Pekua/search

Tuesday, April 26, 2011

MBINU ZA CCM NA MAKABURU KUBAKI MADARAKANI


SARAFINA: Oh kumbe mbinu za MAKABURU kuhakikisha wanabaki madarakani hazitofautiani sana na za CCM! usilete ubishi, rudia tena kuiangalia sarafina na kutafakari.
Top of Form
Mwasakafyuka Samson Ngoja nirudie tena, hahaah.
Saturday at 12:43pm ·
Adam Gwankaja rudia kaka, tafakari hizo mbinu, linganisha na kulinganua, kisha tathmini nafasi yako kama kijana wa Tanzania katika HARAKATI ZA UKOMBOZI WA TANZANIA KIUCHUMI aka UHURU KAMILI. lakini USICHUKUE HATUA. Tulia tuuuu
Saturday at 12:56pm ·
Hoclay Aterio Mganga Ili uwe kijana ni lazima uipinge CCM na uiunge CHADEMA? Kumbuka CCM ndio iliyosaidia kutoka kwa makaburu
Saturday at 1:55pm ·
Adam Gwankaja ha ha haaaa@Hoclay, hayo ya Kuipinga CCM na Kuinga CHADEMA umeyatoa wapi hapa? nawe ni mmoja wa wawewesekaji?Hoja iliyoko ubaoni hapa ni vijana, kwa itikadi zao, waitafakari na kuitathmini vizuri nafasi yao katika kuleta UHURU KAMILI kwa nchi yao TANZANIA.
Saturday at 2:04pm
Hoclay Aterio Mganga Si umesema mwenyewe jamani au mimi naongopa. Mbinu za makuburu loh sawa na za CCM wanataka kutawala. Kisha tathimini kijana nafasi yako.... Achana na ushabiki wa siasa, shabikia timu ya mpira wanasiasa ikifika kipindi cha uchaguzi wamwage sera kisha tuwachague. Sasa tunajenge nchi
Saturday at 2:08pm
Hoclay, endelea na yako kama lengo lako hapa ni ushabiki. Iwapo weye siasa na mpira sawa sawa, basi tafadhali tuachie kina sisi habari hizi (hata kama umepewa kazi maalum). Wenye mapenzi mema na CCM, wataelewa nisemachoo. wanatambua kuwa CC...M kilichopigania uhuru kusini mwa Afrika, sio hiki cha leo kilichojaa walanguzi na wachuuzi aka mafisadi wanaonyukana kila uchao. Wanaoitakia mema nchi hii watamaizi nasema nini! wenye nia njema na Tanzania wanajua uongozi na utawala si uchaguzi peke yake. Nchi gani utaijenga pasipo kutafakari nafasi yako kwanza kama raia? huo ndiyo wito wangu kwa vijana; TAFAKKARINI NAFASI ZENU KATIKA HARAKATI ZA KUILETEA NCHI UHURU KAMILI. Viva Tanzania.See More
Saturday at 2:16pm ·
Sasa kaka hasira za nini? Nani katumwa? Tatizo watu wanataka kufata yale mawazo amabayo ni yake lakini ukiwa na msimamo wako binafsi wanaona unatumwa kwani lazima mtu kuwa kama ww? Tokea enzi za Nyerere kulikuwa na Wahujumu Uchumi na tukiwa...taja ndio hao hao leo wamevaa ngozi za upinzani wakawateka macho vijana wenye fikra finyu kwa mgongo wa kizarendo. Loh jamanii, siasa hii ya kuwaambia wanaume ficheni vitambulisho vya kupiga kura vya wake zenu ili wasikichague kile chama chao. Kisha kumchagua umchague mwenyewe na kumpinga umpinge mwenyewe. Kijana tafuta Album ya Vitalik Maembe inayoitwa Hotuba ya Mfungwa, utayajua mambo mengi na kuachana na ushabiki ulionao. Mwisho wa siku huwezi kumzikia Mboe akimpinga Lowassa hadharani kama ni FisadiSee More
Saturday at 2:48pm ·
Hoclay hakuna hasira hapa!labda useme wewe ndiye mwenye hasira (projection) unaethubutu kuwafanya watu wasijadili siasa bali wakashabikie mpira!Usijibu kisichokuwepo. Kwenye mabano hujaambiwa umetumwa, bali 'hata kama umepewa kazi maalum' u...nasema mengi usiyoulizwa. Wito wa ubaoni hapa ni kutafakari na kutathmini nafasi yako kijana katika harakati za kitaifa kuleta uhuru kamili.Kama wewe ni kiongozi u mwanachama wa CCM,tafakari nafasi yako, na chunguza mbinu za kikaburu kuhakikisha unabaki madarakani, shauri zitumike mbinu bora za kidemokrasia, tazama minyukano ya makundi ndani ya chama chako, tafakari kama kijana, tambua nafasi yako kurekebisha mambo, sio porojo, uzandiki na kuweweseka! simpo kabisa. Tafakari! Je si fikra finyu kuitazama tanzania kwa lensi za CCM na CHADEMA kama ufanyavyo? Ukisikia harakati unadhani CCM vs CHEDEMA? Kijana tafakari, usiwe dodoki! TAFAKARIIIIIIIIIIIIISee More
Saturday at 3:00pm
Hoclay Aterio Mganga Fikra sahihi zinakuja na hoja sahihi. Je ni mbinu gani za kikaburu wanazotumi CCM?
Saturday at 3:18pm ·
Adam Gwankaja hapo sasa tunaenda vizuri: ndizo UTAFAKARI HIZO! Rejea SARAFINA, tena ndugu yangu mhakiki na mtaalam wa mambo hayo ya filamu. Rejea SARAFINA, TAFAKARI, KISHA HAKIKI HOJA YA MSINGI, "Oh kumbe mbinu za MAKABURU kuhakikisha wanabaki madarakani hazitofautiani sana na za CCM!" Ikanushe au uiunge mkono au toa mawazo mbadala kwa hoja hiyo! simpo kabisa!
Paul Celestine ‎@Adam, waswahili hunena kuwa asiyejua maana usimwambie maana na kamwe usimwamshe aliyelala...Mada tajwa inavutia na mtazamo wako una hoja hasa ukizingatia kuwa Afrika ni moja kimatabaka, kifikra, kidhana ya uzalendo, kiutawala, kisiasa, kitamaduni, kiubinafsi, kiupeo, kimaadili na kifalsafa. Epuka kusema SHIKAMOO kwa mantiki usiyoijua. Acha majuha yabebane huku ukiyakumbusha kuwa wafu huzikana wao kwa wao.
Saturday at 5:10pm · Like
Bottom of Form

Sunday, April 10, 2011

HONGERA SAMBWEE; HONGERA CHADEMA: OLE CCM

HONGERA SAMBWEEE SHITAMBALA (uliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA Mbeya) kwa ujasiri (maana si rahisi mwanasheria wa aina yako kuthubutu kuigiza kutojua na kutozingatia sheria kama ulivyofanya ulipogombea jimbo la mbeya vijijini). HONGERA CHADEMA -maana Zigo zito kama hili likikuponyoka sio mchezo, ni nafuu kubwa!! HALAHALA CCM!!(ahsante Frederick Katulanda kwa Picha)
Emmanuel E. Meela kaka kumbe the guy z just a puppet..? Am predicting that they are coming 2 an ugly end CCM watajuta na siasa majitaka zao.!!
Adam Gwankaja yetu macho tuuuuuu, maadam tunayo na mbongo za kutafakari Mungu katujaalia!!!
Junior Matukuta Karibu nyumban SHITAMBALA kwan ulikuwa mwana mpotevu bt umerudi nyumban na hatimaye baba(CCM) amekupokea.I like it!!
Adam Gwankaja ‎@Junior, its great indeed. Shujaa anaporejea, ili AFIE nyumbani pamoja na wenzake.
Junior Matukuta Unajua siasa aianzi ukubwan ila utoton na upinzani umekuja rasmi miaka ya 90 na CCM ipo tang 77 bac ata... na... ni CCM!
Emmanuel E. Meela nyumbani wapi.? Nyumba ipi.? hii hii chakavu yenye kuta kuukuu zilizojaa nyufa za kila aina.? Akarabie na ndani kabisa ili itakapoanguka imfunike na liwe ndio kaburi lake kama mwanasiasa uchwara....@Junior
Adam Gwankaja Duuh Hongera sana@Junior, naona una hoja nzitooo nzitoooo. Nimeipenda hiyo ya siasa kuanza utotoni. hoja maridhawa kabisa. Ila nikukumbushe kidoooogo tu kwamba mfumo wa vyama vingi nchini tanzania haukuanza 1992. Ndiyo mfumo uliokuwepo wakati wa uhuru. ndiyo mfumo uliotafuta uhuru na kuupata. Kama umri ni hoja, multiparty democracy is older!!, lakini HONGERA tuuu
Junior Matukuta Hv ww utakataa kwenu ata kama ni pabaya then uwezo unao wa kurekebisha? bt walio nje ndo wanajua thaman ya CCM@Emmanuel
Adam Gwankaja thamani ya CCM ni kubwa. Nichama pekee ambacho mwenyekiti anaweza kusema anataka iandikwe katiba mpya, lakini waziri aliyeteuliwa naye, ama mwanasheria mkuu aliyemteua, anaweza kupinga hilo, na kisha akaendelea kuwepo kwenye wadhifa huo. Uko sawa kabisa kaka
Junior Matukuta Kama unakumbuka vizuri wapinzan weng waliondoka CCM baada ya kukosa nafac za kugombea bt katiba c ya CCM bali ni ya TZ!
Emmanuel E. Meela junior shabiki wa siasa uliyepumbazwa na na siasa za propaganda..., huwa cpotez muda wngu kubishana na watu wa aina yako.!! Naamini unatambua uwepo wa Mungu..., so try 2 b God fearing hata palipo na maslah yako binafs.. Ni hayo tu
Mussa Mwangoka Kwa SHITAMBALA nilitegemea tena amechelewa sana.
a group of propaganda's pipo in the form of political part, we've to know that there some of 'mafia' is ruling some countries politically, and CCMs is among them, every one know that Tanganyika pipo & CCMs its like a group of ''Jerries'' in... the house of ''Tomies'' dancing and eating together, how this could be? If u had a standard mind u should know it, there is a game in the so called Tanganyika under CCM's pipo coming in the pipo's eyes like a duts, wisemen can see it like a high mountain,See More
Rosca Bugingo Ckuzote wezi au waovu hupenda giza Chadema icho ki2 hakuna so kakimbia kwenye chaka la majambazi wenzie, cunaonawalivyo na nyuso za furaha, bungeni kuna mashine chache2 zinakoboa na kusaga!
Mwamfupe Anyisile ‎@Junior Matukuta, unatakiwa pia kujua kuwa mabadiriko hayaji utotoni bali ukubwani maana, kama tutakuwa waaminifu hata kwenye madogo na kuwa watulivu na wenye kuhitaji kujitenga na Ubaradhuri'' utagundua kuwa CCM haijaanza mwaka 77, isipokuwa bendera ya chama ndiyo imeanza hapo, lakini itikadi ya CCM ni ukoloni in the new shape wachache wapate kula, wengi waishi kwa shida
Negwako Mwakibinga ‎!!!!??? Mwadada!
Adam Gwankaja Polytricks@Negwako.
Deborah Sangu ‎@ matukuta sio kosa lako kaka, kazana labda 2015 utapata udiwani.
Negwako Mwakibinga Mwagona Mwadada! Zimbombo?
Junior Matukuta Sarari iliyopita 2010 kura za maoni azikutosha bt safari ijayo nategemea utakuwa kampen meneja wang@Debby!
Adam Gwankaja ‎@Negwako wewe nawe!! ena wane nyinza sanyona! usiendeleza mi sijui. @Junior,ni vizuri kuutafuta uongozi/uana siasa, lakini inafaa zaidi tukiacha uvuvuzela. tukitazame chama chochote tunachokishabikia critically kisha tutoe mielekeo mbadala, sio kushabikia kila kitu kama unavyojaribu kufanya.samahani lakini, tehe teheeee, mie nyumba ya tope, sihimili vishindo kwi kwihiiiii
Deborah Sangu ‎@ matukuta, sahau kabisa kabisa, mnafki shitambala atakusaidia...
Tinson Nzunda Mwiba hutokea ulipoingilia. Kwa mwenye hekima hathubutu kuusukumiza utokee upannde wa pili.
Hosea Kapula tunahitaji watu wenye uwezo
Resty Nyamizi Nenda mwanakwenda,na kama umesahau chochote CHADEMA tutakuletea huko huko! makapi yote yatatoka na watabaki wale tu wenye dhamira safi.
Felix Mwakyembe Ilieleweka huyo, mwache kafuata UDC na viti maalum vya JK
Adam Gwankaja asalimie dunia. Mwisho wa uhuni huu hauko mbali.
Asifiwe Alinanuswe uhuni huu hauko mbali? hapana uko MBALI sana ndugu Adamu tena mbali mno maana wamewapanda kama mchicha si unajua uwingi wa mbeguze? sasa watatoka kama hawataki,, na mbaya zaidi kuna wepesi ambao hupulizwa na hao watokao,, na nzuri zaidi greens wanajua kuwafanya watu wasijue elimu ya uraia,, fikiria mtu hajui kuwa vyama vingi viliuwawa kwa kuwa na katiba mbovu,,, hawa matambala,,,, ooh sorry hawa watokao waende tu, maana birds of the same feather flock together
Rashid Mkwinda LIPO JAMBO LILILOJIFICHA NDANI YA CHADEMA AMBALO NADHANI WENGI HAWAJALIJUA NA KAMA LITAENDELEA KUWA HIVYO WENGI WATAONDOKA HUMO, NILIONGEA NA SHITAMBALA KABLA HATA HAJAFIKIRIA KUHAMIA HUKO KWA KIJANI...MUHIMU KUWEKA UMUHIMU KWA WATU MUHIMU WALIOSAIDIA KUKIFANYA CHADEMA KUWEPO HAPO KILIPO.
 Rashid Mkwinda NAKUMBUKA NILIWAHI KUZUNGUKA KATIKA OPERESHENI SANGARA NA VIONGOZI WA CHADEMA KATIKA MAENEO KADHAA YA MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI, NAAMINI VIONGOZI WA CHADEMA WANAJUA WAZI KUWA HIVI SASA CHAMA HICHO NDO KIMEANZA KUMEA VIJIJINI KABLA YA HAPO HAKUKUWEPO NA CHAMA HICHO....JIULIZENI NINI MUSTAKABALI WA CHAMA HICHO....KWA KWELI INATIA UCHUNGU, CKUAMINI KILICHOTOKEA LAKINI NAAMINI PIA SHITAMBALA AMEAMUA KUFANYA UAMUZI MGUMU AMBAO HATA YEYE MWENYEWE ANAJUA NI MGUMU KWA MASLAHI YA WATZ
Mussa Mwangoka Mkwinda kwani tatizo nini huko CHADEMA?.
Adam Gwankaja Naam@Mussa, Rashid atujuze! Tatzo mzee wa tamathali za semi nahau na methali sana huyu Rashid
Elias Mhegera Thanks Adam for your observaton he was indeed a liability to CHADEMA
Bottom of Form


Saturday, April 9, 2011

MASKINI JK! HATA LA KATIBA MPYA ATAKUWA MDEBWEDOOOOO!!!!


Maskini JK wetu. Kaporwa hata turufu yake muhimu ambayo walau ingemrejesha kwenye chati kwenye nyoyo za watz, yaani kuanzisha na kufanikisha mchakato huru wa kuandika KATIBA MPYA! Hawezi kuwa BABA MDOGO WA TAIFA. Hata kuwa KAKA WA TAIFA hataweza! Pole JK. Pole zetu Watanzania. Adam Gwankaja
Top of Form
Linda Madeleka Kafanyaje tena @ adam?
Muswada unaopelekwa bungeni unasomeka,' The Constitutional Review Act 2011' wengine tulitegemea usomeke, The New Constitution Act 2011'. Kwa mantiki ya jina hilo tu, ni moja kwa moja kwamba UMESHACHAKACHULIWA, kinachopendekezwa kufanywa na ...serikali ya JK sio tulichokitaka. Tunataka katiba mpya. Uandaaji wa katiba mpya ofkoz unahusisha mapitio (review) ya hii 'kuu kuu'. Mchakato/means justifes the end. JK aliahidi, na taarifa zinasema yeye hakuwa na tatizo na uandaaji wa katiba mpya, ila sasa KAPORWA NA CHAMA, NA WAPAMBE! wach litote!!!See More
Na nimefurahi nimeupata na nikaupitia kwa kina zaidi...it's all about SHIT in it.....na sielewi kwa nini ameamua "KULA MANENO YAKE MWENYEWE"....review badala ya new...ni nini hiki?? Na ategemee makubwa tu kutoka kwa umma kwa upuuzi uliokuwe...mo ndani yake....pamoja na kwamba MUSWADA UNAHUSU REVIEW ( aka uchafu na.1 usiokubalika na umma), ndani ya huo muswada ni sumu na uozo: 1. WANANCHI HAWARUHUSIWI KUIPINGA TUME NA MAAMUZI YAKE (hata kama wamechanganya na pumba??) 2. RAHISI ATAPITIA MAPENDEKEZO YALIYOKUSANYWA KUTOKA KWA WANANCHI na KUYACHAMBUA ndipo YAPELEKWE BUNGENI KWA AJILI YA RASIMU YA KATIBA na KUKAMILISHA VIRAKA VYA KATIBA...aka...GWANDA LA JESHI (nini maana ya katiba ya umma??).....amekuwa king'ang'anizi, TUME KUUNDWA NA YEYE..ni nini hiki!!??....TIBA ISIYOTIBU...safari bado ni ndefu.See More
Linda Madeleka Eeh! I have been so busy of late sijaweza hata kufuatilia! If this is the case then TZ'ans we have a long way to go!
Adam Gwankaja ‎@Linda, we endelea kuwa bi zee hivyo hivyo, utashtukia nchi ishachukuliwa huna habari. For ur info, the preseindent is proposed all the power to create and destroy, read here: Power to appoint the commission, to issue ToRs, appoint secretary, receive the report and analysis, to constitute the constituent Assembly without regard to the present Bunge.... mchezo hadi hapo? Haya ni matokeo ya kuendesha nchi kinafiki. walioandika wanataka kumpendezesha rais, enewei, we are here! wacha litote!
Linda Madeleka Hahaha! @ adam kwa kweli u-busy lazima uishe! But its sad hatuna wazalendo nchi hii!
Asifiwe Alinanuswe uzalendo limebaki kwenye makablasha ya maktaba kuukuu tu, nadhani wanataka kufanya trial without any controll, ngoja mwisho ufike,, kila mtu atakapojua kile asichokijua wale watakao jua kuwa heeee tunakuwa kama wajinga watataka kutokuwa wajinga tena, ndipo watasema to heelll with everything in GREEEEEEEEEN
Bottom of Form
 

Wednesday, April 6, 2011

KATIBA YA VIRAKA BADALA YA KATIBA MPYA: QUO VA DIS TANZANIA?


KATIBA MPYA pole poooole tunahamishwa kwenye agenda. kinachopelekwa Bungeni 'Muswada' ni “The Constitutional Review Act, 2011 wala sio "The New Constitutional Act, 2011" Na hii ndiyo Tanzania. Adam Gwankaja
Top of Form
Zarah Karavina tusibirie tujue nini kitafwata
Goodluck Mlinga Adam katiba mpya haiundwi kwa madai manne, wanachodai hao wanasiasa kupunguza madaraka ya rais kwenye vipengere kama kuteua ma rc,dc,wakuu wa nec,pm na uundwaji wa cabinet hivyo haviwezi kuleta katiba mpya
Oh I c! ila inaundwa kwa madai mangapi@Goodluck? Nadhani una narrow down suala zima kwa wanasiasa. Madai ya katiba mpya si ya wanasiasa au walau si ya wanasiasa peke yao. Miaka hamsini ya uhuru wa Tanganyika na 47 ya Muungano imeshuhudia ka...si ndogo ya maendeleo licha ya raslimali lukuki. hilo peke yake linatosha kutufanya tuandae katiba mpya. Kufanya maptio ya katiba iliyopo ni mchakato mmoja tu wa uundwaji wa katiba mpya ya wananchi. Sasa muswada ukiwa sheria, mapitio yakafanyika, je utapelekwa mwingine? Nadhani its time tuachekea utani. This his last card, mhe JK, rais wetu mpendwa. Asimame kidete kukwepa hila za wapambe wake wanokoSee More
Andulile Raphael Hii itakuwa katiba ya Kikwete pekee yake kaka, sasa wananchi katiba yao itakuwa ipi? Kila kitu uchakachuaji tutafika kaka?
Asifiwe Alinanuswe hawa jamaa wanapenda kufanya watu wote wajinga,, better they learn the signs

Pata nakala ya Muswaada HAPA

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP