Je Wamjua ‘Mtu’ wa Kwanza kuona chanzo cha mto Ruvuma?
Je Wamjua ‘Mtu’ wa Kwanza kuona chanzo cha mto
Ruvuma?
Ni leo (Julai 21)
katika Historia yetu
Hapo mwaka 1886,
Askofu wa Kanisa la Anglikana, Charles Alan Smythies, alikuwa MZUNGU sio mtu wa
Kwanza kuona chanzo cha mto RUVUMA. Inaelezwa kuwa Askofu huyu alifika katika
chanzo cha mto Lujenda, naodaiwa kuwa chanzo muhimu cha mto Ruvuma.
Inasemekana kwamba
wakati askofu huyo alipokiona chanzo hicho, uvumi ulienea miongoni mwa wenyeji
kwamba kwa vile chanzo hicho kilikuwa na MASHETANI basi Askofu Smithies
angekufa. Hata hivyo askofu huyo hakufa kama ilivyohofiwa.
Vile vile yafaa
kukumbushana hapa kwamba Askofu Charles Allan Smithies ndiye alikuwa askofu wa
kwanza wa UMCA (University Mission to Central Africa) – ya Anglikana visiwani
ZANZIBAR hapo mwaka 1892. Leo hii miaka zaidi ya mia moja, karne nzima…Wanaharakati
wanaojiita wa kiislam wanachoma makanisa, ilhali pale mkunazini minara miwili,
Msalaba na mwezi) imekaa sambamba kwa ujirani mwema kabisa kwa miaka nenda
urudi bila fujo.
Bishop
Charles Allan Smithies succeeded Steere and he became the first bishop of UMCA
to be titled Bishop of Zanzibar the commemoration of Bishop Charles went
together with the Zanzibar to become a diocese, hence the Diocese of Zanzibar
was established 1892.
Kanisa KONGWE lililoko MJI MKONGWE huko TANZANIA VISIWANI |
0 comments:
Post a Comment