Pekua/search

Friday, August 20, 2010

MAMBO YAMEIVA UCHAGUZI MKUU- SALA YA WAZALENDO?


Imeitwa - 'sala ya wazalendo'.

"Asante Mungu kwa kuipenda Tanzania hata ukamtuma mwanamapinduzi wa pekee Dr. W. Slaa ili kila Mtanzania atakayempigia kura apate kuleta ukombozi wa kweli.


Tazama umemtuma kwa wapenda haki ili patakatifu (ikulu) pawe na Amani,


Sasa basi Mungu wasaidie watanzania wenzetu wasio na ujuzi wa Kutambua nani kiongozi Bora wamtambue kuwa amekuwa akidai haki zao yapata miaka 15,

Mungu tuepushe na rushwa za vitenge, pombe, simu, na Ahadi za uongo maana wewe hupendi uongo.


NI katika jina la Mungu Baba tunaomba na kushukuru"

Mtunga sala hii: Hajulikani

3 comments:

Anonymous August 22, 2010 at 2:44 AM  

kutoka kwa emelda osea

Mungu ibariki tanzania wabariki watu wote walioko tanzania Pia mtanzame kwa jicho lako na kumpa ujuzi zaidi wa kutunga sala huyu aliye tunga sara hii hapa chini
EEE Mungu tanzama watanzania wanavyo jifikilia mpaka wanatunga sala kama hii hebu uwatanzame kwa jicho la huruma uwapatie kiongozi bora
sifa za kiongozi huyo ziwe hizi:-
ASIWE MWONGO
ASIWE FISADI
NA MAMBO YANAYO FANANA NA HAYO,

RUSHA NDO SUMU

Anonymous August 22, 2010 at 2:46 AM  

kutoka kwa Godfrey Mushema

Huyu kweli ni mzalendo wa kweli kwa mawazo japo hatujajua matendo.

Adam August 22, 2010 at 2:48 AM  

Shukrani Emelda na Godfrey.
Tanzania ni yetu sote, na kila mmoja analofungu lake kumwombea anayeamini kuwa atasaidia kuongoza harakati za ukombozi wa taifa hili kutoka lindi la umaskini.

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP