TRIBUTE TO PROF. JWANI MWAIKUSA
Hilo sitajisifu,
Zaidi ya mshairi mahiri,
Kwamba ndio wake wasifu.
Nilisoma kwa makini,
Nilipojua tu kusoma,
Nikajiuliza samoni (summons)!!
Ni ile ya mahakama?
Huyu fighter, alowaza,
Mimi sikulibaini
Alikuwa na maana gani, nikajiuliza mimi
Ulazwe pema msomi
Pumzika kwa amani peponi,
Twalia, twaomboleza.
Nuru yako ya wema
Mwangaza wako wa upendo
Kamwe hautazimika!!
Kwa walokujua na wa mbali
Watakuenzi daima
Nenda ‘Fighter,
Nenda,
Ee mola wetu mwema,
Ulosheheni rehema,
Waloinyang’anya haki,
Ya profesa kuishi,
Wale maharamia,
MUNGU UWASAMEHE,
Prof. Mwaikusa was murdered by unidentified people (armed robbers??????) Tuesday 13th July, at his place in Dar es Salaam.
NA UTUSAMEHE!
3 comments:
shairi lake moja linaitwa 'an awful dentist'. halichoshi kusoma na usomapo utabaki kucheka tu na utakapomaliza kucheka utahudhunika baada ya kulitafakari na kupata nini alimaanisha.
Ahsante John.
Tanzania imepoteza shujaa wa aina yake. Tafadhali kama una nakala pepe ya shairi hilo nishirikishe tafadhali. Waweza kulibandika hapa ama nitumie kwa lingsadam@yahoo.co.uk.
Kazi njema.
Asante kaka
Post a Comment