Pekua/search

Friday, June 29, 2012

Serikali iliyogoma inapofukuza madaktari waliogoma, wananchi wafanye nini???


KUMBE FUKUZA FUKUZA HII INAWEZA KUTUFIKISHA MBALI EEE

'Hakutakuwa na victimization..lakini ukipigwa na majambawazi au kugongwa na gari usijesema ni silikali, sawa?'

SERIKALI ILIPOGOMA KUTEKELEZA MAKUBALIANO YAKE NA MADAKTARI JUU YA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA IKIWEMO MASLAHI YAO,  NAO MADAKTARI WAKAAMUA KUGOMA KUTUTIBU WANANCHI

SERIKALI INAWAFUKUZA MADAKTARI KWA KUGOMA KUWATIBU WANANCHI
SERIKALI INAWAFUKUZA KWA KUWA IMEWAJIRI MADAKTARI HAO

WANANCHI WAMEKIAJIRI CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) ILI KIUNDE SERIKALI ILIYOWAAJIRI MADAKTARI NA INAYOFUKUZA MADAKTARI KWA KUGOMA KUWATIBU WANANCHI WALIOIAJIRI SERIKALI.

JE WANANCHI WAFANYE NINI NA SERIKALI YA CCM WALIYOIAJIRI?

NAWAZA TU. KIZUNGUZUNGU TU.

3 comments:

Chimbuko Letu June 29, 2012 at 6:39 AM  

Jambo la msingi mimi naona wakae meza moja na kuzungumza upya kwa sababu kila mmoja ana haki ya kutetea jambo analolishikilia. Kwa kweli inasikitisha kwa kweli kwa sababu tunazidi kupunguza nguvu kazi kwa watoto,akina mama wajawazito na wanaume ambao ni mhimili katika familia zao na wamejazana mahospitalini ili wawezetibiwa,tuzidi kumomba Mola alinusuru hili balaa.

Adam June 29, 2012 at 7:03 AM  

Nakusoma kaka, mazungumzo yoyote yenye tija huelekea katika kuwezesha kila upande kutimiza wajibu wake. Na katika mazingira haya kunakuwa na mtoa haki na mpokea haki. Katika hili la Serikali na madaktari, serikali ndiyo DUTY BEARER. LAZIMA WATIMIZE WAJIBU.

SASA SERIKALI INAPOGOMA KUTEKELEZA MAKUBALIANO YAKE NA MADAKTARI, UMUHIMU WA MAZUNGUMZO UNATOKA WAPI? SUALA NI SERIKALI ITIMIZE YALE WALIYOKUBALIANA AMBAYO YALIMSHAWISHI RAIS WETU KUAMINI NA KUSEMA HAPO MWEZI FEBRUARI KUWA MGOMO UTABAKI HISTORIA. SASA JANA TENA SERIKALI IMEOMA KUTOA TAMKO. SIKIZA HAPA http://www.youtube.com/watch?v=H486e4S5rsk

Malenga June 29, 2012 at 12:46 PM  

Enzi za utawala wa Baba wa Taifa tulikuwa na wasomi wachache sana kwenye kada ya uongozi wa juu.

Lakini hekima zao zilikuwa hatua mia moja mbele kuliko hawa wasomi wetu tuliodhani kwamba tumewasomesha kuja kuliendeleza taifa hili.

Dawa ya CCM ni kukaa pembeni ijitathmini na kuanza upya. Mwisho unakaribia

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP