Janga juu ya Janga: Dharau ya Madereva kwa bodaboda
Dharau ya 'waendesha magari' kwa
bodaboda ni janga la kitaifa pia
Tangu ‘mchina’ alipochochea
mapinduzi ya kifikra nchini kuhusiana na usafiri, kumekuwa na ajali nyingi zinazosababishwa
na usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda hata baadhi ya watu maeifikia
hatua ya kuita bodaboda kuwa ni janga la
kitaifa.
Sababu nyingi zimeelezwa kuwa
chanzo cha ongezeko la ajali hizo ikiwa ni pamoja na kukosekana umakini,
kutojali na kutozingatiwa kwa misingi ya usalama barabarani ikiwemo udereva wa
kujihami kwa upande wa madereva wa bodaboda ambao wengi wao hawana hata mafunzo
ya msingi ya kuendesha vyombo hivyo vya moto.
Lakini iko sababu nyingine ya
kuongezeka kwa ajali za bodaboda na ambayo kwa bahati mbaya sana hainyooshewi
kidole mara kwa mara. Sababu hiyo ni DHARAU ya kupindukia miongoni mwa
waendesha magari dhidi ya bodaboda. Dereva wa gari kwa kujua kuwa vyombo vyao ni madhubuti kuliko boraboda wamekuwa wakiwafanyia fujo bodaboda na mara nyingi kuwaumiza. Ninayo mifano mingi inayoshuhudia hili, lakini
wacha niuseme huu mmoja tu nilioshuhudia
siku za karibuni.
Tunafika kituo cha mafuta pale Mlimani City, nashuka kwenye bodaboda
kupisha iwekewe mafuta…dereva wa bodaboda ambaye ni Rafiki na jirani yangu
anasogeza chombo chake kipate mafuta, mhudumu wa kituo cha mafuta anafanya kile
kinachopaswa.
Hilo likiendelea anakuja mwenye gari analisogeza karibu kabisa kwenye
pikipiki kisha anafungua mlango kiasi kwamba Rafiki yangu Katale anashindwa
hata kutoa mguu. Kila mmoja anashangaa. Bahati nzuri kwa ustaarab mkubwa,
dereva wa bodaboda, anahangaika kukinasua chombo chake hasemi hata neno. Mimi
naishia kutwanga picha tu na dada aliyekuwa anajaza mafuta kwenye bodaboda
anabaki kinywa wazi kwa mastaajabu. Picha hiyo inasema kila kitu.
Pamoja na matatizo mengi
yanayohusisha matumizi ya usafiri wa bodaboda ikiwemo ajali na vifo, ni ukweli
usiopingika kwamba bodaboda zimesaidia kupunguza matatizo ya usafiri kwa watu
wengi hususan wenye kipato cha kati kwenda chini. Pia bodaboda zimesaidia sana
kuchochea ari ya kujishughulisha miongoni mwa vijana ambao vinginevyo
wangekuwa vibaka wezi na ama majambazi
kabisa. Suala la kupunguza msongamano wa magari barabarani nalo ni moja ya faida
za bodaboda.
Ni vema basi tunapohimiza umakini
miongoni mwa waendesha bodaboda, tuwasisitizie pia waendesha magari kuwaheshimu
watumia bodaboda, maana nao ni watumiaji halali wa barabara. Katika kujilinda
madereva wa bodaboda wameanzisha umoja na wamekuwa na nguvu ya ajabu. Ukimfanyia
fujo mmoja wanashambulia zaidi ya nyuki au vikosi vya NATO. Hivyo hala hala
wandugu usijekuta unaumia kwa kuendekeza dharau
4 comments:
Adam, im just keen to know where that bodaboda guy got those words down his number plate! purely Luganda!
Thanks
hili ni tatizo,haliishii tu kwenye bodaboda ukipita njia ya bagamoyo or sorry barabara ya bagamoyo waendesha malori hawawajari hata wenye magari madogo, jana jioni tumenusurika kugongwa mimi na jamaa yangu, kisa tuna ka VW afu mshikaji ana FUSO. Hivyo msisitizo uwe wenye magari waheshimu matumizi sahihi ya barabara
Ha ha haaaa Unknown' those words are Bantu. It is a kihaya, I presume. All is for God something like that, or...all belongs to God. the haya shud be related to Luganda
Asifiwe ndugu yangu... nashukuru sana kwa kutupa upana wa suala hili. Hapo DHARAU ndiyo inayotuua. Kila mwenye kidogo hafai anapuuzwa na kunyanyaswa... Walisema wahenga wa kigeni...
Most people are bad..when they are strong they take from the weak.. most good people are weak, they lack strength to be bad.
Msemo mbaya kweli kweli..lakini yawezekana unao ukweli ndani yake.
Post a Comment