Pekua/search

Thursday, July 5, 2012

MADAKTARI WANAPOMALIZA MGOMO; SERIKALI INAANZISHA MGOMO WAKE- MWISHO NINI? LINI?


Manung'uniko ya madaktari nchini hayajaanza leo.
Uduni wa huduma za afya nchini haujaanza leo. Tatizo ni mgomo wa serikali kisha wa madaktari. 


Madaktari wanapokubali kurejea kazini, serikali inaanzisha na kuendeleza mgomo dhidi ya uboreshaji wa maana wa huduma za afya. Madaktari wanavumilia, wakifika ukomo wanagoma, ndipo serikali inaanza tena jitihada za hapa na pale za kuzima moto. Wananchi daima dumu tuko kwenye mgomo wetu wa kushindwa kuiwajibisha serikali inayokusanya kodi zetu. Shame.

Sheria ya Kazi ya mwaka 2004 (Employment and Labour Relations Act, Kifungu cha 6: (20) (4)), kinaelekeza kuwa “Mwajiri atamlipa mwajiriwa walau 5% ya mshahara wa msingi wa mwajiriwa kwa kila saa aliyofanya kazi usiku’’.  Ndiyo kusema kwa wastani daktari angelipwa shilingi 47,000/= kwa saa anapofanya kazi usiku. Lakini cheki MWONGOZO WA SERIKALI Kumb. No. C/AC.17/45/01/F/73 wa tarehe 21 February 2012 kutoka kwa George D. Yambesi (Katibu Mkuu Utumishi) kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wenye kichwa, ‘Malipo ya kuitwa kufanya kazi baada ya saa za kazi (On call allowance)’ unaelekeza kulipa viwango vifuatavyo kwa siku kwa watumishi wa afya kuanzia tarehe 9 February 2012 (Siku 12 Nyuma);
·         Wataalamu bingwa Tshs 25,000/= na
·         madaktari wa kati Tshs 20,000/=.
 TAZAMA SASA  HII KWA WATUMISHI WENGINE:
Waraka wenye Kumb. No. C/AC.17/45/01/125 wa tarehe 11 Februari 2010 wenye kichwa ‘Waraka wa Utumishi wa Serikali Na.2 wa mwaka 2010: Posho ya vikao (Sitting Allowance) Serikalini,’ viwango ‘vipya’ vya posho ya vikao vilivyotajwa ni
·         Mwenyekiti/Katibu 200,000/=,
·         Wajumbe 150,000/=
·         na sekretarieti 100,000/=.
Hapo mshahara wanakuwa wamelipwa na nadhani haijalishi kikao kimefanyika wapi:ofisini hapo hapo au nje kidogo ya ofisi. Analipwa kwa ajili gani? KUKAA na kufanya kazi anayolipwa mshahara.


Mawazo ya msingi na data zimenyofolewa kutoka taarifa ya SIKIKA. Hamasika kusoma zaidi makala hiyo ufahamu kwa undani juu ya migomo ya madaktari na uduni wa huduma za afya nchini: http://www.sikika.or.tz/sw/publications/read.php?uid=235

0 comments:

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP