Unafiki sawa. Kujikomba powa. Lakini Uwanja wa ndege wa songwe kuitwa Kikwete, NO!
Unafiki sawa. Kujikomba powa.
Lakini Uwanja wa ndege wa songwe kuitwa Kikwete, NO!
Kama ni UNAFIKI na KUJIKOMBA basi huku kumetopea upeo...
SONGWE au MBEYA ni majina yanayofaa zaidi kuuita uwanja huo kuliko kuuita jina la Rais Kikwete..Yatosha tu kuwaenzi Nyerere na Karume...baaasi...kwenye viwanja vya ndege.”
SONGWE au MBEYA ni majina yanayofaa zaidi kuuita uwanja huo kuliko kuuita jina la Rais Kikwete..Yatosha tu kuwaenzi Nyerere na Karume...baaasi...kwenye viwanja vya ndege.”
Aidha mchangiaji mwingine kwa jina la Gingo alikuwa na haya ya kusema,
“SONGWE AIPORT KUITWA JK, HAPANA!
Sina chuki na rais Jakaya Kikwete, lakini hili la Uwanja wa ndege wa
Songwe Mbeya kuitwa jina lake natofautiana nalo. Nakubaliana na kuwaunga mkono
NCCR-MAGEUZI. Kama tumekosa majina mengine basi tuuite BENJAMIN MKAPA AIPORT.
Au twaweza kuuita majina ya vivutio vilivyoko mkoani Mbeya na mikoa
jirani. Majina kama KITULO (jina la hifadhi), Rungwe (jina la mlima wenye
Volcano), Ngosi (lile ziwa la maajabu kule Tukuyu), Nyasa (lile ziwa la
wilayani Kyela), nk.
NI MAWAZO YANGU.......
Ukweli ni kwamba majina ya Wanasiasa hayatusaidii hasa linapokuja suala
la kujitangaza na kutangaza sehemu zetu za utalii nk. Mnisamehe kwa kiswahili!!”
Kufuatilia na kushiriki kwenye mijadala kwenye facebook fuata viunganishi
kifuatavyo:
soma pia