the Vicious cycle of MIGOMO YA MADAKTARI TANZANIA:
Serikali IMEGOMA. Madaktari WAMEGOMA. Wananchi TUMEGOMA! Hatari tupu
Serikali IMEGOMA kutimiza makubaliano yake na madaktari
katika kuboresha huduma za afya
Madaktari WAMEGOMA kutimiza wajibu wao wa watibu wananchi
Wananchi WAMEGOMA kutumia haki yao na mamlaka yao ya kuiwajibisha serikali kwa kugoma kuboresha
huduma za afya sambamba na makubaliano yake na madaktari.
Inabaki kuwa MIGOMO MIGOMO MIGOMO MIGOMOOOOOOO.
LAZIMA UWEPO
UPANDE WA KUANZA KUACHA KUGOMA, SERIKALI!
MADAI YA MADAKTARI:
Katibu wa Jumuiya hiyo, Dk Edwin Chitega alitaja madai yaliyowasilishwa katika kamati hiyo kuwa ni hali bora ya mazingira ya utoaji afya nchini, ongezeko la mishahara, posho za kufanya kazi katika mazingira magumu, posho za kufanya kazi katika mazingira hatarishi na posho za kuitwa kazini.
Akizungumzia dai la hali bora ya mazingira ya kazi, alisema hadi sasa hakuna kilichotekelezwa huku hali ya utoaji huduma kwa wagonjwa ikizidi kuwa mbaya.
“Tunaweza kusema tangu tukubali kuingia kwenye meza ya majadiliano hali imezidi kuwa mbaya. Katika hospitali kubwa kama Muhimbili inakosa vitendea kazi, dawa, wagonjwa kulazwa chini huku rufaa za wagonjwa kwenda nje ikiongezeka,” alisema Dk Chitega na kuongeza:
“Tunachotaka sisi ni huduma za afya ziboreshwe ili kuwezesha wananchi kupata huduma bora za afya na kupunguza rufaa za kwenda nje kutibiwa.”
Dk Chitega alitoa mfano wa gharama zilizotumika kwa mwaka wa fedha wa 2010/11, kuwa ni Sh7 bilioni, ilhali fedha zilizotumika kwa kipindi cha mwaka huu kwa ajili ya uendeshaji hospitali kubwa sita za hapa nchini kuwa Sh5 bilioni.
“Tulipendekeza pia mchakato wa rufaa uboreshwe kwa kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda nje kwa kuboresha huduma za ndani, Serikali ilianzisha Taasisi ya Mifupa (MOI), ikapeleka madaktari kwenda kusoma India, wamekuja kufanya kazi wamekosa vifaa wameondoka. Sisi lengo letu ni kuona fedha za nchi zinatumika kuwasaidia Watanzania,” alisema Chitega.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Dk Godbles Charles alisema taarifa zilizotolewa bungeni na Pinda na Dk Mwinyi zimepotoshwa na zina lengo la kuwarejesha kwenye mgomo. CHANZO: http://www.mwananchi.co.tz/habari/-/24108-madaktari-watangaza-mgomo-kesho

0 comments:
Post a Comment