Pekua/search

Tuesday, April 24, 2012

Serikali ya Kijerumani ilimfuta kazi Karl Peters alipo-misbehave. Haikusema, 'NI UPEPO, UTAPITA.'


Ni Leo (Aprili, 25) katika Historia yetu.

Karl Peters afutwa kazi ya Utawala huko Kilimanjaro.

Licha ya kazi 'nzuri' aliyofanya awali, Serikali ya Kijerumani ilimfuta kazi Karl Peters alipo-misbehave. Haikusema, NI UPEPO, UTAPITA.


Tarehe kama ya leo Mwaka 1897, Mtawala wa kijjerumani katika jimbo la Kilimanjaro, Karl Peters alifukuzwa kazi na serikali yake kutokana na ukatili wake wa kupita kiasi uliochochea migogoro mingi kati ya serikali ya kijerumani na wananchi.

Ikumbukwe hata hivyo kuwa kushamiri kwa utawala wa kijerumani huko Kilimanjaro na nchini kwa ujumla kulichangiwa kwa kiasi kikubwa na maujanja ya huyu jamaa, Karl Peters, kwa kupiga songi na kuwahadaa watawala wenyeji (machifu) na hatimaye kutiliana sahihi mikataba ya kilaghai (kirafiki). Walipogundua baadaye, jamaa akawageuzia kibao na kuwapiga vita vikali.

Adam Gwankaja Afu ukimwangalia vizuri pichani si anafanana na yule naibu waziri wa JK yule jamaa yuleeeee mwenye kubeba mibinduki miiingi nk nk!!! anapita tu.

Martin Andimile Mbila Mibinduki siyo? Aisee hao jamaa hawana msalie mtume. Ukituhumiwa tu unaondoka haijalishi ni kweli au si kweli. Point ni kwamba watu wameisha poteza imani na wewe na pia ku-waachia wengine wachukue nafasi yako si dhambi maana nao ni binadamu.

Adam Gwankaja kaka Martin Andimile Mbila kuna mengi makubwa ya kujifunza kwa hawa jamaa katika hili kuhusiana na jinsi tunavyojitawala leo hii. Hata Linda Madeleka asiyependa historia (aiogopa) atawafurahia hawa watu. 
The story goes; ukatili wa huyu bwana ulihusisha kuwabaka dada zetu huko uchagani. Na wengine kibao walikuwa wapenzi wake. sasa kama kanuni ya maisha ilivyo mwosha huoshwa, siku ya siku si akakuta mtumishi wake Mabruk anajishindia mmoja wa mahawara wake,Jagodja; weeeee Peters akawaka mbaya. akaagiza washtakiwe kwa WIZI na UHAINI, kisha wakanyongwa na vijiji vyao kuteketezwa. Sasa sikiza hatua za serikali ya kijerumani baada ya kuona huyu bwana anawaharibia. WAKAMFUTA KAZI. Akarudishwa ujerumani huko akapewa kazi nyingine kuacha UCHUNGUZI huru kufanyika. Hii ilikuwa kati ya 1893 na 1895. Ilipofika mwaka 1897 ndipo uchungizi ulipothibitisha tabia mbaya ya huyu bwana, akahukumiwa KUTUMIA VIBAYA MADARAKA, hivyo akafutwa kazi rasmi na kupoteza mafao yake yote. Kesi nyingine zilianzishwa, ila akatorokea zake UINGEREZAAAAAAAAAA. Linganisha na kulinganua na kinachoendelea nchi Tanzania.

Kujiunga na mjadala kwenye FACEBOOK Bonyeza HAPA

0 comments:

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP