Pekua/search

Wednesday, April 3, 2013

Kukosoa serikali si uchochezi, ni uzalendo zaidi ya kusifia upuuzi!
Kukosoa serikali si uchochezi, ni uzalendo zaidi ya kusifia upuuzi!
Katika kuendelea kujaribu kufuta ujinga, nimekutana nah ii kitu ina kurasa 138 hivi inaitwa KANUNI YA ADHABU (Sheria Kuu). Nakuta maelezo hapa yanayohusu mambo ya uchochezi. Hapa naona kizunguzungu kabisa. Lakini, licha ya makandokando yake habari hii, nafika sehemu ifuatayo kidogo inanipa mwangaza zaidi. Natushirikiane hapa:

Kif. 19; Sura 500 Kif. 36

(2) Kitendo, hotuba au tangazo halitahesabiwa kuwa ni la kichochezi kwa sababu tu linalenga katika:-
(a) kuonyesha kwamba serikali imepotoka au imekosea katika mwenendo wake wowote; au
(b) kuonyesha makosa au mapungufu katika serikali au Katiba ya Jamhuri ya Muungano au kama ilivyowekwa na sheria, au katika usimamiaji utoaji wa haki kwa lengo kurekebisha makosa hayo au upungufu huo; au
(c) kuwashawishi wakati wowote wakazi wa Jamhuri ya Muungano kujaribu kwa njia ya halali kuleta megeuzo ya jambo lolote katika Jamhuri ya Muungano kama ilivyowekwa kwa sheria; au
(d) kuonyesha, kwa nia ya kuvifuta, mambo yoyote yanayoleta au yenye mwelekeo wa kujenga hisia za nia mbaya na uadui baina ya aina mbali mbali za watu wa Jamhuri ya Muungano.

Elimu haina mwisho.

0 comments:

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP