SERIKALI ITATUE MATATIZO SEKTA YA AFYA IACHE VITISHO
- Iongoze bajeti ya afya
- Ibane matumizi kwa kuacha kuongeza wilaya na mikoa na ivunje baadhi ya balozi zake nk.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya madaktari Dkt Steven Ulimboka akiwa amejeruhiwa vibaya |
Kuna
taarifa kwamba tayari serikali imeanza kuwafukuza kazi madaktari wanapigania
kuboreshwa kwa huduma za afya nchini ikiwa ni pamoja na maslahi yao. Mbali ya
kauli za vitisho zilizotolewa na viongozi wakuu wa serikali kuhusu migomo
hususan wa madaktari, serikali imeshindwa kusimamia wajibu wake.
Yangu
ni machache tu kuwa;
- Wajibu wa serikali ni kukusanya raslimali za nchi ikiwemo kodi na ushuru mbali mbali na kuzitumia raslimali hizo kutoa huduma zote za msingi kwa raia wan chi hiyo. Huduma ya afya ni msingi wa misingi yote.
- Wajibu wa wananchi ni kutoa hizo kodi, na kuzilinda na kuzitumia kwa uendelevu mali asili zilizopo kwenye maeneo yao.
- Kwa wataalam, kama madaktari walisomeshwa na serikali, sio kwa hisani bali katika kuwajibika kutimiza wajibu wake(serikali) wanawajibika KUTIMIZA WAJIBU wao na KUPIGANIA KUBORESHWA KWA MAZINGIRA YANAYOHITAJIKA ILI KUTIMIZA WAJIBU WAO.
Serikali
ibane matumizi yake na kuachana nay ale yasiyo ya lazima kama kuendelea
kuongeza mikoa na wilaya (ukoloni) badala ya halmashauri za wilaya, miji na
manispaa (tawala/serikali za wananchi), itimize wajibu wake kwa kutekeleza kile
kilichofanya madaktari wakubali kurudi kazini pale awali. Bora serikali
ikavunja hata balozi zake nyingine ambazo hazina tija kubwa katika kuiendesha
nchi hii (tubaki na zile za kimkakati tu). Serikali itenge bajeti ya kutosha
kwa huduma za afya ili kuung’oa mzizi wa fitna. Hakuna njia ya mkato.
Kuwafukuza
madaktari ni kuzidi kutoa hukumu ya kifo kwa watanzania tulio wengi. Je kama
haina fedha za kutosha kutimiza madai ya madaktari ya kuboresha huduma za afya,
itawezaje kutafuta madaktari mbadala ambao wengi ni ghali? SERIKALI IKOME KUTOA
VITISHO. WANAWEZA KUMUUA DKT MMOJA, LAKINI HAITAWEZA KUDHIBITI GHADHABU YA
WANANCHI INAYOZIDI KUONGEZEKA.
Kwa
kuhitimisha niungane na kauli ya Mbunge wangu wa Ubungo John Mnyika,
“Sababu ya hali
tete ya nchi na maisha ya wananchi kwenye sekta ya afya ni udhaifu wa serikali
na uzembe wa bunge. Rais Jakaya Kikwete ajitokeze alitangazie taifa kuunda tume
huru ya kuchunguza kutaka kuuwawa kwa Dk. Ulimboka Steven na kutoa ahadi ya
kuongeza fedha katika bajeti ya wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2012/2013 ili
kushughulikia chanzo cha mgogoro. Spika Anna Makinda aruhusu bunge litumie
mamlaka yake ya kuisimamia serikali kusuluhisha.”
0 comments:
Post a Comment