Moral obligations si kwa madaktari tu
Moral obligations si kwa madaktari tu
- Serikali iwe mstari wapamoja
- Viongozi wa sekta ya afya waonyeshe mfano
- Madaktari hawaruhusiwi kugoma lakini wana ukomo wa uvumilivu kama binadamu wengine
Dr Marina Njelekela CEO wa Muhimbili. |
Jana katika kipindi maalum kilichorushwa jana (16/7/2012)
usiku na televisheni ya taifa TBC kuhusu mgomo wa madaktari mambo kadhaa
yamenigusa:
Kwanza, Mtangazaji Shaaban Kisu, ameendesha kipindi
kile vizuri, ameuliza maswali ya mazuri kwa ujumla kiasi kwamba amenifanya
nione fahari ya TBC kuwa chombo cha Umma. Nampongeza kaka Shaaban kwa kutimiza
Professional Obligations vizuri pasipo kukiCCM au KukiSerikali kipindi hicho
kama wafanyavyo wengine.
Jambo la Pili nimeguswa na jinsi wasomi wan chi hii;
CEO wa MOI Prof Laurence Mseru Mseru na Mwenyekiti wa
Bodi ya wadhamini ya Hospitali ya Muhimbili, Prof Joseph Kuzilwa, walivyokuwa wakijitahidi kuongea na kuonyesha
uzuri kwa serikali. Mfano prof Mseru yeye anasema hali ya vifaa na vitendea
kazi pale MOI ni nzuri sana... wakati Dr. Marina Njelekela anasema vifaa pale
Muhimbili vipo vingi sana tu tatizo ni idadi ya wagonjwa kuwa kubwa...hata
hivyo anataja hata CT Scan, ilhali inaeleweka kwamba iliharibika na
haikutengenezwa kwa zaidi ya miezi sita!!! Usaliti wa kisomi huu.
Prof Kuzilwa |
Kubwa
zaidi ni msisitizo aliotoa CEO wa Muhimbili dr Marina Njelekela juu ya madaktari
kuongozwa na MORAL OBLIGATIONS. Alilisisitiza sana hili kuwa ndiyo mwarobaini wa
kutatua migogoro miongoni mwa wanataaluma na wataalam wa afya. Moral
obligations ama maadili ya kazi ya udaktari inahusiana na ukweli kwamba taaluma
na utaalamu huu unahusisha kuokoa maisha ya binadamu wenzao (pale Mungu anaporuhusu
hilo litimie).
Nakubaliana
na mtaalam na kiongozi huyu muhimu wa sekta ya afya. Hata hivyo, nadhani
ilikuwa sahihi zaidi pia kugeuza kibao hicho cha obligations kwa upande wa
serikali.
Haitoshi kuendelea kuwakandamiza wataalam wetu hawa wachache wa tiba
kisa, vile tu maadili ya kazi yao haiwaruhusu kugoma kama njia ya kuepusha
migogoro. Serikali isiyokuwa na maadili, isyojali moral obligations, inaziba
masikio na kuziba channels zote za kutatua migogoro na kutanzua kero za waganga
kwa sababu wanajua madaktari hawataweza kugoma.
Mtangazaji Shaaban Kisu (Kulia) |
Pia
nadhani ni wakati muafaka kuacha kuwalaumu madaktari eti si wavumilivu. Na hapa
ndipo kaka Shaaban Kissu ambambo alinikosha kwa kuuliza, hivi madai ya
madaktari ni mapya? Wasomi hawa wakabaki
wanajibu kwa kujiumauma.
Ufike
wakati kauli ya moral authority isisitizwe kwa kila mmoja lakini serikali ndiyo
iwe ya mfano. Iache usanii huku ikitegemea watanzania wengine wataendelea kuwa
waadilifu. Kilichotokea kiwe fundisho muhimu sana kwa kila mtanzania lakini
zaidi kwa serikali na vibaraka wake katika sekta ya afya.
0 comments:
Post a Comment