Pekua/search

Tuesday, April 26, 2011

MBINU ZA CCM NA MAKABURU KUBAKI MADARAKANI


SARAFINA: Oh kumbe mbinu za MAKABURU kuhakikisha wanabaki madarakani hazitofautiani sana na za CCM! usilete ubishi, rudia tena kuiangalia sarafina na kutafakari.
Top of Form
Mwasakafyuka Samson Ngoja nirudie tena, hahaah.
Saturday at 12:43pm ·
Adam Gwankaja rudia kaka, tafakari hizo mbinu, linganisha na kulinganua, kisha tathmini nafasi yako kama kijana wa Tanzania katika HARAKATI ZA UKOMBOZI WA TANZANIA KIUCHUMI aka UHURU KAMILI. lakini USICHUKUE HATUA. Tulia tuuuu
Saturday at 12:56pm ·
Hoclay Aterio Mganga Ili uwe kijana ni lazima uipinge CCM na uiunge CHADEMA? Kumbuka CCM ndio iliyosaidia kutoka kwa makaburu
Saturday at 1:55pm ·
Adam Gwankaja ha ha haaaa@Hoclay, hayo ya Kuipinga CCM na Kuinga CHADEMA umeyatoa wapi hapa? nawe ni mmoja wa wawewesekaji?Hoja iliyoko ubaoni hapa ni vijana, kwa itikadi zao, waitafakari na kuitathmini vizuri nafasi yao katika kuleta UHURU KAMILI kwa nchi yao TANZANIA.
Saturday at 2:04pm
Hoclay Aterio Mganga Si umesema mwenyewe jamani au mimi naongopa. Mbinu za makuburu loh sawa na za CCM wanataka kutawala. Kisha tathimini kijana nafasi yako.... Achana na ushabiki wa siasa, shabikia timu ya mpira wanasiasa ikifika kipindi cha uchaguzi wamwage sera kisha tuwachague. Sasa tunajenge nchi
Saturday at 2:08pm
Hoclay, endelea na yako kama lengo lako hapa ni ushabiki. Iwapo weye siasa na mpira sawa sawa, basi tafadhali tuachie kina sisi habari hizi (hata kama umepewa kazi maalum). Wenye mapenzi mema na CCM, wataelewa nisemachoo. wanatambua kuwa CC...M kilichopigania uhuru kusini mwa Afrika, sio hiki cha leo kilichojaa walanguzi na wachuuzi aka mafisadi wanaonyukana kila uchao. Wanaoitakia mema nchi hii watamaizi nasema nini! wenye nia njema na Tanzania wanajua uongozi na utawala si uchaguzi peke yake. Nchi gani utaijenga pasipo kutafakari nafasi yako kwanza kama raia? huo ndiyo wito wangu kwa vijana; TAFAKKARINI NAFASI ZENU KATIKA HARAKATI ZA KUILETEA NCHI UHURU KAMILI. Viva Tanzania.See More
Saturday at 2:16pm ·
Sasa kaka hasira za nini? Nani katumwa? Tatizo watu wanataka kufata yale mawazo amabayo ni yake lakini ukiwa na msimamo wako binafsi wanaona unatumwa kwani lazima mtu kuwa kama ww? Tokea enzi za Nyerere kulikuwa na Wahujumu Uchumi na tukiwa...taja ndio hao hao leo wamevaa ngozi za upinzani wakawateka macho vijana wenye fikra finyu kwa mgongo wa kizarendo. Loh jamanii, siasa hii ya kuwaambia wanaume ficheni vitambulisho vya kupiga kura vya wake zenu ili wasikichague kile chama chao. Kisha kumchagua umchague mwenyewe na kumpinga umpinge mwenyewe. Kijana tafuta Album ya Vitalik Maembe inayoitwa Hotuba ya Mfungwa, utayajua mambo mengi na kuachana na ushabiki ulionao. Mwisho wa siku huwezi kumzikia Mboe akimpinga Lowassa hadharani kama ni FisadiSee More
Saturday at 2:48pm ·
Hoclay hakuna hasira hapa!labda useme wewe ndiye mwenye hasira (projection) unaethubutu kuwafanya watu wasijadili siasa bali wakashabikie mpira!Usijibu kisichokuwepo. Kwenye mabano hujaambiwa umetumwa, bali 'hata kama umepewa kazi maalum' u...nasema mengi usiyoulizwa. Wito wa ubaoni hapa ni kutafakari na kutathmini nafasi yako kijana katika harakati za kitaifa kuleta uhuru kamili.Kama wewe ni kiongozi u mwanachama wa CCM,tafakari nafasi yako, na chunguza mbinu za kikaburu kuhakikisha unabaki madarakani, shauri zitumike mbinu bora za kidemokrasia, tazama minyukano ya makundi ndani ya chama chako, tafakari kama kijana, tambua nafasi yako kurekebisha mambo, sio porojo, uzandiki na kuweweseka! simpo kabisa. Tafakari! Je si fikra finyu kuitazama tanzania kwa lensi za CCM na CHADEMA kama ufanyavyo? Ukisikia harakati unadhani CCM vs CHEDEMA? Kijana tafakari, usiwe dodoki! TAFAKARIIIIIIIIIIIIISee More
Saturday at 3:00pm
Hoclay Aterio Mganga Fikra sahihi zinakuja na hoja sahihi. Je ni mbinu gani za kikaburu wanazotumi CCM?
Saturday at 3:18pm ·
Adam Gwankaja hapo sasa tunaenda vizuri: ndizo UTAFAKARI HIZO! Rejea SARAFINA, tena ndugu yangu mhakiki na mtaalam wa mambo hayo ya filamu. Rejea SARAFINA, TAFAKARI, KISHA HAKIKI HOJA YA MSINGI, "Oh kumbe mbinu za MAKABURU kuhakikisha wanabaki madarakani hazitofautiani sana na za CCM!" Ikanushe au uiunge mkono au toa mawazo mbadala kwa hoja hiyo! simpo kabisa!
Paul Celestine ‎@Adam, waswahili hunena kuwa asiyejua maana usimwambie maana na kamwe usimwamshe aliyelala...Mada tajwa inavutia na mtazamo wako una hoja hasa ukizingatia kuwa Afrika ni moja kimatabaka, kifikra, kidhana ya uzalendo, kiutawala, kisiasa, kitamaduni, kiubinafsi, kiupeo, kimaadili na kifalsafa. Epuka kusema SHIKAMOO kwa mantiki usiyoijua. Acha majuha yabebane huku ukiyakumbusha kuwa wafu huzikana wao kwa wao.
Saturday at 5:10pm · Like
Bottom of Form

0 comments:

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP