HII NI TANZANIA MIAKA 48 BAADA YA MUUNGANO
HII NI TANZANIA MIAKA 48 BAADA YA MUUNGANO
PAMOJA NA HAYO TWAWEZA KUCHEKA PAMOJA - nduhu taabu |
Mwalimu Nashoni Mlewa wa shule ya msingi Mwamagembe, wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, akiwa darasani (darasa la Sita) shuleni hapo leo hii April 27, 2012.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo, bwana Daniel Kaji anasema shule hiyo ina wanafunzi wapatao 312 na walimu sita (ikiwa ni wa kike mmoja). kuna vyumba vinne tu vya madarasa hali inayowafanya wanafunzi wengine kusomea chini ya mti.
Najiuliza hivi ningekuwa mwalimu wa shule hii ningefurahi kufundisha chini ya mti? Ningefanya nini? hivi sasa naweza kufanya nini??? Je mbunge wa eneo hili anaona fahari gani? Mwenyekiti wa kijiji? Diwani? Wananchi wenye dhahabu nyeupe (pamba), mang'ombe na michele kibao, wanajisikiaje? Mkurugenzi wa halmashauri? Afisa elimu na wakaguzi wa shule? Asasi za kiraia, zinajisikiaje? TANZANIA INAGEUKA TANZIA KWA BAADHI YA WATOTO.
2 comments:
Hayo maswali unayojiuliza ni maswali yanayoulizwa na kila Mtanzania Mzalendo mwenye uchungu na nchi yake na watanzania wenzake. Ningefurahi kama ungetuwekea picha ya wanafunzi wanaosoma katika shule ambazo watoto wa "wenye nchi husoma" ili tutokwe na machozi kabisa. Kwa wenzetu ambao hawapati fursa ya kufanya kazi vijijini na kuona umaskini ulioko huko wanaweza wakadhani mpiga hiyo picha ni CHADEMA au katokea chama cha upinzani. Hawaamini kabisa kuwa hayo maisha ni ya kweli. Tunawanyima watoto wetu walioko vijijini hata starehe ya kusoma ndani ya jengo/darasa achilia mbali kuwa na dawati. Unaongelea habari za Diwani, Mwenyekiji, Mbunge n.k. kutoka sehemu hiyo ya Kishapu? Wenzetu siku hizi wamekuwa vipofu kwa mateso ya Watanzania!
Ukiwatafakari wenzetu ambao wamekamata mafungu ya umma, badala ya kutumia mafungu hayo inavyotakiwa wanakwenda kujenga manyumba ya kifahari ambayo hata hawaishi humo, majumba mengine wameyajenga vijijini na kuacha yanakaliwa na popo wakati wao wanaishi mijini!
Tuwaombee sana viongozi wetu Mungu awajaalie hekima ya kuwawezesha waone mateso ya Watanzania na wachukue hatua.
Nashukuru ndugu yangu. Kwa maneno uliyosema tayari ushatutoa machozi wengine sisi.
Hivi unajua kuwa huko Kishapu ndiko katika mwaka mmoja tu wa fedha, zimetafunwa shilingi BILIONI SITA kulingana na taarifa ya Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa fwedha za serikali!!!! moto waja.
Post a Comment