Pekua/search

Friday, January 16, 2009

PLAU LINGEWEZA KUKUZA UZALISHAJI KAMA WADAU MBALIMBALI WANGEWEKA MSUKUMO

Teknolojia rahisi ya kulima kwa kutumia jembe la kukokotwa na wanyama ilikuweko na ilithaminiwa zaidi ya miaka elfu mbili sasa. Rejea habari ya Mtu mmoja tajiri kwenye biblia, aliyewaalika watu kwenye karamu.Mmoja kati ya wale ambao hawakufika, alitoa udhulu kwamba, amenunua ng'ombe 'maksai' anakwenda kuwajaribu, hivyo hawezi kwenda karamuni. Pamoja na ukweli huo, teknolojia hiyo haijaweka kuotesha mizizi sehemu nyingi nchini ili walau kuwaokoa watanzania dhidi ya madhila ya jembe la mkono.Pichani mkazi wa kijiji cha Mbambo, Rungwe, ndugu Ndula Mwakipesile ni miongozni mwa wakulima wachache wanaotumia 'plau'. Wakulima wenye majembe ya aina hiyo kwenye kijiji hicho hawazidi watano!! Ni nini msisitizo wa wanasiasa na wanaharakati?

3 comments:

Adfam Foya January 27, 2009 at 3:36 AM  

Adam
Napenda kukushukuru kwa kuandika juu ya matumizi ya plau katika kilimo. Ukweli kilimo cha jembe la mkono hakiwezi kutufikisha kokote. Japo tangu tunapata Uhuru serikali inasema jembe la mkono haliwezi kuletea mabadiliko ya kilimo, cha ajabu serikali hiyo hiyo inasema kwamba sasa ni Mageuzi ya Kijani 'Green Revoluation' na hakuna mikakati ya makusudi ya kuleta hayo mageuzi.
Changamoto nyingine pia ni baadhi ya jamii sio wafugaji wa wanyama wanaweza kuvuta plau. Kwa mfano kule Kigoma, baadhi ya maeneo ni vigumu sana kukuta ngombe. Hivyo mbadala wa plau ambao ni trekta au 'Power tiller' (sijapata kiswahili chake) bado ni vigumu kwa wakulima wengi kwani wengi wao hawawezi kununua na baadhi wanao pewa kwenye program za maendelo changamoto inakuwa ni gharama za uzalishaji.
Juu ya kilimo mengi yamesemwa na tafiti nyingi sana zimefanyika sasa ni wakati wa vitendo sio maneno.
Mtoto wa mkulima amesema 'Vigogo wajinyonge ili wawasaidie wakulima'

Nawasilisha
Adam Jackson Foya

Adam January 27, 2009 at 3:52 AM  

Nimekufahamu kaka.Ni kweli sana maneno uliyosema. Tunasema zaidi kuliko kutenda. Vitu hivyo vinahitaji zaidi utashi wa kisiasa. Huwa najiuliza sana, eti. Mfano suala tulilowahi kujadili suala la kueneza UMEME WA NGUVU YA JUA. Kwa nini serikali haikomalii?? Kwanini wadau wa sekta isiyo ya kiserikali hatukomalii?? kweli tuko serious na chochote? Hebu pata mawazo ndugu yangu tufanye nini zaidi kati ya haya - mimi na wewe? hataikiwa ni kukuza mjadala tu?

Maria March 14, 2009 at 3:22 PM  

Home sweet home

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP