Pekua/search

Thursday, February 24, 2011

MMILIKI WA DOWANS, WAHARIRI NA KUZUIWA KUPIGA PICHA

Katuni kutoka gazeti la Majira
Ingekuwa vipi waandishi wa habari wa Bongo wangegoma kukubali masharti na dharau ya 'mmiliki' wa DOWANS kutotaka kupigwa picha?: hutaki upigwe picha au kuwa recorded? Fine, kwa heri! they walk out! Hili nadhani hata magazeti ya New Habari House yasingebaki ukumbuni; ingekuwa vipi?
Uhariri mdogo umefanyika ambapo ni picha tu zilizoondolewa, mawazo ya wachangiaji yamebaki kama yalivyo. Soma, shiriki mjidala hii ya kitaifa.
Top of Form
Barrack Mwamakula Brother ni dharau kubwa,nadhani ilitakiwa tufanye hivyo,cjui kwann hatukufanya!
Lusajho Mwambipile Kwanini usitake kupigwa picha na kurekodiwa? sababu aliyoitoa mie sioni kama inaridhisha, kweli wangeondoka ingeweza kujenga heshima. Hiyo ni dharau na fedheha kubwa mno kwa waandishi wetu wa habari
Bernard Elias Dharau tosha, tulishaambiwa mmiliki hajulikani, kajileta na kasema Rost tamu ndo alimsukia dili, akagoma asionwe na wabongo. Huyu jamaa ni wa hapa hapa, tukimwona tutamfahamu tu.
Japhet Mwaipopo I hope ingekuwa poa. Sasa kama hataki kupigwa picha kwnn aliwaita waandish? Hata waandish wa bongo hawana msimamo mi nadhan kulikuwa hakuna hata haja ya kuandika habari yake wangeitia kapuni. Sema ttzo lipo pale ambapo magazeti kadhaa yangegoma basi magazeti ya wale ambao wanamiliki hiyo dowans bila shaka wangeandika kwa uzuri sana. Any way acha hivyo hivyo tutafika tu kama libya kimenuka basi yawezekana kuni ya akiba inakaribia kuwekwa na yenyewe iweze kuivisha chungu. Siku njema.
Linda Madeleka Kwa nini asipigwe picha - au there is a big possibility kuwa the so called "mmiliki" is not the real mmiliki anaogopa akipigwa picha ikatokea kwenye magazeti itajulikana siye mmiliki halisi?? Its strange kwa kweli and it only happens in Tanzania.
Bernard Rwebangira Nashindwa kuelewa kama aliwapora kamera au alisema tu nao wakatii, yaani umetuita kuongea nasi alafu watuwekea masharti?? ingekuwa vipi wote wakaondoka na kumwacha mwenyewe? hii ni dharau kwa kweli.
Kaka Gano Wangegoma vipi wakati wamelipwa kabla ya kuingia mkutanoni??
Bernard Rwebangira Njaaa hizi zinatuuuwa na kuua taaluma pia @Kaka
Gulila Nuru lawama zangu kwa waandishi,lakini kwa kuwa najua maisha ya bongo kibaba haya na taarifa za kiintelijensia nazo zilichelewa achukuliwe picha hata kwa sniper shots? ili angalau tumuone tumfananishe asije akawa mwarabu wa Kariakoo halafu tunaambiwa General huko kwao! ama kweli nchi pekee duniani ambayo unakuja maskini unaondoka tajiri wa kutupwa ni hii nchi ya JK!
