Pekua/search

Thursday, March 22, 2012

Lowassa na Bomu lake la ajira kwa vijana; kama kweli anaguswa afanye haya badala ya kuwa domo kaya


Kama kweli Lowassa anamaanisha na kuguswa na hili 'bomu', kwanini badala ya kupayuka tuu mikutanoni afanye machache yafuatayo:


  • Akiwa Mbunge, tena anayedaiwa kuwa na ukwasi wakutosha, basi abuni na kuanzisha kampeni ya ajira jimboni kwake, hususanan kipindi hiki ambapo jamii ya wafugaji inakabiliwa na changamoto ya kutafuta livelihood mbadala, kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.


  • Kwa nafasi yake ua ujumbe wa NEC ya CCM anapaswa kuishawishi NEC nzima, iielekeze serikali kufanya moja, mbili tatuuu kuhakikisha 'bomu lake' linateguliwa. Hajafanya hivyo badala yake anapayuka tu kwenye media.

  • Kwa nafasi yake ya Mwenyekiti wa kamati ya Bunge mambo ya nje, ulinzi na usalama - anayo mengi ya kufanya zaidi ya kutusumbua na upuuzi huu wa 'bomu' kwenye media. Angeweza mathalan akashawishi ofisi zooote za ubalozi kuanzisha vituo vya kufundisha Kiswahili ambapo wahitimu wa kiswahili wataajiriwa; angeweza kushawishi na kuhimiza viongozi wetu waongee Kiswahili pale wageni wajapo nchini jambo ambalo lingewapatia vijana wa kitanzania ajira ya ukarimani na ufasili; angeweza pia kuhimiza uanzishwaji wa kampeni ya kuwaandaa na kuwatafutia watanzania ajira nje ya nchi.

Kama hawezi haya yaliyo katika uwezo wake, asitusumbue. Atulie. Lakini pia mnaompenda mumshauri kwa kamsemo haka, 'he should Respect the today's King, so as he is respected when his turn comes, if at all he will live to see it come'

Tuesday, March 6, 2012

MGODI WA ALMASI MWADUI WAGUNDULIWA - hadi leo zaidi ya Karat milioni 20 zimeisha vunwa

Leo (Machi 6) katika Historia yetu 

Williamson mwenyewe

 Mwaka 1940 John T williamson Mkanada Mtaalam wa madini 'aligundua' ALMASI huko Mwadui shinyanga. alifariki miaka 18 baadaye na akazikwa huko huko Mwadui. Maisha ya huyu ndugu yanalo somo murua kujifunza.

Mgodi wa Mwadui unakadiriwa hadi kufikia mwaka 2008 kutoa Karati 20 million. Maswali mengine jiulize mwenyewe!!!


Soma zaidi kuhusu jamaa hawa HAPA

Thursday, March 1, 2012

KUANZISHWA KWA SERIKALI ZA MAJIMBO na BAADAYE MIKOA NCHINI - Leo (Machi 1) katika Historia yetu -

Bendera ya Tanganyika 1919 -1961
Leo (Machi 1) katika Historia yetu -

Mwaka 1926 Utawala Waingereza uliiganwanya Tanganyika katika maeneo ya utawala yaliyoitwa MAJIMBO (Provinces) kila jimbo likiongozwa na MTAWALA aliyeitwa Provincial Commissioner aliyewajibika moja kwa moja kwa GAVANA (Wakati huo akiwa D. C. Cameroon.

Mwaka 1962, siku kama ya leo, katika Tanganyika Huru, majimbo hayo yaligeuzwa majina na kuwa MIKOA, na hivyo kutwaa mahali pa majimbo yaliyowekwa na WAKOLONI mwaka 1926.

SWALI. Je, dhana ya ukoloni kwa wakuu wa mikoa/wilaya imebadilika? Wanaongoza au bado WANATAWALA? jinsi wanavyopatikana inaashiria uhuru au bado ni katika mfumo wa uteuzi wa Gavana/Rais?


kusoma mjadala unaoendelea FACEBOOK bonyeza HAPA

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP