Pekua/search

Friday, April 19, 2013

Utawala Bora Chimbuko lake Katiba yetuUtawala Bora Chimbuko lake Katiba yetu

Katika harakati za kufuta ujinga nimekutana na hii kitu kuhusu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa chimbuko la Misingi ya Utawala Bora:

       Wananchi ndio chimbuko la mamlaka na madaraka ya serikali; Ibara 8 (1)(a);

      Katiba ya nchi ndiyo sheria ya msingi (sheria mama) na sheria zingine zote hufuata masharti ya Katiba – Ibara 64(5);

      Ushiriki wa wananchi katika vyombo vya dola - Ibara 8 (1) (d), Ibara 21;
      Mgawanyo wa madaraka – Ibara 4;

      Serikali kuwajibika kwa wananchi – Ibara 8(C)


      Heshima kwa binadamu na utu wa mtu – Ibara 12;

      Utawala wa Sheria – Ibara 9(b);

      Usawa mbele ya sheria – Ibara 13.  Hiki ni kile kifungu kisemacho, “
Watu wote ni sawa mbele ya sheria na wanayo haki bila ubaguzi wowote, kulindwa na  kupata haki sawa mbele ya sheria.”
.

0 comments:

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP