Pekua/search

Monday, September 7, 2009

RUNGWE YAPIGA HATUA KUIMARISHA UTAWALA BORA





















































Kuimarisha utawala bora ni mchakato endelevu. Katika kutimiza hilo, Halmashauri ya wilaya ya Rungwe imepiga hatua kwa kuweka 'ubao' wa matangazo uliorafiki kwa watumiaji. Sifa bainifu za ubao rafiki ni pamoja na kuwa na sehemu z aidi ya moja na kutumiwa kuweka matangazo si tu na utawala bali watumia huduma pia (interactive); na kuwekwa mahali panapofikika kirahisi bila hofu na wakati wowote. Halmashauri ya wilaya ya Rungwe imeondosha ubao wa matangazo kwenye ukuta wa ofisi za halmashauri hiyo na kujenga katika eneo la wazi zaidi na linalofikika karibu wakati wote. Hatua hiyo haina budi KUPONGEZWA. Hata hivyo wadau hawanabudi kuzingatia kwamba KUWEKA miundo mbinu ni hatua moja na KUITUMIA yaweza kuwa jukumu tofauti kabisa.


4 comments:

Anonymous September 14, 2009 at 11:50 PM  

samahani naomba kufahamu wilaya ya rungwe ipo mkoa gani?.

Adam September 15, 2009 at 2:40 AM  

Du!
shukrani kwa kuuliza, aulizaye ataka kujua. Rungwe ni moja ya wilaya saba za mkoa wa mbeya. Mara nyingi inatajwa kimakosa (common mistake kama kwa 'mkoa wa Bukoba badala ya Kagera, mkoa wa songea badala ya Ruvuma, mkoa wa musoma badala ya Mara, na mkoa wa sumbawanga badala ya Rukwa)) kama Tukuyu. Tukuyu ni makao makuu ya wilaya hiyo. Mkoa wa Mbeya upo kusini magharibi ya Tanzania.

Anonymous September 15, 2009 at 11:36 PM  

asante kwa kunijibu ingawa ulianza kushangaa sio kama siju nafahamu Adam.Niliuliza hivyo ili ufahamu kuwa una wasomaji wa aina mbalimbali na wenye uelewa tofauti.Hivyo basi ni vema ukawa unaweka vitu wazi.Ni rahisi mtu kujua mkoa kuliko wilaya.Samahani kwa usumbufu

Adam September 16, 2009 at 12:24 AM  

Sawa sawa kabisa. Haya ni makosa ya kidhahanifu katika uandishi ambapo 'assumptions' na nia ya kuandika vitu vichache hutawala zaidi.

Kweli ndugu yangu kuna siku tulikuwa kibondo (na wanaharakati wawili) likatujia wazo kuwauliza wenzetu kadhaa. Kati ya kumi tuliowauliza, saba hawakujua kibondo iko wapi. Wengine kati yao hawakuweza hata kueleza hata kama ni mashariki, kusini n.k mwa Tanzania. Wote hawa walikuwa wahitimu wa shahada kwa kiwango cha chini.hili linaipa uzito hata zaidi hoja yako.

Japo kwa upande wa pili, kwa vile nia moja wapo ya gazeti tando hili ni kuchochea na kuamsha fikra na mijadala, sio mbaya sana maana yeyote aliyeshindwa kujua Rungwe iko wapi atakuwa amechagizwa kufuatilia na hivyo kwenda hatua moja zaidi katika kutafuta maarifa kuliko kuishia kuangalia katuni hapa!!! (SIASA)

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP