USHINDI WA SHEIN NA UTEUZI WA BILALI - NANI KASHINDA?
Nadhani ni bila bila. Nadhani mnyukano wa makundi bado unaendelea.
Nafariji hata hivyo kuona kwamba bado ni bila bila. hakuna kundi ndani ya CCM linaweza kujitapa na kutamba kuwa juu ya jingine. balance of terror imeonekana kabisa. siamini kama ni hiari ya JK kumteua Bilali, lakini nguvu yake, na tishio la kusambaratika kwa chama, ndicho kilichowezesha kutotoshwa jumla kwa Bilali.
Natamani mnyukano huo ungekuwepo kati ya CCM chama tawala kwa upande mmoja na upinzani kwa upande wa pili. Huu ushindi wa kishindo wa CCM kwa kweli hauna faida sana kwa mustakabali wa nchi yetu. Wabunge wa uoinzani, madiwni kutoka kambi ya upinzani ikiongezeka, itasaidia maslahi ya taifa yanayotokana na matakwa ya wananchi walio wengi yataweza kuwekwa mbele.
Kwa hili, Nampongeza rais Kikwete, kwa kumteua Bilali, maana hiyo inathibitisha ukweli kwamba Chama chochote hakipaswi kuwa mali ya mtu mmoja au kikundi kidogo cha wababe wachache.
0 comments:
Post a Comment