Pekua/search

Tuesday, May 10, 2011

MITIKISIKO YA MUUNGANO - KUCHOMWA KWA MABANDA YA WABARA HUKO UNGUJA

Hii ya Wahuni huko Zanzibar kuchoma maduka ya 'Wa Bara' haina budi kulaaniwa na kuandamwa vikali lakini iwe ni salaam muhimu kwa watawala kwamba wanapaswa kuwa WASIKIVU zaidi.Ikiwafikia 'Wa Pemba' wa Kariakoo mbona itakuwa kazi kweli kweli!!! DHAMBI YA UBAGUZI NI ZAO LA DHAMBI YA SERIKALI KUKOSA USIKIVU.
Top of Form
Isaya James Mmh! Hili nalo neno!
Leah Mafwenga Mhhh sijui nani awaambie jamani
Adam Gwankaja salaam zitafika tu
Leah Mafwenga kwa njia gani we uadhani? ingawa nakubaliana na wewe zitafika tu ila sielewi zitafikaje
Adam Gwankaja hata zile mbaya na za kishenzi zaidi kama hiyo waliyotumia zenji. salaam zitafika tu
Leah Mafwenga poa nimekuelewa wangu
Arnold Samugabo Hawa jamaa hawatupendi sijui kwanini tunajipendekeza: watuambie mara ngapi tuwaelewe?
Leah Mafwenga mhhhhhhhhhhhhhhh!
Felix Mwakyembe ukweli hawatuhitaji japokuwa watu wenyewe njaa tupu
David John Dhambi hii ni mbaya sana, tena Serikali iwachukulie hatua haraka wale wote wanatuhumiwa kuhusika na kitendo iki cha kinyama ktk taifa letu...!
David John Dhambi hii ni mbaya sana, tena Serikali iwachukulie hatua haraka wale wote wanatuhumiwa kuhusika na kitendo iki cha kinyama ktk taifa letu...!
David John Dhambi hii ni mbaya sana, tena Serikali iwachukulie hatua haraka
David John Dhambi hii ni mbaya sana, tena Serikali iwachukulie hatua haraka wale wote wanatuhumiwa kuhusika na kitendo iki cha kinyama ktk taifa letu...!
Ninyi mnadhani hakukuwa na taarifa zozote za ki inteligencia? japo police ni ya muungano lakini police waliowengi ni wazanzibar. Wananchi wengi wa Zanzibar wanaona Muungano unawanufaisha wanasiasa na watu wenye pesa, lakini kwa walalahoi ha...See More
Umenena vema sana Baraka Loya Mwambipile. WAPI TAARIFA ZA KIINTELIJENSIA? Hata hivyo nadhani hao 'wananchi wengi' wa zenji si kweli kwamba wanaona muungano hauna faida kwao, ila ni wanafiki may be. Je hawajui kuwa maduka ya KWA MPEMBA yako ...See More
Mimi ninayasema haya kaka nipo huku na nimeyaona yoote hayo na wapo wachache wanaoyatambua hayo. Narudia tena, wananchi wa kawaida wanaona wanaofaidi ni wenye pesa/matajiri na wanasiasa, mwananchi wa kawaida halioni hilo, wanaona ni sawa tu...See More
Gulila Nuru Tuwaanzishie wapemba walioko huku,kama hawawezi kuwavumilia wabara wetu kwanini sisi tuwavumilie? serikali inasemaje? wasijifanye wao watakatifu wakati wanachuma kwenye ardhi yetu na tunawaita ndugu wao wanatufanya kafiri,SIAFIKI MUUNGANO JAMANI!
uko sawa Baraka, lakini haingii akilini sana kwamba hawaoni faida. It is something they are made to believe hao maamuma, chanzo kiko mahali pengine kabisaaa, yaani nafsi za wanasiasa na wazandiki wengine. HIVI MWANANCHI WA KAWAIDA NI NANI huko Zenji? Hawa watumishi, wafanya biashara wadogo, wakati na wakubwa, hawa wanasiasa nk mbali mbali waliosambaa na kutapakaa huku bara, wametoka wapi? Wamedondoka kutoka mwezini? Hawana udugu na hao 'wananchi wa kawaida?' sio kaka, dada, shangazi, binamu, mjomba, baba na mama wa hao wananchi wa kawaida? Nani haupendi muungano? nani anadhani hafaidiki na muungano in real sense na kwa sababu gani? Lakini pia tujiulize kwanza, wazanzibar wanaoona hawanufaiki na muungano, WALITAKA WANUFAIKEJE? Wawe wakibebwa? Wakitawadhwa? NAAM, TUNAHITAJI KUJADILI HILI. TATIZO SERIKALI TULIYONAYO IMEPOTEZA UHALALI. INA HOFU. INA MASHAKA. HAIJIAMINI. NANI ATASIMAMIA MJADALA HUU?
Mimi nakuomba siku moja njoo kisiwa cha Pemba, halafu ufanye kama reseach fulani. Karibu kipindi ambacho ntakuwepo huku, maana sio wakati wote nakuwepo. Then yote hayo tunayoyaongea uta prove. Nasema hivi watu walioko bara hawatofautishwi na watu wa Zanzibar wowote ambao wako nchi za nje. Yaani bara ni sawa na nchi zingine tuu, kwamba unaweza hata kwenda kuomba msaada kama Tanzania inavyoomba misaada nchi zingine. Hivi unajua kuwa wewe hapo huwezi kumilki/kununua ardhi Zanzibar lakini wao wananunua tu bara mpaka nasikia wametengewa na eneo huko Bagamoyo kuwa kama la Zanzibar? Wanatambua kuwa ndugu zao wengi wako bara, lakini wakiwa nchi nyingine kama walivyo na ndugu hata uarabuni. Wanawafukuza wabara kama nasi kule kariakoo tunavyopambana na wachina kuuza ama kufanya umachinga wakati hata sisi waenyewe wa Tz tunaweza. Hapa ni kwamba kuna haja ya kuujadili kiupana muungano. And for sure kama kutakuwa na kupiga kura kwa wa Zenji kuwa muungano uwepo ama usiwepo, wangi wao watasema uvunjike kabisaa, wala hawautaki.
Felix Mwakyembe yote hayo yanayokana na kuwadekeza, niliwahi comment kuna siku kila Mzanzibari atakuwa kiongozi, Bara imewadekea sana tangu enzi za Mwalimu, hawa jamaa ni wale wenye chako changu lkn changu ni changu, ni wabaguzi wakubwa linapokuja sula la Tanganyika na Zanzibar
‎"hawa jamaa ni wale wenye chako changu lkn changu ni changu, ni wabaguzi wakubwa linapokuja sula la Tanganyika na Zanzibar" kaka Felix, tutazungumza mengi sana, lakini hawa jamaa hapo ndipo waliposimamia. Na hilo ndo kosa kubwa sana lililofanyika. Ndio maana wao wanazionesha waziwazi dalili za kuuvunja muungano lakini uongozi wa juu hautaki kulitazama hili jambo, wameweka pamba kwenye masikio na macho yao yana makengeza kiasi kwamba hawasikii wala hawaoni. Swali ninalojiuliza mimi ni je sisi wananchi wa kawaida tufanyeje? hapo ndo ninapokwama mimi binafsi
Felix Mwakyembe Baraka, nimekulia Zanzibar na kusoma huko tangu darasa la kwanza, nawaelewa sana so thinking yangu juu yao inatokana na experience ya tangu utoto, wabara tu wavumilivu saana, hata shuleni tulitengwa kiaina, kukitokea uharibifu wowote shuleni mnakusanywa watoto toka bara, etisisi ndo wakorofi, lkn uhuni wao wa hadi kulawiti vitoto vidogo hawausemi, kwangu Muungano hauna faida kweti heri uvunjwe
kwa kweli sina uzoefu sana zanzibar. Nimefanyakazi Unguja miezi minne tu, intennsively. Pemba sijafika bado.Siwezi kujisifu kujua hali halisi ya huko, lakini mambo flani flani ni dhahiri. Naamini pamoja na maelezo yenye hisia ya Baraka na Felix kwamba hapo Wabasiasa na viongozi wengine toke huko wana hatari zaidi kuliko 'wananchi' wa kawaida wa Baraka. Viongozi wanachochea hali hii.Ni viongozi wa vyama na serikali ndiyo waliopigania Wimbo wa taifa lao, ndiyo waliotaka bendera yao na ndiyo waliobadili katiba ya nchi yao. Hebu endelea kujiuliza hili swali dogo, Unguja ni kisiwa kidogo tu, ZILIKUWA WAPI TAARIFA ZA KIINTELIJENSIA, hata ufedhri huo ukafanyika ? - watu wakakusanyana, wakala njama, wakajiandaa, hadi wakatekeleza azma yao? Kama ulivyosema felix kwenye wanabidii, hivi wabara ndiyo mafirauni zaidi hapa nchini? Baraka, kosa kubwa kubwa la viongozi wetu ni KUKOSA SIFA NA HIVYO KUPOTEZA KUJIAMINI. Kasoro kubwa ni kwamba Tanzania Bara haina mtetezi popote pale. Maana kwa mujibu wa katiba Rais wa Muungano ndiye msimamizi wa masuala ya bara yasiyo ya Muungano, he is two in one. Mwinyi alitutetea sana. Its time kabisa, we openly discuss haya masuala na kama vipi muungano na tuuwache, jamani. Baraka jiandae kurejea kaka. Hutakufa njaa, aseeee!
Kaka Adam kufanya kazi kwangu huku sio kwamba nimekosa sehemu ya kufanya kazi! hapana bali ilikuwa ni katika kuudumisha muungano na ukizingatia niko serikalini na kazi ninayofanya ni ya muungano, kwa hiyo kwa haya yanayotokea ndo nazidi kujifunza. Ila ninachoshukuru ni kwamba kazi yangu ni profesional so hakuna mtu anayenibughudhi kwa mimi kufanya kazi hii, japo huwa kunakuwa na vijineno vya hapa na pale vya nao wabara hao, kwani hizi kazi sisi hatuziwezi? lakini ningetaka kuhama ni kuomba tuu na kwa issue za kisiasa wala maboss hawawezi kunikatalia. Kwa hiyo uwepo wangu huku sio kwamba nanyanyasika , hapana, nipo naishi kama nyumbani ila by being carefull maana huwezi jua wanakufikiria nini.
Kwa namna wanavyofanya wazanzibar hata sioni haja ya kuwa na muungano na ingekuwa amri yangu ni kuuvunjilia mbali kabisa.
Sawa Baraka Loya Mwambipile, ni vizuri kujifunza kama ufanyavyo, hata hivyo si vema wapemba wakafika pahala wakadhani tunaenda huko kuganga njaa kama wanavyohemea misosi huku kwetu, na ndiyo msingi wa kukwambia jiandae kurejea kwetu, neema iko tele. Vijineno kwenye kazi ni kawaida, hata tulioko huku vipo. Lakini tukubaliane naposema hawa washkaji niwapuuzi; wanapodai kuwa hizo kazi mnazofanya huko wao wanaziweza, ilhali wakijua fika kuwa ndugu zao kibao wanafanya kazi upande huu wa Tz. Time is a good ticha, WE WAIT N SEE.
19 hours ago · Like · 1 person
Bottom of Form

0 comments:

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP