Mwigulu Nchemba Aonywa: Asiwe Msemaji wa CHADEMA, Selasini
SELASINI ASEMA;
- Sijawahi kumwajiri Mwigulu Nchemba kuwa msemaji wangu!.
- Mwigulu Nchemba si mkweli na hajui chochote kuhusu mimi wala CHADEMA.
- Mwigulu Nchemba anataka nionekane sina shukrani kwa viongozi na Chama changu kwa Umoja na Ushirikiano wanaoendelea kunipatia hata sasa.
- Viongozi wangu wanafuatilia kwa karibu sana matibabu yangu na Mke wangu.
Ni baada ya Mwigulu Nchemba kuripotiwa kutangaza
kuwa CHADEMA kimemtupa, hakina msaada wala Ushirikiano Joseph Selani, Mbunge wa
Rombo kupitia CHADEMA na na mimi kwenye Matatizo yaliyojitokeza. Soma tarifa
kamili:
"TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA UZUSHI
UNAOENEZWA NA MH.MWIGULU NCHEMBA JUU YANGU NA CHAMA CHANGU.
Ndugu zangu
kwanza nachukua nafasi hii kuendelea kumshukuru Mungu kwa afya njema
anayoendelea kunijalia mimi na Mke wangu hapa Hospitali ya KCMC. Pia
niwashukuru wote walionifariji/wanaoendelea kunifariji katika kipindi chote cha
matatizo yaliyotokea.
UTANGULIZI.
Itakumbukwa
kuwa tarehe 28/05/2012 nilipata mbaya ya gari. Ajali hiyo ilitokea maeneo ya
Boma karibu na chuo cha VETA. Watu wa kwanza kufika kwenye Eneo la ajali na
kutupa msaada walikuwa ni Askari Polisi waliokuwa Doria karibu na eneo lile na
Raia waliofika wa pia walikuwemo MWENYEKITI WA CHADEMA (W) YA HAI pamoja na
MWENYEKITI WA BAVICHA (W) YA HAI. Walisaidiana na Polisi kuchukua majeruhi
(Mimi nikiwemo) pamoja na marehemu waliofariki pale hadi Hospitalini.
Baada ya
kufika hospitalini pia walifika MHE.MEYA WA MANISPAA YA MOSHI (AMBAYE PIA NI
DIWANI WA CHADEMA) akiongozana na baadhi ya VIONGOZI WA CHADEMA WA KATA YAKE NA
BAADHI YA MAENEO YA MOSHI MJINI.. Baadaye alifika KATIBU WA CHADEMA MKOA WA
KILIMANJARO AKIONGOZANA NA BAADHI YA MADIWANI WA CHADEMA WA MOSHI NA ARUSHA na
Viongozi wengine ambapo nakumbuka walitokea Wilaya ya Mwanga kwenye Mikutano ya
Hadhara. Tulikuwa wote hadi tunapatiwa huduma na majeruhi tukapelekwa Wodini.
Siku iliyofuata nilipokea Simu kutoka kwa MHE. FREEMAN MBOWE (MWENYEKITI WA
CHADEMA NA KIONGOZI WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI) akiwa Mtwara kwa shughuli za
Chama akinipa Pole kwa yaliyotokea na kunifariji.
Baadaye hali
yangu ilipoimarika kidogo tukapanga taratibu za mazishi ya Marehemu Mama yangu
Mzazi (R.I.P) na miongoni mwa watu waliohudhuria kwanza ni WANACHAMA WA
CHADEMA, MADIWANI WOTE WA CHADEMA ARUSHA, MADIWANI WA MOSHI MJINI NA MOSHI
VIJIJINI. Kutoka makao makuu ya CHADEMA waliwakilishwa na Mhe.Rwakatare na
Ndg.Anthony Komu (Mkurugenzi wa Fedha na Utawala) Pia walihudhuria Baadhi ya
WWABUNGE WA CHADEMA wakieleza sababu za viongozi na wabunge wengine
kutokuhudhuria (Na zilikuwa Sababu za Msingi kabisa) kwa sababu hata baadhi ya
viongozi wa serikali waliohudhuria walileta salam za wakubwa wao ambao nao
walitamani kuhudhuria lakini kutokana na sababu mbali mbali walishindwa!..
Pamoja na
hayo,MHAMA JOSEPHINE MUSHUMBUSI (MKE WA MHE.KATIBU MKUU WA CHADEMA)
alinitembelea hospitalini akiwa na wajumbe kadhaa... Aliniletea salam za pole
kutoka kwa KATIBU WANGU MKUU WA CHAMA. Nilifarijika sana kuona kuwa kiongozi
wangu pamoja na kuwepo kwake safarini kikazi lakini bado aliweza kutuma ujumbe
kwangu..
Baadaye
nilihamishiwa MOI (Muhimbili) kwa ajili ya matibabu Zaidi. Nakumbuka walifika
wabunge wengi sana wa CHADEMA lakini kubwa zaidi alifika MHE.FREEMAN MBOWE
(MWENYEKITI WA CHADEMA KIONGOZI WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI).
KANUSHO.
Nimekuwa
nikisikia kwenye vyombo vya habari kuwa Mwigulu Nchemba (Mb-CCM) Anatangaza
kuwa Chama changu kimenitupa na hakina msaada wala Ushirikiano na mimi kwenye
Matatizo yaliyojitokeza..
Kwanza:
Sijawahi kumwajiri Mwigulu Nchemba kuwa msemaji wangu!.
Pili:
Mwigulu Nchemba si mkweli na hajui chochote kuhusu mimi wala CHADEMA.
Tatu:
Mwigulu Nchemba anataka nionekane sina shukrani kwa viongozi na Chama changu
kwa Umoja na Ushirikiano wanaoendelea kunipatia hata sasa.
Nne:
Viongozi wangu wanafuatilia kwa karibu sana matibabu yangu na Mke wangu.
MWISHO:
Naomba
Mwigulu aelewe kuwa sitaki malumbano yasiyo na Tija kwangu wala kwa Wananchi
wangu Walionichagua. Pia nisingependa kumtaja Marehemu Mama Yangu (R.I.P) kabla
hata ya Arobaini. Zaidi ya yote akumbuke kuwa Viongozi na Wabunge wa CHADEMA
wana mambo mengi ya kufanya na hawatakuwa tayari tena kujibu uongo na uzushi
DHAIFU kama aliouzusha!!.
Ahsanteni
Sana,
Mungu
aendelee kuwabariki.
Joseph
Selasini
(Mb)
Rombo-CHADEMA."
0 comments:
Post a Comment