CCM Kitaachwa kiwakumbatie Mafisadi mpaka lini?
CCM Kitaachwa
kiwakumbatie Mafisadi mpaka lini?
Wengi wameshitushwa na habari iliyotolewa na gazeti la
Tanzania Daima la Alhamisi tarehe 4 Aprili mwaka huu kuwa kamanda wa upambanaji dhidi ya
ufisadi Dkt Harrison Mwakyembe naye ni fisadi (http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=47479
). Bahati nzuri chama cha mapinduzi CCM kupitia katibu wake
mwenezi Nape Nnaye kimejibu tuhuma hizo
na kusisitiza kwamba zabuni hata haijapewa kampuni ya chama hicho bado. Lipi ni sahihi tunaendelea kuchakata kwenye mbongo zetu na waandishi wa habari uchunguzi watatujuza inshallah.
Katika taarifa ya Nnauye aliyoitoa kwa vyombo vya habari
anaeleza yafuatayo,
“Lakini tunazo taarifa kuwa uongo
huu wamelishwa na baadhi ya mafisadi waliotakakutumia eneo hili la CCM kujaribu
kukaa katikati ya mwekezaji yeyote atakayejitokeza na Jitegemee kwa lengo la
kujinufaisha wao binafsi. Na huu ni mwendelezo waChadema kutumiwa na mafisadi
katika kutimiza mambo yao.”...anahitimisha taarifa hiyo kwa kusema, “Tunawataka
wasikatishwe (wizara ya uchukuzi chini ya Mwakyembe) tamaa na mafisadi wachache,wachape kazi kwa
uzalendo huohuo waliouonesha.”
Kwa mujibu wa taarifa hiyo kwa mara
nyingine CCM kinaeleza waziwazi kuwa kinawafahamu mafisadi na kwamba kinajua
kuwa mafisadi wamekuwa wakikitumia CHADEMA. Hawa mafisadi ni kina nani? Wako chama
gani? Yawezekana wakawa chama chochote ama hawana chama kabisa, lakini je CCM ambacho ni chama tawala pamoja na serikali
yake kinafaidika vipi kwa kuwatazama tu hawa mafisadi? Kitaendelea kuwafuga
hata lini? Najiuliza tu.
Wakati umefika wa
moja ya mambo haya kufanyika;
(i)
CCM
kuiagiza serikali yake kuwashughulikia mafisadi au
Watanzania kukiwajibisha chama hiki kwa kukumbatia
mafisadi
0 comments:
Post a Comment