Evance Mvamila kuna tofauti gani ya kutokumfahamu mmiliki wa Dowans,na kuletewa kwa masharti ya kutokupigwa picha wala kuwa recorded na kuruhusu waandishi wachache kwa masharti hayo magumu. Suala linabaki vile vile hatumfahamu,hatuwafamu,wameshinda vipi tenda hatufahamu wala rais wangu hamfahamu... wajinga ndio waliwao.. walisema mababu zetu, mungu awarehemu
kwanini amekuja basi, tukisema kila siku waandishi wetu njaa imezidi,wanaona watu wabaya..mwandishi wa habari unaenda sehemu bila nyenzo za kuchukulia habari kwelii!!! huo ndio uandishi wa habari, tukisema walinunuliwa ili wathibitishe kuwa... mmiliki wa Dowans yupo na sio lodilofa wala ro..bert watabisha. waandishi wanaipeleka wapi fani hii
kaka sasa bora tutulie tuepushe msongamano.... haina tofauti na hadithi za paukwa... pakawaSee More
Christina Sifael Mbise Nadhani tunahitaji Tsumani iondoe tabaka hili kije kizazi kianze upya maana every corner ni uozo. Sijui nini kifanyike kusafisha bongo za watanzania. akili finyu sana! unapokea hicho ila ukirudi kwako umeme juu, elilmu ola, afya ola, barabara utalia, etc hivi vijisenti hivyo ndo vimekusaidia nini? watoto wako na wajukuu wako unawaandalia nini??? sh............!......!
Bernard Rwebangira KANYABOYAAAAAAAAA!!! MTAKE MSITAKE,
Adam Gwankaja wallah hii ni hatari. so helpless. extremely hopeless!!! mweeeeeeeeee
Hamis Shimye Adam usihukumu habari corporations pekee bali rejea ni magazeti mangapi yaliyotoa habari ile nakuona upi mwelekeo wao hivo nashwishikia kuamini huo ndio uandishi wa tanzania
Adam Gwankaja ‎@Hamis, nakubaliana na uchambuzi wako juu ya mwelekeo wa uandishi wa Tz. Sikuhumu NHcorp la hasha, nimewapigia mfano kwa vile mgongano wa kimaslahi wa RA ni dhahiri! Tukubaliane kuwa picha haiko clear! Ni chengachenga tu!
Asubisye Mwamfupe Adam, mmiliki alikataa kupigwa picha kwasababu yeye mwenyewe haonekani hata ukikutana naye sasa ungepiga picha nini?
Oswald Bankobeza HII NDO TZ. KUNA SIKU MTU ATAAMBIWA KUPIGA MAGOTI ASALIMIE NDO ARUHUSIWE KULA! Mchakato wooote ni wa kifisadifisadi hata huyo huenda ana lake jambo lakini TAA NNE DISCO kama kawaita si waende tusaidiwe kumjua? MBONA WANAKWEPA?
Rashid Mkwinda Duu!!! mnacheza na mmiliki wa DOWANS nini ana uwezo wa kuwalisha Watz kwa miaka kadhaa ijayo na ana vijisent vya kula hadi dunia iishe,vijipaparazi na vijikamera vyao vya Mchina wapi na wapi,gharama ya kijikamera chake haizidi hata gharama ya Tai au kamba ya kiatu cha Mmiliki wa Dowans nyie mnafanya mchezo na Mihela nini?
Emmanuel Arsenal Imani Ingekuwa poa sana maana wanatuzingua tu na michezo yao!
Bottom of Form

Monday, February 21, 2011

YA TUNISIA, MISRI, NA LIBYA- OLE KWA WATANZANIA VING'ANG'ANIZI; HAKIKA HAYATAPITA BURE


Kilianza Tunisia, kikajibu Misri, sasa kimenuka Libya. Upepo huu ni mkali!Unazitisha hata nchi za magharibi.Utavuma bara zima na zaidi!Wenye macho na wafahamu! Vyama vikongwe kama CCM na visome alama za nyakati! Wabunge waliodumu miaka 20, na bado wamo watambue! Wenyeviti wa vyama wa 'maisha' kina Mrema, Lipumba, Mtikila nk nk na wafunguke macho sasa!
Kutoka mtandao wa kijamii wa Face book  Lingson Gwankaja kuanzia Februari 20, 2011
Rosca Bugingo Kinanukia tz ukiweka nahaya matatizo ya G'mboto kama wahusika wakijifanya viziwi au vpofu itakula kwao watamsababishia boss wao kuwa mashakani dah,ila jamaa amekonda huyo mpk mapozi yake yamekwisha!!!
Lusajho Mwambipile Kwa sababu hili taifa ni letu wote, kuna haja ya kupokezana ili liweze kusonga mbele, sio kwamba wao ndio bora sana kuliko wengine. Haiwezekani mtu toka ajira yako ya kwanza ukiwa na miaka 23 ni mbunge mpaka kufikia zaidi ya umri wa miaka zaidi ya 60, i.e Mh. Anne Makinda (62) na wengine wengi. Kuna umuhimu wa kuwa na kikomo kwenye hizi nafasi za kisiasa maana watu wanajisahau kana kwamba hii nchi ni ya familia na ukoo wao.
Adam Gwankaja ‎@Rosca, tuendelee kumwombea mhe rais wetu!@ Lusajho, hata sheria ya ukomo wa muda kwa wabunge isipowekwa, yatawakuta ya Misri nk. Hamkani si Shwari tena. Mfano wa jimbo flani huko kwenu,mbunge aliyekuwepo kwa muda wa miaka 15, maendeleo ya...kafifia, yakadunishwaaaaa ile mbaya, wananchi wakakata tamaa, lakini wakaona hakuna mbadala.alipokuja kuingia mtanzania mwingine, haaaaa!! wananchi wakashangaa, kumbe inaleta maana kuwa na mbunge!!!miaka mitano tu ya awali, mambo yakawa yemebadilika sana. tumaini lilirejea. miaka kumi kumi na tano ya ubunge inatosha sana. watu wasigeuze kuwa permanent employment.See More
Linda Madeleka Miaka 15 bado tu mbunge? No ways! Binafsi ningefikiri miaka 10 inatosha - the thing is unapoingia ubunge si unajua kwamba unatakiwa kuwajibika kwa wananchi wako in terms of kuwawakilisha vyema na kutafuta mianya mizuri ya kuwaletea maendele...o wanajimbo?hakupaswi kuwa na eti "muda wa kujifunza"! sasa ukiwa makini from the word GO nina imani miaka 10 utakuwa umelitumikia jimbo ipasavyo - na kingine, ni pale wananchi nao wanapokuwa na mamlaka juu ya ubunge wako kwa maana ya wao kuwa na uwezo wa hata kukufukuza kazi au kukuita jimboni na kukufanyia tathmini ya uwajibikaji wako... hapo ndio patakuwa na raha na maendeleo ya uhakika katika nchi hii!See More
Rosca Bugingo ‎@adam hakuna kumuombea wala nini kaharibu nchi kila ki2 kimepanda bei hali yenyewe imekua ngumu kilakukicha mwana me cna ata hamu yakumuona kabisa wapo wanaoweza ebu 2wape nafasi nao wajaribu! Remember u never knw til ua av tried!! 2siseme nao niwalewale ebu 2wape 2uone, @lusajo ukisemacho nikweli kaka! Uvumilivu uki2iishia 2tafika pabaya!!
Rosca Bugingo Weona yametokea mbagala sasa G'mboto wa2 walewale then wanasema hawawezi kuwajibika kwahyo wanaona wa2waopoteza uhai kwao sawa 2!! No we cnt go that way lazima 2wawajibishe wao wakosalama ukicheka na nyani mabua lazima uvune ha2ko tayari kuwaona sura zao kila cku kwny tv eti bht mbaya, twice??!! No tc enough bora lawama kuliko hasara.
Lusajho Mwambipile Watu uongozi wa kisiasa wanachukulia kama ndo ajira zao za kudumu, ndi maana wanajisahau sana mpaka wanadhani ni zao binafsi wanaziingiza familia zao zote, sanasana ubunge na uongozi wa vyama vya siasa. Kukiwa na time limit itakuwa vema, hii nchi ni yetu sote
Adam Gwankaja Rosca afu argument wanayoadvance ni fallacy! Eti wanasema wanajeshi huwa hawajiuzulu! Wanaacha hoja ya msingi kuwa watz kwa mfano hawataki ajiuzulu uanajeshi! Hawataki ajiuzulu ujenerali!wanaongelea cheo chake cha 'kisiasa' cha u CDF! @Lind...a na Lusajho, maneno mazuri hayo! Na kwakuwa wabadilisha sheria ni wao, wanaweza wasitake kuweka uko! Pinda kama kawaida yake aliwahi kurecite ngonjera kama hii!kwa hiyo tujipange kuwamisri!kuwa tunisia kwa kuandamana majimboni na kushinikiza hata wasichukue fomu! Kina maua daftari hadi wamejimilikisha viti maalum! Tz the biggest political animal farmSee More
Rosca Bugingo ‎@adam dc tym wataachia 2 ha2jaamua hawawezi kushinda nguvu ya umma!! Hatawaziri wao nae anajifanya kiziwi anafikiri 2mepotezea 2nangoja 2 wa2 majonzi yapungue ndo 2lianzishe othrws km wanataka waendelee kubaki in power wa2ue wote ili 2candamane.
Linda Madeleka I fully agree with you - tuwafariji kwanza walioathirika na mabomu, halafu shughuli ianze, inasikitisha namna watu wasivyokuwa na uoga wa Mungu - yule yule aliyewaumba na kuwaachia pumzi mpaka dakika hii.
Rosca Bugingo Linda i blv dat ata ikiwakwakumwaga damu wataachia 2 and our bloodshade wl irrigate our victory serious i tel u 2kicheka nao 2taisha wenye wao wako salama saivi kila m2 anajifanya kaguswa kuuza sura zao 2!!@linda blv we can!!!
Oswald Bankobeza Mwanangu upo juu,unajua nakumbuka enzi zetu mitaa ya Kizwite-tulikuwa tunaamini mbegu haioti bila kuzikwa na kufa ndipo inatoa mazao mengi! So,hakuna aliyezaliwa na Uwezo wa Kuongoza au Kutawala milele. Ni Mungu pekee! LET ALL WHO HAVE EYES SEE AND HEAR WHAT IS GOING ON IN ARAB COUNTRIES. IT'S THE BEST LESSON.
Adam Gwankaja Ha haaaaa Oswald mwenyekiti wangu duu umenikumbusha mbali!umenkumbusha harakati!
Ipyana Mwaipaja Hayo mnayoongea ni point nzuri sana, tujitahidi yaingie katika marekebisho ya katiba mpya. Ubunge isizidi 10 years bwana!!Bottom of Form

Friday, February 4, 2011

WAPI TAARIFA ZA KIINTELIJENSIA hata watanzania wachanga 10 wanafukiwa ?


WAPI TAARIFA ZA KIINTELIJENSIA hata watanzania wachanga 10 wanafukiwa (wakiwa hai au wamekufa) katika shimo moja jirani na Hospitali ya Mwananyamala. Afu mwaunda tume! Wapelelezi wameshindwa jamani? Oh sorry, wako bize kujadili siasa! Too bad! Quo va dis Tanzania? Wanakupeleka wapi mamaland?

Top of Form
Alphonce Assenga Kweli yatia huruma, hizo tume za kuundwa kila mara si jinsi ya kula kwa wanasiasa tu.

Atieno Kashy Albert Mwisho wa mambo yote umekaribia!

Adam Gwankaja Wandugu unaweza kuwa sio ule mwisho, ama mwisho wa mwanzo, bali kwa yakini huu ni mwanzo wa ule mwisho!

Patrick Lusiano Tsere Adam. I need clarification. Waliotupwa ni vitoto vichanga au ni foetuses? Au ambao ni still born. Nisichoelewa shuka ya hospitali iltumiwa na wazazi wako wapi?

Rashid Mkwinda Mmhhh hili jambo lataka wasaa inawezekana ni watoto waliokufa kabla ya kutimiza miezi wakiwa matumboni ktk hospitali kubwa kwa hiyo waliona njia ya kusitiri ni kuwazika katika kaburi moja...hebu tujadili hili na kulichunguza kwa undaani zakidi z it inawezekana unyama wa aina hii kufanywa na binadamu aliyeumbwa Mwenyezi Mungu na kuzaliwa kupitia tumbo la mama? impossible

Kiongozi Patrick, nilichosoma na kuelewa na kwa mujibu wa tag (birth tag kwa maana hiyo) iliyokutwa pale ikimtaja mama mmoja inaonyesha pre mature ambaye kwa kiswahili nandhani mtoto aliyezaliwa njiti! Pia kuna taarifa kuwa saba walikuwa nj...iti na watatu walishafikisha umri wa kuzaliwa kabisa, ndo kusema walizaliwa na sio abortion!picha nilizoziona kwenye uwazi kwa kweli hata kama mimi sio tabibu, watoto wengine walikuwa wakubwa kabisa wajameni! Walikuwa watoto! Hata waandishi habari akiwemo sam mahela wa itv aliyekuwepo eneo la tukio alimbishia mganga wa mwananyamala mbele ya DC Lugimbana kuhusu kuwa watoto hao wote saba walikuwa 'foetuses' !! Wazazi wako wapi, na ni nani aliwafukia (sio kuwazika) ndicho ambacho mimi nadhani kinahitaji CID sio siasa za tume jamani!ikumbukwe hili limetokea siku chache tu baada za ripoti ya mtanzania mwingine huko mwanza kutoonyeshwa maiti au walipozikwa mapacha wake! What a sub culture in medical field hapa kwetu!? Disgusting!See More

Nuswe Mwakiluma ‎...ndivo walivyo viongozi wetu hawawezi kujadili masuala ambayo hayaathiri maslai yao moja kwa moja na ambayo hayana maslai kwao..watajadili tu namna gani tuilipe DOWANS...lini wananchi wanaandamana na polisi waweke risasi ngapi kwenye binduki zao...hicho tu basi lakini si vinginevyo...its too bad

Ileta Taguaba kweli kabisa @adam, Usalama wa Taifa katika nchi yetu ni kitengo cha ajabu sana na imeshajengeka mazoea ikitokea tukio la kusikitisha ndani ya jamii ndo mwanya wa kutoa fedha kwa wajanja ndani ya serikali, si unajua mishahara haitoshi, ..disgusting zaidi ni pale chombo kilichopo badala kilete ufanisi wanaunda kingine kibovu zaidi. .we kaanzishe kipindi kama kile cha jerry muro..kama hayajakukuta.so sad jamani...natamani kupata mwandishi wakuandika ya ndani ya serikali ye2..maovu yote tuyaanike na kusambaza ulimwengu kote..

Hiyo ni kazi ya Police. Shuka ya hospital imekutwa pale ushahidi tosha wametoka Mwananyamala. Hivi hiyo hospitali vipi jamani mbona vituko kila wakati. Kawaida watu wanakabidhiwa vitoto vyao wakazike wenyewe na inaonekana hao ni watoto sio ...vimimba.

Adam Gwankaja ‎@Ileta, umenena vema kabisa. Imagine we have experts wa upelelezi wa makosa ya jinai na africa nzima ni miamba(taarifa za kiintelijensia nilizopata), halafu ati mwaunda tume!@Lucy, kweli kabisa! Hata vingekuwa cvimimba, ndo mtupe jalalani? Kwa sisi wenye imani haba, tukijumuisha matukio haya mawili la bugando na hili, there must be some terrible businesss behind this!

Ileta Taguaba aibu.unaweza ukakuta ndo system nzima ya mahospitali ye2..kwa wale marehemu wasio na ndugu...uenda ndo njia watumiayo mahospitali ya serikalii,,,na serikali inajua hilo..maana mfuko husika uenda hautoshi kufanya mazishi ya heshima.u neva know?

Adam Gwankaja Am telling u @Ileta, it might be a common practice for some benefit! Ndo unajiuliza, wapi taarifa za kiinteligensia? Anyway there is an end to everything, and here come!so many qns to be answered!

Salome Kitomari kwanz aumeona huo muundo wa tume yenyewe?ni sawa na kesi ya mahindi kumpelekea ngedere

Adam Gwankaja Kweli kabisa@salome,aibu! Tumezidi maigizo!

Michael Emanuel Karau intelijensia wanadai "UDINI" umezidi huku maiti 10 zikizikwa shimo moja. ingetokea UK, leo hata bibi yangu pale Umbwe Kibosho angesikia na kuona BBC waziri au kiongozi husika akiachia ngazi

‎@Ileta ..do not talk about usalama wa Taifa u know that guyz they think wao ni everything....Usalama wa Taifa iz u,ambaye ukiona nchi inahujumiwa una react mara moja kuona hakuna hujuma inayoendelea,usalama wa Taifa unaowadhani ndio hao ha...o wapo tunao na madudu ya DOWANS yanatokea na matokeo ya uchaguzi yanachakachuliwa na mengine ni hayo vitoto vinazikwa shimo moja kungekuwa na usalama wa Taifa hayo yasingetokea,yangeibuliwa kabla hata ya kutendeka na watu wangewajibika...

''EWE NCHI TANZANIA ILIYOZALIWA KUTOKANA NA NCHI MBILI AMANI ULIYONAYO NI HAZINA INAYOTOBOLEWA MATUNDU MATUNDU PUNDE ITAVUJA NA KUSHUHUDIA YANAYOTOKEA NCHI ZINGINE,SIMAMA WIMA EWE TANZANIA MWENYEWE BAINISHA NANI ANAFAA KUWA MLINZI WAKO''See More

Kweli@Rashid. Nadhani TISS ni miongoni mwa idara za ku overhaul! Vichwa vyenye fikra za enzi za vita vya ukombozi kusini kusini mwa afrika visipewe majukumu makubwa idarani. Wao wanadhani usalama wa nchi ni kulinda viongozi; kumbe mambo yas...hageukam hivi sasa its about uchumi, umaskini, rushwa nk. Hivi kenya watangaze knjaro na hujuma nyingine maafisa wako wapi?wanafanya nini?kwanini tanzanite iliuzwa kenya zaidi kuliko tz inakochimbwa?karamagi alitiaje saini kihuni hotelini mkataba wa buzwagi na mikataba mingi ya kilaghai, TISS wako wapi?See More

Ileta Taguaba kweli kabisa @rashid, kila mwananchi anawajibika na ulinzi wa nchi yake, wakati jeshi la usalama tuliyempa dhaman ya usalama wa raia umeshindwa kazi, mpaka iundwe tume kulisaidia jeshi la polisi.. sio wanadhani @adam.ndo hali halisi...nimependa manano ya ngo ya sikika..ya kutaka tume hewa ivunjwe na kuletwa nyingine isiyohusika na govt..big up sikika..ila wamesikika kweli?

Adam Gwankaja Aiseee sikika wanasikika!wasiposikizwa na wenye mamlaka, watasikizwa hata na mawe! Sikika pana vichwa naviheshimu sana!

Ileta Taguaba wacha wasikike,,,bt adam hapa hamna kesi...maana unadhani serikali ilivyo bahili kwa raia wake,,ndo itaenda nunulia sanduku mimba zilizoharibika..the same is done @muhimbili,na hospital zote za serikali,hii ya mwananyamala i think ni bahati mbaya kwao hawakuzika vema..mbona hata kwe2 wa2 wazima.2nazikana juu kwa juu..yaani maiti juu ya nyingine..coz makaburi yamejaa...sembuse vichanga..serikali itamke tu ukweli..na si kujikanyagakanyaga

Salome Kitomari tatizo wenye shibe hawawajui wenye njaa,tuna taifa la wafunga mikanda na walegeza mikanda,walegeza mikanda ni bomu linaloandaliwa kulipuka baadaye

Adam Gwankaja Na ikumbukwe pia kuwa mwenye njaa hana miiko! Ni bomu kweli kweli!

Rashid Mkwinda Ni bomu punde litaripuka,punde litaangamiza jamii,punde litaangamiza vizazi,punde litaangamiza rasilimali zetu na kuifanya nchi yetu kuwa kisiwa cha Upweke katika bahari ya Wanyonge wadhulumika na Wadanganyika
Bottom of Form

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP