Pekua/search

Thursday, March 12, 2009

KUPIGWA KWA MZEE MWINYI - 'SECURITY IS LIKE A MYTH IT DOESNT EXIST'

(for the english version of the saga read here)

Niungane na watanzania wengi waliofadhaishwa sana. waliosikitishwa na kuumizwa sana kwa kitendo cha kupigwa kwa mzee Ruksa (kutazama kipande cha video kuhusu tukio hilo bofya hapa - chanzo:jamii googlegroups). nimeumizwa nafsi nilipoangalia na kutazama kipande hicho na kwa kweli ninashawishika kuamini kwamba hakiwezi kuhalalishwa au kuhalalishika kwa namna yoyote iwayo. Lakini tuna mengi ya kujifunza kwa tukio hilo. hivi usalama uko wapi?

Jamaa, Ibrahim Said (ambaye Suleiman Kova, kamanda wa kanda maalum ya dar es salaam ya kipolisi anajaribu kuanza kuziandaa akili zetu ziamini hayuko timamu) alitoka alipoketi, kajongeambele, akapanda jukwaani, akasogea kwa mzee ruksa, akajipinda (kama anapiga penalti, akamnasa kibao mzee wa watu!!!!).

Inashangaza na kustaajabisha kwa jamii ya kitanzania iliyoshibishwa imani ya kutisha kuhusu ufanisi wa 'vijana wa kazi' wa usalama wa taifa na majeshi yetu ya ulinzi na usalama (au ndiyo habari zile zile kama za 'tusiponunua mitambo ya Dowans eeeeh balaa linakuja!!!!). Katika jamii ya kitanzania ambamo mahela na mijifedha isiyokaguliwa inatumika kwenye kuwaandaa na kuwafunza na kuwastawisha vijana wa kazi, inakuwaje habari ya lijitu flani hivi kuinuka na kumnanga kibao si tu cha aibu bali cha haja pia, mzee wetu hadharani?

Ama kweli vijana wa kazi wapo tu kwa ajili ya kushughulika na matukio, si kuzuia matukio (reactive na siyo proactive), maana tumewaona walivyofanya mbwembwe za mitama na kumbeba mzobemzobe yule jamaa, lakini angekuwa na kisu ishakuwa tayari mzee ruksa keshadhulika, usiseme kuhusu bunduki na mabomu!!!

kwa tukio hili nashawishika kuamini kwamba, USALAMA NI KAMA IMANI TU, HAUPO POPOTE!!! Kwa waumini wa dini, UPO MIKONONI MWA MUNGU, kama msemaji mmoja alivyoliweka vema, SECURITY IS LIKE A MYTH, IT DOESNT EXIST!!!

Pole mzee mwinyi kwa mshtuko na maumivu,
Pole watanzania kwa kufadhaishwa na kufikirishwa,
Lakini zaidi pole wanausalama na wazandiki wote maana mnakazi ya kusafisha picha ya utendaji wenu legevu!!!

1 comments:

Anonymous March 16, 2009 at 2:13 PM  

I am less concerned with securities. I am troubled with the abrupt vanishing of ethical-life in Tanzania.

It is a pity that some folks are backing up the assailant. Somewhere something is wrong.

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP