J.A. Mwamsiku the Great Inspirator dies
A J Mwamsiku the Great Inspirator
dies
Ni leo (Julai 27) katika Historia
yangu
R.I.P Jubeck A. Mwamsiku |
Hapo mwaka 2009 aliondoka duniani kurejea kwa muumba, baba yetu
baada ya kupambana vikali na kansa. Alfajiri ile tulipopata habari ilikuwa
ngumu na chungu. Ila mwisho wa yote tunamshukuru Mungu kwanza kwamba alitupa
baba ambaye alikuwa rafiki, kiongozi madhubuti na aliyetupenda na kuwapenda
binadamu wenzake sana.
Wiki
moja kabla ya kifo chake mimi na Peter tulikuwa naye akitupa tumaini!
Akitabasamu kutupa moyo! Na tulipoagana kurudi Arusha nakumbuka alisema, “Nendeni
tutaonana Mungu akipenda. Nimefurahi sana kuwaona.” Naam alimaanisha tutaona
siku moja tusioijua lakini iliyodhahiri katika ulimwengu wa imani.
Swali
moja tu sikukuuliza ewe kiongozi wangu! Nilitamaani kukuuliza wiki ile ya
mwisho lakini ulikuwa mgonjwa zaidi. Nikaahirisha. Ni swali hilo tu ulilopona .
Hata hivyo namshukuru Mungu kwamba alikujaalia hekima kuu maana
ulistahimili mvua ya maswali tangu utoto
wangu. Nashukuru kwamba ulinijibu kwa uaminifu. Ulinipa misingi ya kuishi
katika maisha haya.
Wajukuu zako wanaendelea kupenda kujifunza |
Nilimuuliza
mama swali lile, naye alinijibu. Limenifungua macho ila ninamiss ungekuwepo
ningekuuliza mwenyewe. Wajukuu zako wakikua nami nikiishi sana, I will ask them
what they think about this qn.
Kilimo:
Kati
ya mambo mawili, ulisisitiza kilimo. Mechanizing agriculture japo ulipinga
pawatila. Naam tumeanza. Kaka Edom na Afyusisye wanaendelea. Wale vidume sasa
wamekuwa maksai, japo mmoja kawadhaifu tumembadilisha. Kubwa zaidi natamani
ungekuwepo japo nikusimulie mwanzo mzuri wa Gwankaja Creations Agriculture
scheme.
Elimu:
Wajukuu
zako wanaendelea kusoma. Naam watasoma vizuri kwa msaada wake Mungu. Msisitizo
wako katika elimu tunauendeleza na tutaendelea kusisitiza watu kujifunza.
Mama yetu (Mkeo), Tummenye, anaendelea kujitegemea |
Rafiki yako P, the senior anasema anamiss ulivyokuwa unamsomea. |