Pekua/search

Sunday, March 31, 2013

Unafiki sawa. Kujikomba powa. Lakini Uwanja wa ndege wa songwe kuitwa Kikwete, NO!Unafiki sawa. Kujikomba powa. Lakini Uwanja wa ndege wa songwe kuitwa Kikwete, NO!


Kama ni UNAFIKI na KUJIKOMBA basi huku kumetopea upeo...
SONGWE au MBEYA ni majina yanayofaa zaidi kuuita uwanja huo kuliko kuuita jina la Rais Kikwete..Yatosha tu kuwaenzi Nyerere na Karume...baaasi...kwenye viwanja vya ndege.”

Aidha mchangiaji mwingine kwa jina la Gingo alikuwa na haya ya kusema,

“SONGWE AIPORT KUITWA JK, HAPANA!

Sina chuki na rais Jakaya Kikwete, lakini hili la Uwanja wa ndege wa Songwe Mbeya kuitwa jina lake natofautiana nalo. Nakubaliana na kuwaunga mkono NCCR-MAGEUZI. Kama tumekosa majina mengine basi tuuite BENJAMIN MKAPA AIPORT.

Au twaweza kuuita majina ya vivutio vilivyoko mkoani Mbeya na mikoa jirani. Majina kama KITULO (jina la hifadhi), Rungwe (jina la mlima wenye Volcano), Ngosi (lile ziwa la maajabu kule Tukuyu), Nyasa (lile ziwa la wilayani Kyela), nk.

NI MAWAZO YANGU.......
Ukweli ni kwamba majina ya Wanasiasa hayatusaidii hasa linapokuja suala la kujitangaza na kutangaza sehemu zetu za utalii nk. Mnisamehe kwa kiswahili!!”

Kufuatilia na kushiriki kwenye mijadala kwenye facebook fuata viunganishi kifuatavyo:

soma pia

0 comments:

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP