Pekua/search

Sunday, December 27, 2009

KILIMO KWANZA NA UJANJA UJANJA KTK UTOAJI MBOLEA YA RUZUKU:TUTAFIKA TANZANIA?


Mbali ya kuendelea kujihoji iwapo KILIMO KWANZA ni SERA, MKAKATI, MPANGO, PROGRAMU AU KAULI MBIU, taarifa za ujanja ujanja katika mwelekeo wa kutekeleza hilo (nisilojua ni nini - nimesoma majuzi katabu ka kilimo kwanza nimekuta kakitaja kuwa ni dhana, sera, mpango, kauli mbiu nk) zinaonyesha kuwa ugawaji wa mbolea ya ruzuku kwa wakulima umekuwa na mushkeli. usinichoshe, nisikuchoshe, SOMA taarifa ifuatayo kutoka kwa msomaji wa blog hii ndugu Mwamakula aliyeko Lwangwa wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya.


“Jamani ninyi mlio huko kweupe tunaomba mtusaidie! Huku kwetu kijijini (LWANGWA TUKUYU MBEYA) tumeletewa mbolea inayoitwa ya ruzuku! Lkn tulitakiwa kulipa sh. 113,000 ndipo unapatiwa mifuko 4 ya mbolea! Tulipowaambia hiyo pesa hatuna,wameamua Kutusaidia! Tunapewa mfuko mmoja tu ila bure kabisa,pengine sh.3000 tu ya nauli. Ila tunasaini tumepewa mifuko minne ya mbolea! Je ni halali au tunaibiwa?”

Akaongeza taarifazaidi

“Wajameni bado tunaomba msaada wenu!Hii mbolea ya ruzuku ya kutumia vocha utaratibu wa kuipata kwa sasa uko hivi:

Mkulima analipa sh. 95,000 hivi,anatakiwa apatiwe mifuko 3 ya mbolea na kilo 10 za mahindi!Hapa lwangwa wananchi waligoma sababu mbolea hiyo hiyo inauzwa madukani sh. 25,000 kwa mfuko lkn wakala anasema hii ya ruzuku ni sh. 27,500 kwa mfuko!Kwa mifuko 3 ukinunua dukani itakuwa sh. 75,000 tu!

Sasa wanahoji hiyo ruzuku iko wapi? Wakala anasema ya ruzuku bei iko juu sababu ni mbolea original na hii ya madukani ni feki! Baada ya kuona watu wamegoma na hawana hiyo fedha,kinachofanyik a sasa mkulima analipa sh 3000 tu ya nauli,anapewa mfuko mmoja tu wa mbolea. Ila anatakiwa asaini amechukua mifuko 3 ya mbolea na kilo 10 za mahindi! Kwa kuwa hii inaonekana rahisi,wakulima wengi wamekubali kuchukua mfuko mmoja bure ingawa wanasaini mifuko 3! Pia hakuna mwenye taarifa sahihi juu ya utaratibu huu!Tafadhali tupeni elimu,ruzuku hii ikoje?”

HAPO VIPI NDUGU MSOMAJI? FANYA JAMBO, WALAU SEMA NENO HAPA UBAONI

0 comments:

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP