Pekua/search

Tuesday, March 31, 2009

UBEPARI UMEFIKA MWISHO? MJADALA

Wanazuoni,
AMANI IWE JUU YENU.
Kama mjuavyo mwisho wa wiki liyopita ulishuhudia, maandamano makubwa jijini London ambapo wanaharakati na wana wa nchi duniani kote waliungana na kuandamana kuwafikishia ujumbe viongozi wa mataifa tajiri 20 duniani watakaokutana jijini hapa baadaye wiki hii.

ujumbe mkubwa ulikuwa WATU KWANZA. KINACHOPASWA KUOKOLEWA NI BINADAMU, SIYO MABENKI!!!

Kama vile MENE MENE TEKELI NA PELESI kwa ubepari, baadhi ya mabango yaliushutumu ubepari moja kwa moja kuwa kiini cha mwanguko/mporomoko wa uchumi duniani na kueleza bayana kwamba ubepari UMESHINDWA!! !

Kujionea baadhi ya picha na ujumbe katika maandamano hayo bofya HAPA. Kwa mjadala zaidi iwapo UBEPARI UMEFIKA MWISHO bofya HAPA (zaidi ya wachangia 5 wametoa maoni yao)
Wasalaam
Lingson
Mtoto Mpole sana

CHANZO: wanazuoni yahoogroups

URGENT PETITION TO KEEP UEL OPEN DURING G20 SUMMIT

TO SIGN FOLLOW THIS LINK:
http://www.petitiononline.com/openUEL/

Dear friends the University of East London (UEL) was supposed to host an alternative summit on April 1st in the context of the upcoming G20 meeting on April 2nd. Following the media and police hype about possible disruptions to the city, the University withdrew its support for the alternative summit. Subsequently, management of the University decided to close down the university all together on April the 1st and 2nd, cancelling lectures and closing the library, effectively trying to turn the university into a wasteland in the very moment when the university should instead be up to the task of hosting critical debate and be a hub of creative energies. As the text of the petition makes clear, this is not just about UEL, but about reclaiming universities and education in these times of crisis.
PLEASE FORWARD WIDELY -- PLEASE SIGN URGENTLY.
SOURCE:wanazuoni yahoo groups

Sunday, March 29, 2009

MARCH 28 MARCH:DEMONSTRATIONS TO KNOCK SOME SENSE INTO THE BRAINS OF G20 LEADERS- LONDON. MAANDAMANO JIJINI LONDON


What we want? PUT THE PEOPLE FIRST; When we want it? NOW!!!
BAILOUT THE PEOPLE; NOT THE BANKERS!!!!!!!



A section of the tens of thousands at the Hyde Park Rally -London on he 28th March!!!!

For more pictures click HERE

Posted by Picasa

Thursday, March 12, 2009

KUPIGWA KWA MZEE MWINYI - 'SECURITY IS LIKE A MYTH IT DOESNT EXIST'

(for the english version of the saga read here)

Niungane na watanzania wengi waliofadhaishwa sana. waliosikitishwa na kuumizwa sana kwa kitendo cha kupigwa kwa mzee Ruksa (kutazama kipande cha video kuhusu tukio hilo bofya hapa - chanzo:jamii googlegroups). nimeumizwa nafsi nilipoangalia na kutazama kipande hicho na kwa kweli ninashawishika kuamini kwamba hakiwezi kuhalalishwa au kuhalalishika kwa namna yoyote iwayo. Lakini tuna mengi ya kujifunza kwa tukio hilo. hivi usalama uko wapi?

Jamaa, Ibrahim Said (ambaye Suleiman Kova, kamanda wa kanda maalum ya dar es salaam ya kipolisi anajaribu kuanza kuziandaa akili zetu ziamini hayuko timamu) alitoka alipoketi, kajongeambele, akapanda jukwaani, akasogea kwa mzee ruksa, akajipinda (kama anapiga penalti, akamnasa kibao mzee wa watu!!!!).

Inashangaza na kustaajabisha kwa jamii ya kitanzania iliyoshibishwa imani ya kutisha kuhusu ufanisi wa 'vijana wa kazi' wa usalama wa taifa na majeshi yetu ya ulinzi na usalama (au ndiyo habari zile zile kama za 'tusiponunua mitambo ya Dowans eeeeh balaa linakuja!!!!). Katika jamii ya kitanzania ambamo mahela na mijifedha isiyokaguliwa inatumika kwenye kuwaandaa na kuwafunza na kuwastawisha vijana wa kazi, inakuwaje habari ya lijitu flani hivi kuinuka na kumnanga kibao si tu cha aibu bali cha haja pia, mzee wetu hadharani?

Ama kweli vijana wa kazi wapo tu kwa ajili ya kushughulika na matukio, si kuzuia matukio (reactive na siyo proactive), maana tumewaona walivyofanya mbwembwe za mitama na kumbeba mzobemzobe yule jamaa, lakini angekuwa na kisu ishakuwa tayari mzee ruksa keshadhulika, usiseme kuhusu bunduki na mabomu!!!

kwa tukio hili nashawishika kuamini kwamba, USALAMA NI KAMA IMANI TU, HAUPO POPOTE!!! Kwa waumini wa dini, UPO MIKONONI MWA MUNGU, kama msemaji mmoja alivyoliweka vema, SECURITY IS LIKE A MYTH, IT DOESNT EXIST!!!

Pole mzee mwinyi kwa mshtuko na maumivu,
Pole watanzania kwa kufadhaishwa na kufikirishwa,
Lakini zaidi pole wanausalama na wazandiki wote maana mnakazi ya kusafisha picha ya utendaji wenu legevu!!!

Sunday, March 1, 2009

KUNJI KILA MAHALI


Mamia ya wanafunzi wa vyuo mbali mbali vya elimu ya juu jijini London mchana wa tarehe 25 .2. 2009 waliandamana kupinga kupanda kwa ada za elimu ya juu.Wanafunzi hao walikusanyika kwenye viunga vya School of Oriental and Frican Studies (SOAS) jijini London kutoa dukuduku lao kutaka ELIMU IWE YA BURE NA KILA MWANAFUNZI ALIPIWE GHARAMA ZA KUISHI AWAPO CHUONI.Wanafunzi hao waliungwa mkono na taasisi mbali mbali zenye kupigania haki za binadamu.
Hawakupigwa mabomu ya machozi wala virungu havikutembea!!!!!!!!!

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP