Pekua/search

Thursday, November 5, 2009

UWAZI KATIKA KUIMARISHA UTAWALA BORA - Lugha rahisi itachochea mafanikio



UWAZI ni mojawapo ya misingi muhimu ya utawala bora. Sifa na misingi mingine ya utawala bora ni pamoja Demokrasia, Uwajibikaji, Utawala wa sheria,Uadilifu na ushirikishwaji wa wananchi katika kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kutathimini shughuli za maendeleo yao.


Njia mojawapo ya kuimarisha uwazi ni kuwapo kwa miundombinu endelevu na shirikishi tena jumuishi ya mawasiliano. Pichani ni bango la tangazo la ujenzi wa barabara lililokutwa na kamera yetu mjini Tukuyu likielezea kinagaubaga juu ya mradi wa ukarabati na matengenezo ya barabara ya tukuyu – Mbambo hadi ipinda. Taarifa zilizoko kwenye ubao huo zinaonyesha chanzo cha fedha, mkandarasi, msimamizi n.k taarifa ambazo tumezoea kuziona kwenye mabango ya aina hiyo. Kipekee tangazo hilo limekwenda hatua zaidi kwa kubainisha kiasi cha fedha kitakachotumika na muda wa kuanza na kumalizika kazi hiyo.


Hii ni hatua muhimu ya kupongezwa. Haina budi kuigwa na Halmashauri zote za wilaya, miji, manispaa na majiji, Wakala wa Barabara (TANROADS) na wadau wengine wote!!!!


Hata hivyo, kasoro kubwa katika bango hilo ni LUGHA iliyotumika. Msomaji kama mimi, ambaye nadema dema na kiingereza, analazimika kujiuliza hivi nani alilengwa kwa taarifa hiyo? tatizo ni nini hasa? Kama mlengwa ni mwananchi, kwanini isiandikwe taarifa hiyo katika lugha yake, KISWAHILI?


Wakati umefika tubadilike, na kulimaliza tatizo hili. Si ajabu halmashauri za wilaya kutoa tangazo la mizania ya mahesabu yake gazetini katika lugha ngumu na ya kitaalamu gazetini ‘consolidated audited financial sijui nini na nini balance sheet. kwa hakika badala ya kuwa balance sheet iliyokusidiwa taarifa hiyo kwa wengi wetu inageuka kuwa just a shit!!!


TAARIFA ZIWE RAFIKI KWA WASOMAJI NA KATIKA LUGHA INAYOELEWEKA KWA WENGI NCHINI, KISWAHILI!!!

0 comments:

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP