Naunga mkono 'ukorofi' wa wabunge 'wakorofi' Bungeni
Naunga mkono 'ukorofi' wa
wabunge 'wakorofi' Bungeni
Nachukua fursa hii kuwapongeza kwa dhati kabisa wabunge wa
Upinzani Bungeni wanaojitoa kimasomaso kukabiliana na kanuni na taratibu
kandamizi kwa ustawi wa taifa letu. Msingi wa pongezi hizi uko katika usemi
unaodai “Good People Disobey Bad Laws”
yaani Watu wema Hawatii Sheria mbovu. Shime
wabunge wa upinzani, endeleeni kutuondoa kwenye ka ‘comfort zone’ ketu
tulimodumu kwa miaka nenda rudi na kujikuta leo hii tumefika hapa taifa
limegota na kusuasua tu kwa kufanya mambo kimazoea.
Heri hili bunge linaloonekana la vurugu lakini mawaziri
wanalazimika kufikiria mara mbili mbili wanapojiandaa kuepeleka hoja zao;
kuliko bunge la ‘kishemiwa’ na ‘staha’
ambamo serikali inajiachia itakavyo kwa kujua itaungwa mkono mia kwa mia
asilimia!
Bora mkaonekana wakorofi kwa kuuliza mwongozo mara kwa mara
na kupigania haki na masuala muhimu yanayofunikwafunikwa kama kuumizwa kwa Dkt
Ulimboka na kuuawa kwa Mwangosi; kuliko kuonekana ‘wastaarabu’ kwa kutukana
mitusi mizito kama FUCK YOU!
Heri mkaonekana na kuitwa majina yoyote mabaya yaliyopo
duniani (comedians, wataka sifa, msiojitambua nk nk) mkizikinza kanuni na taratibu zinazodidimiza nchi kuliko mkaonekana
wastaarabu mnaounga mkono hoja mbofumbofu!!!
0 comments:
Post a Comment