AHADI KUMI ZA RAIS KIKWETE KWA WATANZANIA: JE BADO LIPO TUMAINI???
Mojawapo ya Hotuba muhimu alizowahi kutoa mhe. Rais jakaya Mrisho Kikwete ni ile aliyoitoa akifungua rasmi bunge 'jipya' la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Desemba 30, 2005. Tujikumbushe ahadi alizotoa (mambo kumi) tujihoji na kuhoji TUMEFANIKIWA KWA KIWANGO GANI hadi sasa tunapoelekea kumaliza ngwe hiyo ya miaka mitano!!! HAYA TWENDE:
"...Kwa kuzingatia majukumu haya ya msingi, na mbinu na mikakati mbalimbali ya kuyatekeleza, Watanzania watarajie mambo kumi yafuatayo katika miaka mitano ijayo:
1. Serikali ya Awamu ya Nne itahakikisha kuwa Amani, Utulivu na Umoja wa nchi yetu na
watu wake vinadumishwa;
2. Serikali ya Awamu ya Nne itadumisha na kuendeleza mafanikio yaliyopatikana tangu
Serikali ya Awamu ya Kwanza hadi leo;
3. Serikali ya Awamu ya Nne itaendeleza vita dhidi ya umaskini, ujinga na maradhi, tena kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya;
4. Serikali ya Awamu ya Nne itatimiza ipasavyo wajibu wake wa utawala na maendeleo, na
itaendesha dola kwa misingi ya utawala bora na uwajibikaji; utawala wa sheria unaoheshimu na kulinda haki za binadamu;
5. Serikali ya Awamu ya Nne itaimarisha uwezo wake wa kulinda maisha na mali za raia wake. Tutapambana na uhalifu wa kila aina, na majambazi hayataachwa yatambe yatakavyo;
6. Serikali ya Awamu ya Nne itahakikisha mipaka ya nchi yetu ipo salama. Hatutamruhusu mtu au nchi yeyote kuchezea mipaka ya nchi yetu na uhuru wetu;
7. Serikali ya Awamu ya Nne itafanya kila iwezalo kuhakikisha Tanzania ina mahusiano
mazuri na mataifa yote duniani, pamoja na mashirika ya kimataifa na kikanda;
8. Serikali ya Awamu ya Nne itajali sana maslahi na mahitaji ya makundi maalum katika jamii kama vile wanawake, vijana, watoto, wazee, walemavu na yatima;
9. Serikali ya Awamu ya Nne itaongoza mapambano mapya ya kuhifadhi mazingira ili
vizazi vijavyo virithi nchi nzuri, na msingi imara wa maendeleo endelevu; na
10. Serikali ya Awamu ya Nne itaendeleza michezo, na shughuli za utamaduni na
burudani."
Maneno mazuri sana haya. Je tumeyafikia? Tafakuri ya utekelezaji wa haya yaweza kuwa mwanzo mzuri wa kuamua mustakabali wa upigaji kura wetu tunapochagua viongozi wa serikali za mitaa na mwakani madiwani na wabunge na rais wao!!!
1 comments:
Predilection casinos? bear out this unformed [url=http://www.realcazinoz.com]casino[/url] advisor and tergiversate online casino games like slots, blackjack, roulette, baccarat and more at www.realcazinoz.com .
you can also into our redesigned [url=http://freecasinogames2010.webs.com]casino[/url] orientate at http://freecasinogames2010.webs.com and augment the guide legitimate folding spondulix !
another voguish [url=http://www.ttittancasino.com]casino spiele[/url] splash is www.ttittancasino.com , impartially than of german gamblers, submit c be communicated during humanitarian [url=http://www.realcazinoz.com]online casino[/url] bonus. so check this leading [url=http://www.omniget.co.il]online casino[/url] for free [url=http://www.casinosaction.com]casino bonus[/url] and 100's of online [url=http://www.thecasino.co.il]casino[/url] games.
Post a Comment