Pekua/search

Friday, August 24, 2012

Kinjekitile Ngware wa Majimaji atiwa nguvuni na wajerumani.


Kinjekitile Ngware wa Majimaji atiwa nguvuni na wajerumani.
Ni leo (Agosti 24) katika Historia yetu

Rais Kikwete lipozindua mnara wa kumbukumbu ya mashujaa wa Maji maji Agosti 2010 huko kilwa
Mwaka 1905, Wajerumani walimkamata mtanzania aliyekuwa chimbuko la ujasiri wa wana wan chi katika kuukabili uvamizi wa wageni toka ujerumani huko kusini mwa Tanzania enzi hizo. Huyu si mwingine bali Kinjekitile Ngware. Hatimaye madhalimu haya yalimnyonga shujaa na mwanafalsafa wa kitanzania Kinjekitile Ngware, tena yalimnyonga hadharani huko muhoro, Rufiji.

Jikumbushe baadhi ya matukio muhimu kuhusu vita vya maji maji:
Agosti mosi, 1905 vita ya maji maji dhidi ya Wajerumani iliyokuwa imeanza mwaka huo ilienea na kuyahusisha maeneo ya Songea, Masasi, mtwara, Lindi, Rufiji na maeneo mengine ya ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi nchini.
Baadhi ya mashujaa wa maji maji wakiwa wametekwa na madhalimu ya kijerumani
 Agosti 5 1905 wapiganaji wa maji maji walishambulia misheni ya kanisa katoliki Nachingwea na kumwua Askofu Cassian Speiss. Huyu alikuwa askofu wa kwanza wa kanisa katoliki jijini Dar es salaam. Kifo kilimfika askoofu huyo akiwa safarini kueneza dini huku Mukukunumbu, Nachingwea.

Agosti 14, vita kali na vilivyoua watu wengi vilipiganwa huko Liwale, Nachingwea kati ya wapiganaji wa maji maji na majeshi ya wajerumani. Vita hiyo ilipiganwa kufuatia kushambuliwa kwa boma ya wajerumani ya Liwale.
Septemba mosi, kitete kiliwapanda wajerumani maana mashambulizi ya wazalendo yalikuwa makli san asana sana, hivyo wajerumani walipiga simu nyumbani kwao ujerumani wakiomba majeshi ya ziada ili kuzatiti mapambano yaliyokuwa yakiendelea.

Chanzo kikuu: Mwanahistoria J. E.  Makaidi.


0 comments:

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP