Pekua/search

Thursday, January 31, 2013

UJASIRI WA KIFARANGA: Anayakana mazingira ‘mazuri’ kuUtafuta uhuru.




UJASIRI WA KIFARANGA: Anayakana mazingira ‘mazuri’ kuUtafuta uhuru.

Naam, tunahitaji ujasiri wa kifaranga (kama mtu binafsi na taifa). KIFARANGA Anayakana mazingira mazuri (ndani ya yai) yaliyomlea. Inafika wakati Anaamua kutoka nje na kuutafuta uhuru wa kweli, liwalo na liwe- vicheche vipanga mwewe nk...lakini huko ndiko inakopatikana fursa ya kumfanya kuwa KUKU halisi.

Wengi wetu nchini Tanzania tumenufaika kwa namna mmoja ama nyingine na Mfumo OZO uliopo...lakini tumuige kifaranga sasa...tusiendelee sana ndani ya ya yai!  Tunie kuubadili mfumo huu kwa dhati ya nafsi zetu. INAWEZA KUTIMIA. TUKITAKA KWA DHATI KABISA.

Thursday, January 17, 2013

Pongezi Salma Kikwete kuhutubia kwa Kiingereza siku hizi.


Pongezi Salma Kikwete kuhutubia kwa Kiingereza siku hizi.
Mama Salma Kikwete

Hongera mama Salma Kikwete kwa hatua uliyopiga. Uko juu mamaaetu!!! Kumbe unaweza kuhutubia kwa lugha ya KIINGEREZA siku hizi!!! Ila ndiyo umenivunja moyo ile mbayaaaaaaaaaa….

Nimebahatika kwa kushuhudia mwenyewe si kama nilivyokuwa naambiwa, kuwa mama yetu mama kiongozi, na kiongozi wa shirika la WANAWAKE NA MAENDELEO, Salma, nahutubia hadhara za kimataifa siku hizi kwa Kimombo. Nimemshuhudia mimi mwmenyewe kwenye TV (analojia) akihutubia kwa Kiingereza kizuri sana leo huko mjini Arusha.

Lakini Kwanini hiyo imenivunja moyo na kuisononesha nafsi…soma hapa:
Baada ya Rais Jakaya Kikwete kuingia madarakani mwishoni kabisa mwa mwaka 2005, mama Salma alikuwa akihutubia kwa lugha ya adhimu ya Kiswahili kwenye hadhara zote iwe za kitaifa na kimataifa. Alinikuna kweli kweli. Akanifanya niondoke mafichoni, nirejee kwenye fani, nikaishika kalamu makala gazetini nikaandika (http://www.upolesana.blogspot.com/2009/09/kujifunza-kwa-salma-kikwete-kuhusu.html) Sikusema jingine lolote bali kumwagia sifa mke wa rais wetu, mama yetu kwa kukienzi Kiswahili. Nikijua kwamba kwa hadhi yake ya ualimu, alikuwa akikijua kiingereza cha kutosha, lakini alichagua uanaharakati wa kukuza Kiswahili. Hakika nilimwelezea kuwa ni mama kiongozi wa mfano..

Niliona mama Salma akijipambanua vizuri sana katika matumizi ya Kiswahili. Nilifurahia hata kuanzisha asasi ya WAMA, yaani Wanawake na Maendeleo ikiwa katika jina la Kiswahili pengine tofauti na menginyo tuliyoyazoea, kama vile ‘Iko potyuniti fo alu ’. Nikamwona yu mama wa mfano kweli kweli ambaye hata alimpa changamoto mumewe, Rais wetu katika kuiendeleza lulu hii, ambayo si tu ni fahari kwetu bali ni fursa ya utajirisho.

Ziko faida kubwa kwa viongozi wetu KUTUMIA Kiswahili mbali ya fahari, iko faida kwamba kuna watanzania wanapata kazi kwa mfano, kufasiri na kukarimani. Kiswahili kinaongeza mvuto na ladha yake kunoga zaidi. Nikiri kwamba sifahamu, ni mjinga mimi mathalani, sijui inakuwa vipi viongozi kama Obama wakienda Korea, Japani koote huko, hivi viongozi wan chi hizo hulazimika kuongea Kiingereza, ambayo wengi tunaipamba kuwa lugha ya dunia na ya lazima? Aaaagh mama Salma….!!!!!!!!Naam, siku hazigandi…Lakini NAKUPONGEZA TU kwa kuwa mjanja zaidi kuweza kuumwaga ung’eng’e, ni maendeleo pia.


Thursday, January 10, 2013

peku peku - Zanzibar ni njema atakae na aje



Kwetu Zanzibar shwari tu twapekua kama kawa!!!!



Friday, January 4, 2013

Maneno ya Wanasiasa wetu kama kisa cha buibui na nzi



The Spider and the Fly - by Mary Howitt


Will you walk into my parlour?" said the Spider to the Fly,
'Tis the prettiest little parlour that ever you did spy;
The way into my parlour is up a winding stair,
And I've a many curious things to shew when you are there."
Oh no, no," said the little Fly, "to ask me is in vain,
For who goes up your winding stair can ne'er come down again."


"I'm sure you must be weary, dear, with soaring up so high;
Will you rest upon my little bed?" said the Spider to the Fly.
"There are pretty curtains drawn around; the sheets are fine and thin,
And if you like to rest awhile, I'll snugly tuck you in!"
Oh no, no," said the little Fly, "for I've often heard it said,
They never, never wake again, who sleep upon your bed!"


Said the cunning Spider to the Fly, " Dear friend what can I do,
To prove the warm affection I 've always felt for you?
I have within my pantry, good store of all that's nice;
I'm sure you're very welcome -- will you please to take a slice?"
"Oh no, no," said the little Fly, "kind Sir, that cannot be,
I've heard what's in your pantry, and I do not wish to see!"


"Sweet creature!" said the Spider, "you're witty and you're wise,
How handsome are your gauzy wings, how brilliant are your eyes!
I've a little looking-glass upon my parlour shelf,
If you'll step in one moment, dear, you shall behold yourself."
"I thank you, gentle sir," she said, "for what you 're pleased to say,
And bidding you good morning now, I'll call another day."


The Spider turned him round about, and went into his den,
For well he knew the silly Fly would soon come back again:
So he wove a subtle web, in a little corner sly,
And set his table ready, to dine upon the Fly.
Then he came out to his door again, and merrily did sing,
"Come hither, hither, pretty Fly, with the pearl and silver wing;
Your robes are green and purple -- there's a crest upon your head;
Your eyes are like the diamond bright, but mine are dull as lead!"

Alas, alas! how very soon this silly little Fly,
Hearing his wily, flattering words, came slowly flitting by;
With buzzing wings she hung aloft, then near and nearer drew,
Thinking only of her brilliant eyes, and green and purple hue --
Thinking only of her crested head -- poor foolish thing! At last,
Up jumped the cunning Spider, and fiercely held her fast.
He dragged her up his winding stair, into his dismal den,
Within his little parlour -- but she ne'er came out again!


And now dear little children, who may this story read,
To idle, silly flattering words, I pray you ne'er give heed:
Unto an evil counsellor, close heart and ear and eye,
And take a lesson from this tale, of the Spider and the Fly.

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP