HELKOPTA, MIJIGARI, MBWEMBWE NA TAMBO ZA KAMPENI MSIBANI
Ukishuhudia mbwembwe na tambo wakati huu wa kampeni,
Ukiona mijigari mikubwa ilosheheni,
Na helkopta zikipasua mawimbi angani,
Picha za helkopta kutoka blogu ya mzee wa matukio |
Ukiona tunavyoshangilia,
kwa mayowe na nderemo tukishabikia,
makofi ya uzito tukiwa pigia,
Utaamini sio sisi kila uchao tunaolia.
Kama kawa kura tutawapigia,
Kisha tutaendelea kuwatumikia,
maana sisi zumbukuku tulopindukia,
Kutenda si yetu ada bali kulia.