TUNAWEZA HATA KUFUGA FISI - Tunayo maarifa mengi
Tunayo maarifa mengi. Kwanini Hatuendelei kwa kasi zaidi?
Msanii wa ngoma ya asili ya Kisukuma (jina halikupatikana) akionyesha fiisi wakati kikundi chake kilipotumbuiza katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika kijiji cha Chela wilayani Kahama Februari 25, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Mjadala kwenye Facebook:
Shununa Isaack kaka adam,asb njema kwanza.huyo
jamaa ana kibali chakufuga hujo fisi?au jamaa mambo fulani...
Adam Gwankaja ahsante, na iwe njema sana na kwako dadaangu Shununa Isaack.
Hapo sasa kwenye swali lako ndipo tatizo linapoanzia. sheria zetu
nyingi ni za kipuuzi sana, maana hazizingatii traditional au ile
indigenous knowledge base. Zimeatikwa tu kutoka hukooo
ughaibuni. mfano ni Kwanini awe na kibali? Kwani kufuga mbwa twachukua
vibali? Usukumani, FISI ni mali aiseee. ha ha ha haaaaaa. Anaweza kuwa
mnyama pori au wa kufugwa, upo?? Sikiza sasa wapigania haki za wanyama
wenye mrengo wa kimagharibi!!!
Niitiwe Mwansasu Kaka huenda hata siyo fisi, binadamu wana mambo mengi huwawezi!!! Jiulize amempata wapi?
Adam Gwankaja
Niitiwe
Mwansasu, kwani mbwa tunawapata wapi? Hiyo ni indigenous knowldge
mwana wane. Usukumani fisi aweza kufugwa bila taabu ujue.
Niitiwe
Mwansasu Wenye kwao watanisamehe lkn Dom wanafuga punda ila kwa
baadhi ni kitoweo na kuwasaidia kubeba mizigo!! Sasa anawasaidia nini km co mambo
fulani....???
Adam Gwankaja
ha ha haaaaa dadaangu weye!!!! hata hayo mambo flan ni maarifa, ila ukristo
ulipkuja ukatuharibia sana, na tukazidi kuyaficha; tukayaficha yale distructive
na constructive kwa pamoja. moja ya matumizi ya fisi huku naambiwa ni USAFIRI!
Shununa Isaack nakubaliana nawewe kaka
adam.makatiba yetu sio.watuache tujifugie manyoka,fisi nk.mi ntafuga tembo na
jamaa simba.niwaone wezi.pia siku navuna meno yangu ya tembo nisione mtu
anasogea.pia kaka wale swala ntafuga kwa wingi kila siku kamoja kanaliwa.upo
hapo vyetu bwana
Niitiwe
Mwansasu Mpendwa wangu hayo mambo fulani yana faida gani kwetu?
Mbona tunazidi kuwa masikini wa kutupwa! Makubwa usafiri wa fisi unakuwaje?
Jamani hebu wamkumbuke mungu kwanza ili awasaidie!!!
Adam Gwankaja
Ha ha ha haaaa ushaanza fujo zako Shununa Isaack dadaaangu. Tamaduni ni muhimu.
majuzi hivi nilikuwa Nepal huko mashariki chini ya Himalayas, nimestaajabu
wanafuga tembo ujue. Hana fujo wala nini. Ziko nchi nyingine wanafuga
mbogo/nyati ujue.
Adam Gwankaja
Niitiwe
Mwansasu kwa hali iliyomo leo baada ya uharibifu uliofanywa na
ukoloni na utamaduni wao, nakubaliana na wewe. Lakini tumekosea sana kudhani
kila maarifa asilia ni dhambi. sio kweli. mfano mdogo, wamisionari waliwakataza
wazee wetu hata kutumia mitishamba, leo wamerudi na products za miti ile ile
(alovera kwa mfano) wanatufundisha kuitumia. So nalitazama suala hili kwa upana
namna hiyo. Kwamba yako maarifa yetu yanapotea, na kuzidi kupotea.
Kujiunga na mjadala: bofya HAPA
0 comments:
Post a Comment