old ways of celebrating christmas on extinction - are new ones any better?
Mambo ya kusangula - a way to celebrate Christmas that is now on the edges of its extinction in Rungwe Tanzania marking the end of 'those golden old days!'
By Baraka Herbart - recently in Lwangwa Tukuyu - Tanzania
'Kusangula' ni moja kati ya matukio yenye mvuto wa aina yake ambayo mara nyingi hufanywa na vijana na watoto wa kwetu hasa nyakati za sikukuu za krismas na mwaka mpya!
Kundi la vijana na watoto wake kwa waume hupita nyumba kwa nyumba wakiimba na kuserebuka 'nyasima kapapike napile imbange...eeh hodi hodi..'! Wakifika kwako,unatakiwa kuwapa japo zawadi ndogo ndogo tu kama hindi,ndizi au hata vijisenti kidogo!Lakini si lazima sana kama huna!Wao huenda kugawana!Hawa hunogesha kijiji kizima kwa mirindimo ya shangwe,vifijo, nderemo n.k!Acha tu!
Leo hii hawapo tena!Utandawazi! Vijana wapo 'mageto' na 'vimwana' wao na watoto nao wamekaa masebuleni 'wakikodolea' Tv!Kijiji kimya,utadhani hapana sikukuu!Ukibahatika kuwaona ni kama hawa wachache wamekuja nyumbani kwangu,nawapa vijisenti kidogo!Mara nao wametokomea, hawapo!Kumbe ni wale wale 'wajasiriamali' ,ambao wanatafuta namna baada ya kuganga na kiu ya 'kalita'!!Hatimaye nawakuta wamejipumzisha 'Kipangamansi' ,moja ya vilabu vya pombe maarufu sana hapa Lwangwa!Nadhani ni baada ya mifuko kunona!Tamaduni hizi zaelekea kwisha!!!
0 comments:
Post a Comment