MAMBO YA THELUJI YA LONDON/ SNOWY LONDON
DEVELOPED OR NOT, WE ARENT RIPE ENOUGH: theluji ya Uingereza
Kama inavyojulika kote duniani Jiji la London (na sehemu kubwa ya Uingreza) leo (Jumatatu) limepigwa na bumbuwazi kutoka na janga la kuanguka kwa theluji/barafu? Inaelezwa barafu nzito namna hii ni ya kwanza kutokea katika miaka 18 iliopita, kwa hiyo kwa hapa imekuwa afadhali, maana wenyeji na wageni sote tunashangaa shangaa.
Matokeo ya hali hii wakazi wa jiji hili wamejikuta wakihangaika kwa mambo mengi, hususan usafiri kugota. Barabara zimejaa ‘tope’ la theluji.
Wengine sisi wa kuja tumefurahi kuona hali hii maana kwetu kijijini nasikia hadithi tu, kwa hiyo pamoja na baridi kuwa kali, wadaku kama mimi vyumba havikukalika. Kubwa lililonipa kisebusebu ni kwenda kuangalia wenzetu wanakabili vipi hili janga (wameendelea watu hawa). Kikubwa ni kwamba taarifa za hali hii mbaya zilishatolewa mapema, nadhani siku tatu au tano nyuma.
Bwana weee, hakuna cha kuendelea wala nini, lijikiwanja lao la Heathrow tumeambiwa hapakurukika mijidege wala kutua, matreni yao ya mapangoni almaarufu kama ma’tube’ kwa njia za kuingia katikakati ya London nadhani ni Picadilly line tu. Mabasi ndiyo usiseme, halikuwepo hata moja barabarani (kwa maeneo niliyozurura na kwa mujibu wa taarifa za habari) ungeambiwa utafute moja la dawa, we anza kufa mapema, hulikuti. Inaelezwa kuwa ndiyo mara ya kwanza mabasi yao kuwahi kusitisha safari.
Kutokana na hali hiyo ya usafiri kupooza, shughuli nyingi hapa central London zilizimia. Mabenki yalifungwa, maduka muhimu vivyo, usiseme kuhusu shule na vyuo, walimu (wanafunzi pia) hawakufika, shule itakwenda vipi, hapa na hata vyuo vingine maktaba hazikufunguliwa, wahudumu hawapo!!!!
Ingekuwa kwa Alhaj Kimbisa Dar au Kapunga kule mbeya, tungesema aah bwana umaskini, oo dunia ya tatu sijui mara nini. Sijifariji, wala sifurahii tunavyoshindwa kukabili majanga yanayoepukika, lakini ninachojifunza ni kwamba matatizo ya nchi zinazoendelea yanasababishwa na sababu zaidi na labda tofauti na zile zinazotajwa kila siku ‘conventional’, ama sivyo hawa jamaa wasinge ‘bakwa’ na hali hii, maana walau walijua na wameendelea hawa!!! BINADAMU NI WALE WALE. MENGINE MBWEMBWE TU!! HAKUNA LOLOTE! UZUSHI MTUPU. WIZI MTUPU!!
Ahsante
Tazama picha zaidi kwenye PHOTO GALLERY kulia kwako
0 comments:
Post a Comment