Kwanini Sophia Simba Anampongeza Rose Kamili kwa kumpinga Slaa Kuoa?
Kwanini Wanampongeza Rose Kamili kwa kumpinga Slaa Kumwoa Josephine Mushumbusi?
- Je ni kwa sababu wanaunga mkono harakati za mwanamke mwenzao kulinda ndoa yake?
- Je ni kwa vile wanamtakia mema Rose Kamili?
- Je ni kwa kuwa wao ni makada wa CCM na wanaamini kuwa kesi hii itamfunga spidi gavana ndg .Slaa katika kukimbiza chama chao?
CAPTION INASOMEKA: "Waziri wa Maendeleo
ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba na Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Ester
Bulaya wakimpongeza Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Rose Kamili (kulia) katika
Viwanja vya Bunge jana baada ya kupata taarifa kuwa Rose amefungua kesi ya
kuzuia ndoa ya aliyekuwa mumewe, Katibu Mkuu wa Chadema,Dk Willibrod Slaa
inayotarajiwa kufungwa Julai 21. Picha na Edwin Mjwahuzi" chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/component/content/article/37-tanzania-top-news-story/24703-ndoa-ya-slaa-njia-panda.html
2 comments:
si huyu Sophia aliwahi sema kama mumeo si ccm usimpe unyumba? what else do you expect of her?
Ni kweli kabisa. Hizi harakati na uchama chama sijui tutaishia wapi nazo
Post a Comment