Pekua/search

Wednesday, June 13, 2012

CCM KILIVYOKUCHOKWA, KUPOTEZA DIRA NA MWELEKEO-Shairi

Kolimba tulimsurubu,
Na kusababisha ububu,
Ukweli kutohutubu,
Kauliye kuiharibu.

Hakustahili hukumu,
Wala kumshutumu,
Na kumfanya haramu,
Na kumrushia sumu

Ukweli aliusema,
CCM haina wema,
Imeipoteza neema,
Imeleta hujuma.

Imepoteza dira,
Kwa uongozi wa hira,
Imepitwa na majira,
Haina tena sura.

Mimi najiuliza,
Nani wa kunijuza,
Hivi kweli tunaweza,
Kuwaondoa hawa vilaza.

Mimi si mahoka,
CCM nimeichoka,
Nimeitupa kama taka,
Kuyaondoa mashaka.

Ni Sanaa tu kukuza lugha nisiwe adui ingawa ......

Chanzo: Mwamfupe Anyisile: Jukwaa la Umoja Village huko facebook. 
 

0 comments:

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP