Pongezi Salma Kikwete kuhutubia kwa Kiingereza siku hizi.
Pongezi Salma Kikwete kuhutubia kwa Kiingereza siku hizi.
Hongera mama Salma Kikwete kwa hatua
uliyopiga. Uko juu mamaaetu!!! Kumbe unaweza kuhutubia kwa lugha ya KIINGEREZA
siku hizi!!! Ila ndiyo umenivunja moyo ile mbayaaaaaaaaaa….
Nimebahatika kwa kushuhudia
mwenyewe si kama nilivyokuwa naambiwa, kuwa mama yetu mama kiongozi, na
kiongozi wa shirika la WANAWAKE NA MAENDELEO, Salma, nahutubia hadhara za
kimataifa siku hizi kwa Kimombo. Nimemshuhudia mimi mwmenyewe kwenye TV
(analojia) akihutubia kwa Kiingereza kizuri sana leo huko mjini Arusha.
Lakini Kwanini hiyo imenivunja
moyo na kuisononesha nafsi…soma hapa:
Baada ya Rais Jakaya Kikwete
kuingia madarakani mwishoni kabisa mwa mwaka 2005, mama Salma alikuwa
akihutubia kwa lugha ya adhimu ya Kiswahili kwenye hadhara zote iwe za kitaifa
na kimataifa. Alinikuna kweli kweli. Akanifanya niondoke mafichoni, nirejee
kwenye fani, nikaishika kalamu makala gazetini nikaandika (http://www.upolesana.blogspot.com/2009/09/kujifunza-kwa-salma-kikwete-kuhusu.html)
Sikusema jingine lolote bali kumwagia sifa mke wa rais wetu, mama yetu kwa
kukienzi Kiswahili. Nikijua kwamba kwa hadhi yake ya ualimu, alikuwa akikijua
kiingereza cha kutosha, lakini alichagua uanaharakati wa kukuza Kiswahili. Hakika
nilimwelezea kuwa ni mama kiongozi wa mfano..
Niliona mama Salma akijipambanua
vizuri sana katika matumizi ya Kiswahili. Nilifurahia hata kuanzisha asasi ya
WAMA, yaani Wanawake na Maendeleo ikiwa katika jina la Kiswahili pengine
tofauti na menginyo tuliyoyazoea, kama vile ‘Iko potyuniti fo alu ’. Nikamwona
yu mama wa mfano kweli kweli ambaye hata alimpa changamoto mumewe, Rais wetu
katika kuiendeleza lulu hii, ambayo si tu ni fahari kwetu bali ni fursa ya
utajirisho.
Ziko faida kubwa kwa viongozi
wetu KUTUMIA Kiswahili mbali ya fahari, iko faida kwamba kuna watanzania
wanapata kazi kwa mfano, kufasiri na kukarimani. Kiswahili kinaongeza mvuto na
ladha yake kunoga zaidi. Nikiri kwamba sifahamu, ni mjinga mimi mathalani,
sijui inakuwa vipi viongozi kama Obama wakienda Korea, Japani koote huko, hivi
viongozi wan chi hizo hulazimika kuongea Kiingereza, ambayo wengi tunaipamba
kuwa lugha ya dunia na ya lazima? Aaaagh mama Salma….!!!!!!!!Naam, siku
hazigandi…Lakini NAKUPONGEZA TU kwa kuwa mjanja zaidi kuweza kuumwaga ung’eng’e,
ni maendeleo pia.
0 comments:
Post a Comment