Serikali haikuwa na sababu ya kumdhuru Ulimboka?
Serikali haikuwa na sababu ya kumdhuru Ulimboka?
- Hoja ya kushirikiana naye haina mashiko
- Ushirikiano haukuzaa matunda
- Kuwatisha madaktari si sababu ndogo kwa serikali.
“Kama
nilivyosema awali, sioni sababu ya serikali kuhusika na kipigo cha Ulimboka
ambaye tulikuwa tukishirikiana naye vizuri kwenye vikao vya majadiliano,” Pinda
akijibu Swali la Freeman Freeman Aikaeli Mbowe, jana Alhamis Julai 5 2012.
Kwa
mujibu wa nukuu ya gazeti la Tanzania Daima Julai 6 2012, Mbowe alisema , “Kwa
kuwa kumekuwa na ongezeko la matukio ya mauaji kwa raia wasio na hatia na
kumekuwa na hisia kwamba matendo hayo yanafanywa na Jeshi la Polisi. Mfano wa
matukio hayo ni pamoja na lile la kupigwa kwa wabunge wawili na hili la hivi
karibuni la kutekwa kwa Dk. Ulimboka, tukio ambalo limelichafua taifa; je,
serikali iko tayari kuunda tume huru kuchunguza matukio hayo?”
Ndipo
Waziri Mkuu alipotoa maelezo hayo na pia alisema “Mh. Mbowe, kwanza tukio la
Ulimboka sio mfano mzuri sana kwa sababu hakuna mwenye ushahidi wa serikali
kuhusika kumteka na kumpiga Dk. Ulimboka...”
Katika hali ya kawaida maelezo ya Mheshimiwa
Waziri Mkuu yanaleta maana. Lakini sio katika hali yenye uvulivuli, ilojaa utusitusi na utata. Bado
ziko sababu nyingi na znye mashiko zinazotusukuma kina sisi tunaoamini kuwa serikali, wakala wake au mtumishi aliyekuwa katika kutekeleza
majukumu yake ya kutumwa na serikali wanazosababu za kutaka kumfanyia
walichomfanyia dkt Ulimboka.
Hoja ya
kushirikiana naye ingekuwa na mashiko iwapo tu ingezaa muafaka. Lakini sasa
muafaka haukupatikana, na kumfanya Ulimboka aendelee kuonekana mwiba. Hiyo sababu
ya kwanza. Lakini pia wiki lililotangulia waziri mkuu alitamka bayana kwamba
mjadala na mbinu za kimahakama zinaelekea kukwama na hivyo serikali ikasema
LITAKALOKUWA NA LIWE! Lipi hilo? Tunakosea vipi kuamini hilo ni moja wapo la
kuwanyamazisha madaktari.
Ikohoja
pia ya watawala duniani kutumia mabavu pale wanapoishiwa au hoja zao kuzidiwa
na upande wa pili. VITISHO. Hili linaweza kuwa sababu kubwa kabisa ya kutaka kumzimisha msemaje, nap
engine mwenye msimamo binafsi usioyumba ikiwa pia ni njia ya kuwatisha wengine.
Kuna wakati moto huweza kuzimwa kwa mafuta ya taa.
Kama
ambavyo watu wengi wameeleza, inawezekana mtumishi wa dola mmoja aliagizwa kutafuta
habari kutoka kwa ulimboka kuhusiana na mgomo, baada ya kuzikosa akatumia nguvu
kujaribu kuzipata, hilo nalo ni zito sana tu. Kwanini serikali ina pre empty?
Kwanini
serikali inaendelea kukana kuhusika ilhali uchunguzi haujafanyika? Sawa, hakuna
mwenye hatia kabla ya kuthibitishwa, lkn pale mchunguzi anapokuwa mtuhumiwa
mwenyewe natural justice hii inapoteza maana. Kwanini serikali inapata
kigugumizi kuhusu kuunda tume huru?
Natamani
kukaa kimya. ILA ROHO INAUMA. INAUMA
SANA.
0 comments:
Post a Comment