Pekua/search

Sunday, January 17, 2010

he is an american - he must be loving tanzania; more than you?


MGENI ANAPOTUZIDI UZALENDO
Na Mch. Emmanuel Bwatta - University of the South, Tennessee, USA.

Mwenye hii gari ni Mmarekani na mwanafunzi wa uchungaji hapa ninaposoma. Alikuja Tanzania (Arusha) June mwaka jana. Nilivutiwa jinsi anavyoonyesha kuipenda Tanzania labda kuliko sisi wenyewe. Nadhani hiiyo picha ni kielelezo tosha.

1 comments:

Mbele February 24, 2010 at 8:17 AM  

Ukizunguka sehemu mbali mbali za Tanzania, utawakuta waMarekani wakiwa katika shughuli za kujitolea, wakiwa wameletwa na mashirika kama Peace Corps, Global Service Corps, Cross-Cultural Solutions, Global Volunteers na kadhalika. Wanaishi maisha ya kawaida na kazi wanafanya kwa moyo moja hadi ndani kabisa vijijini.

Papo hapo, utawakuta waTanzania wengi wako vijiweni au wako baa wanakula ulabu, wakati kuna dhiki tele hapo hapo walipo, kama vile jengo la shule kuwa bovu, na kutokuwa na madawati au nyumba ya mwalimu. Wakati hao waMarekani wanaojitolea wanatembelea basi au baiskeli au hata mguu, utawakuta vigogo wetu wanakatiza mitaa hiyo hiyo na magari ya fahari, wakati wananchi wanaishi kwa dhiki.

Moyo wa kujitolea umefifia Tanzania. Halafu, hata ile akili au dhamiri ya kuona umuhimu wa kuwaangalia na kuwaiga hao wageni hatuna. Wageni wanaendelea kujitolea, wakati sisi tunatumia muda wetu kwenye vikao vya sherehe na matanuzi.

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP