahamashisha vijana wengie waende wakapate uzoefu wa Watanzania. Hakika maisha ya elimu, ujuzi na uzoefu usiogusa maisha ya watu hauwezi kuwa ni chachu sahihi ya kuleta mabadiliko endelevu yanayogusa maisha ya wengi.

Kinachonifurahisha ni kuona kuwa kuna Wanazuoni wengi wanaogusa maisha ya watu kwa namna moja au nyingine na hasa walio vijijini. Nikianza kuwataja hapa sitamaliza, bali ninawapongeza kwa utumishi wao ulotumika. Nawatakia mafanikio katika yote yaliyo mbele yenu.

Mungu ibariki Tanzania,
Mungu wabariki wale wote wanaojitoa kwa dhati kwa ajili ya wengi.

Wenu,

KISINDA, Octavius A.
The Millenium Court No. 20
8 Cottam Avenue
BRADFORD, Western Yorkshire
BD7 2BT
Mobile: +44 7501 871 805 , +255 754 470 321


'Quid Non Deo Juvante (With God Everything is Possible).'
----- Original Message ----From: Mbogela Jackson To: wanazuoni@yahoogrou ps.comSent: Monday, October 6, 2008 2:49:07 PMSubject: [wanazuoni] Hongera Annastazia
Hongera Anastazia kwa kazi nzuri Mufindi, Umetoa mchngo wako katika Jamii ya watanzania, tunatahitaji kuwekeza nguvu kidogo sana hapo baadaye kama sasa hivi tutajitolea kluokoa Rasilimali za Taifa zitumike kwa jaili ya walio wengi. Nimeipenda kazi yako Mufindi, Hongera sana. Jackson Mbogela Haarweg 95 – 3166709 PT WageningenThe Netherlands
Cell: +316 43 63 73 73
Tz: +255 787 410 315
Sauti ya Nyika PIUMA WEBSITE PIUMA, IKONDA & TANWAT
Change does not roll in on the wheels of inevitability, but comes through continuous struggle.
Martin Luther King, Jr.
To: wanazuoni@yahoogrou ps.comFrom: neemarug@yahoo. comDate: Mon, 6 Oct 2008 02:16:44 -0700Subject: Re: [wanazuoni] HAPPY BIRTHDAY !
Hongera sana Chambi, u mean a lot to us thatʼs why tunakuombea uongezeke si miaka tu bali ujuzi na maarifa. Keep in mind that the ladder of success is not crowded at the top so keep it up!
HAPPY BIRTHDAY CHAMBI, Bravo

Annastazia Rugaba
Interim Manager-Media Unit
Haki Elimu

NB: Pia nitumie fursa hii kuwasalimia wanazuoni na kuwajulisha kuwa mimi ambaye ndiye katibu wa mtandao huu nimerejea Dar es Salaam toka Mafinga-Mufindi- Iringa-Tanzania nilikokuwa tangu December mwaka jana! nimekuwa na miezi kumi ya maisha magumu kiasi ila yenye vionjo vilivyopevuka. nilikuwa huko nikisimamia Project ya Ku support 200 Orphans & vulnerable children kwa kuwapatia misaada mbalimbali pamoja na vocational training in Electrical Installation, welding and fabrication, masonry and brick laying, Tailoring, Carpentry, food processing and Preservation, chalk making, batik tie & dye, and soap making. Haikuwa kazi rahisi kukaa na vijana 200 wenye matatizo kibao: waathirika wa ukimwi, waliobobea katika biashara hatarishi, wenye matatizo ya akili, wenye msongo na tabia tata kutokana na kupotelewa wazazi, kunyanyaswa na ugumu wa maisha, wahanga wa ubakwaji, wasiojua kusoma wala kuandika, nk. Kuwasimamia na pia kufanya tasks za Manager, Muhasibu, karani, matron, mshauri, mwalimu, afisa na mratibu wa mradi, n.k yote hayo yamewezekana. Kazi imekwenda vizuri na imesababisha kuongezewa fungu la kutosha kurecruit vijana 100 tena kabla project haijaisha.

Atakaependa taarifa zaidi juu ya
· Namna ya kuishi vijijini kikazi na kumudu maisha(kwa vijana wanaotoka vyuoni na hawana uzoefu wa field)
· Namna ya kuleta changamoto kwa jamii masikini ziweze kuhamasika kimaendeleo
· Kuifanya miradi ya wafadhili iwe shirikishi kwa jamii yaani jamii ijisikie kuimiliki miradi na kuleta uadilifu na uwajibikaji
· Kuwamudu vijana yatima na wanaotoka katika mazingira magumu
· Namna ya kupata products zinazotengenezwa na hawa wajasiriamali wachanga kutokana na kozi tajwa hapo juu(kwani licha ya kuwafundisha pia tumewapa mashine, mitaji, elimu ya ujasiriamali na tumewaweka katika makundi na kuakodia business canters)
· Na mengineyo kuhusiana na project hii anaweza wasiliana name sasa niko Haki Elimu nikikaimu nafasi ya Mwanazuoni mwenzetu ambae kwa moyo mmoja ninampongeza sana kwa kupata nafasi ya masomo nje ya nchi. Ninaiahidi tena jamii, wanazuoni na mwanazuoni Nyanda Shuli kuwa nitafanya kazi kwa bidii na kamwe sito waangusha.

Nawashauri wanazuoni wenye uoga na kukimbia assignments za field hata wanapopata fursa hizo, wanakosea sana. Mimi mwenzao nimekombolewa katika hilo, najivunia uzoefu nilioupata katika kazi hiyo na nina uhakika nimewapiga gap kubwa sana graduates wenzangu wengi ambao walipata fursa hizo na kuzipuuza ati kwa kutaka kubaki mjini.
Ahsanteni jamani

CHANZO:wanazuoni yahoogroups

0 comments:

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP