|
Mzee Sefu |
Mzee Thabit Sefu wa mjini Mbeya amekuwa kwa muda mrefu akitumbuiza kwenye hadhara mbali mbali mjini mbeya hususan za kisiasa. Ujumbe wa nyimbo zake katika ngoma yake yenye asili ya kingoni almaarufu kama DZOMBE umekuwa ukichoma moyo, kuamsha hisia na kufikirisha. Zaidi sana amekuwa nguvu kubwa ya kuwakusanya watu. Nilipofanya mahojiano naye mwaka 2007 alikuwa hakumbuki umri wake lakini kulingana na matukio anayokumbuka na kuhadithia alikadiriwa kuwa na miaka 80. Mzee Sefu amepitia mikasa mbali mbali ikiwemo kuchimbwa mkwara kwa kutumbuiza kwenye shughuli za VYAMA VYA SIASA VYA UPINZANI. Soma makala
HAPA.
Hivi sasa hali ya mzee huyu inaelezwa kuwa mbaya sana (Bonyeza
HAPA kufuatilia mjadala kwenye facebook). Si wanasiasa wa CCM ama wa Upinzani wanaomtupia jicho. Kama KONDOMU wamemtumia, wamefanikisha malengo yao, Washamaliza haja zao, WAMEMTUPILIA MBALI. Usanii ni laana nchini? kipaji ni balaa!!! Pole mzee SEFU.
0 comments:
Post a Comment