Pekua/search

Monday, March 8, 2010

KILIMO KWANZA WAKULIMA WA MPUNGA WASHURTISHWA KUCHUKUA MBEGU ZA MAHINDI

Hivi sasa KILIMO KWANZA wimbo 'mtamu' uimbwao na wanasiasa wa Tanzania.
Utoaji wa pembejeo za kilimo (sema mbolea na mbegu 'bora') ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Kilimo kwanza ambao ni mpango/kauli mbiu/tamko/programu/dhana/sera/ chochote tu; nk ulioasisiwa kwa pamoja kati ya serikali na jumuiya ya wafanya biashara nchini(sijui ni kwanini hawakuasisi - BIASHARA KWANZA);umezusha mushkeli wilayani monduli mkoani Arusha. Hapa nakupa mifano michache tu:

Kijiji cha Olarash
Kijiji kilipewa vocha 100 kwa ajili ya mbolea na mbegu za mahindi kama ruzuku kwa wananchi ‘wanaoweza kuzalisha mali’. Wakazi wa kijiji hiki ni wafugaji/wakulima. Wanayo mbolea (samadi) kibao kwenye maboma yao. HAWAHITAJI MBOLEA ya chumvichumvi hawa. Ngoma ni pale wanapotakiwa kulipa shilingi 38,000/= ili kupatiwa kilo kumi za mbegu za mahindi na mfuko mmoja wa mbolea.

Wachache waliochangamkia vocha hizo, walitarajia kupata mbegu za mahindi, ndiyo MAHITAJI YAO. Lakini wanawekewa ngumu wakishinikizwa kuchukua na mbolea pia (ambayo hawahitaji, kwani wanayo ya kutosha na iliyo bora na rafiki zaidi kwa mazingira, SAMADI).Taarifa zilizopo ni kwamba ni kufuatia shinikizo hilo, wananchi wamegoma kuchukua vocha za ruzuku, na wachache waliochukua wamazikalia majumbani mwao pasipo kwenda kununua pembejeo.

Mto wa mbu
Wakulima wa mpunga wamepelekewa mbolea ya kupandia mahindi pamoja na mbegu za mahindi wakati wao wanahitaji mbolea ya kukuzia mpunga wao.Mfano wa wendawazimu wa top down planning, mh Hapana huu ni corrupt planning. Ufisadi tu. Punda hata akifa lakini mzigo ufike. Wakulima walazimishwe kununua pembejeo wasizohitaji, uzalishaji ubaki vile vile, lakini BIASHARA SI ITAKUWA IMEFANYIKA? Naam, hayo ni matunda ya mpango wa kilimo uliobuniwa na wafanyabiashara matajiri.

Minjingu:
Inaelezwa kwamba huko ndiko kunakochimbwa malighafi ya mbolea ya minjingu, udongo wake una fosfeti, lakini mbado nao wamepelekewa phosphate hiyo hiyo ya minjingu. JAMANI WATOA RUZUKU, SI KILA MTU ANATAKA MBOLEA, ACHILIA MBALI YA AINA MOJA!!!

0 comments:

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP