Ningekuwa daktari ningekubaliana na wito wa serikali
Ningekuwa daktari ningekubaliana na wito wa
serikali;
- Ningekubaliana na kauli ya Rais Kikwete..ama ningerudi kazini au ningejiendea huko kwingine.
- Ningeunga mkono kauli ya waziri mkuu litakalokuwa na liwe
- Uzalendo hauwezi kuhimizwa na viongozi wasio nao
Nimesoma makala kwenye gazeti la Raia Mwema toleo
la jana kwamba madaktari kadhaa wameitikia wito wa serikali kurudisha leseni
zao za udaktari kama walivyoagizwa kufanya. Na kwamba zaidi ya madaktari 50
kati ya takribani 400 walio’futwa kazi’ na serikali wanafanya mipango kwenda
nchi moja rafiki. La zaidi kwamba nchi kama Namibia, Botswana, Lesotho, Sudan
Kusini, Rwanda na Swaziland zinafanya jitihada ya kuwadaka wataalamu hao adhimu
na adimu waende wakafanye kazi huko.
Wakati tunapowapongeza madaktari walioitikia wito
wa serikali na kurejea kazini kufanya kazi bora liende-liwalo na liwe hata kama
huduma hazitaboreshwa, nawiwa pia kuwapongeza hawa wengine walioitikia wito wa
serikali kupitia mtendaji wake mkuu yaani Rais Kikwete kuwa waende wanakoweza
kupata mazingira bora ya kazi ikiwemo malipo bora zaidi.
Naam, naona wenzetu wameanza kuchukua hatua.
Serikali imechukua hatua kwa kuendelea kugoma kutimiza mahitaji ya madaktari
nchini na madaktari wengine wamechukua hatua za ama kurejea kazini au kurejesha
leseni na kuanza kutafuta maisha kwingineko. Kibarua kinabaki kwa wananchi kina
sisi kufanya maamuzi na kuchukua hatua dhidi ya serikali tuliyiweka madarakani
ikusanye kodi na kusimamia raslimali tulizojaaliwa nchini na kasha itupatie
huduma bora! Sijui tutaendelea kukaa kimya mpaka lini? Oh sorry, kumbe nasi
tumefanya maamuzi tayari, yaani kukaa kimya! Safi kabisa.
Nukuu
kutoka Gazeti Raia Mwema,
“Wapo
madaktari 50 tayari wamekwishakuzungumza na Waziri wa Afya katika moja ya nchi
zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara ili waende kufanya kazi huko na kwa kweli
kuna makubaliano watakwenda huko lakini wakifika wataingizwa katika mfumo wa
mafunzo ya kidaktari kwa vitendo (interns). Watakuwa chini ya uangalizi wa
madaktari wengine ili hatimaye kuwapa uhalali wa kitaaluma wa kuwa na leseni ya
udaktari,” kilieleza chanzo chetu cha habari.
Kusoma habari kamili Madaktari warejesha
leseni bonyeza
kiunganishi kifuatacho
1 comments:
wananchi tumegoma kwa kuwa hatujui kuwa sisi ndio wenye mamalaka kubwa kushinda hao tuliowakabidhi hayo madaraka,,
watu ambao hawana priority tumewafanya wawe viongozi wetu,,twataraji nini? zaidi ya liwalo na liwe? zaidi ya kusema nendeni mnakoona kunawafaa. Najiuliza yeye Kikwete anawahitaji hawa madaktari? wa nini wakati anaye wake peke yake? wa nini hawa wakati yeye anauhakika wa tiba bure mpaka Mungu amchukue? wa nini yeye wakati wanae wamo kwenye mfumo nao wanatibiwa bure, wanakula IKULU? Wa nini kwao? liwalo na liwe
Post a Comment